Somo: Maana halisi ya neno linalotumiwa na Wasanii wa kizazi kipya FREE STYLE.

Kwa hyo wanaosema Mheshimiwa hotuba zake ni freestyle kumbe hawajakosea
Ikiwa amezungumza bila kuzingatia sheria na taratibu za hotuba basi wapo sahihi kabisa ila iwapo amezingatia hawapo sahihi

Japo katika hotuba hakuna Neno la Hotuba huru (free style spech)
 
Yaani mimi huwa naona bandiko halina maana. Nikiona mtu anayejitapa kufundisha halafu ndani ya maelezo yake kunakuwa na makosa mengi.
Mfano: Unaposema nyimbo badala ya wimbo moja kwa moja hoja yako yote ni mfu.
Ukitaka kuelimisha hakikisha mambo yote yanakuwa sawa.
This thread is useless
Chukua hilo kosa lake na wewe ulete Uzi kwa lengo la kuelimisha mana hata yeye co mjuzi wa kila neno la kiswahili.
 
Mkuu nadhani hakuna aliekamilika kikubwa na cha msingi ujumbe wangu umefika na wachache wamenielewa ninacholenga ila sijajua unamaanisha nini pale unaposema ninajitapa

Kujitapa= maana yake nini? hapa nilichokiandika kinaeleweka hata na mtoto wa darasa la kwanza sasa unadai najitapa sjajua wewe ulitaka iweje??
Mkuu ww chapa kazi achana na huyo jamaa anaejaribu kukudis.ni hulka ya mtu asiependa kujifunza na kubadilika na matokeo yake ndio kama hayo yakutaka wengine wawe kama yy .uzandiki,chuki,wivu na husda ndio vimejaa moyoni mwake...
 
Mkuu ww chapa kazi achana na huyo jamaa anaejaribu kukudis.ni hulka ya mtu asiependa kujifunza na kubadilika na matokeo yake ndio kama hayo yakutaka wengine wawe kama yy .uzandiki,chuki,wivu na husda ndio vimejaa moyoni mwake...
PmojaMkuu tunapokuw tunajifunza huwa tunakubali kukosolewa ila inashangaza msomi anakosoa kitu pasipokuonesha kosa au usahihi wa jambo analotaka watu waliamini

Sasa sijui anataka watu wakae upande upi na waamini nini?

Hii ndio Tanzania nchi ya Viwanda!

Ikiwa umekosoa mtu bila kuweka sababu basi wewe hujui bali utakuwa M'bishi tu!
 
PmojaMkuu tunapokuw tunajifunza huwa tunakubali kukosolewa ila inashangaza msomi anakosoa kitu pasipokuonesha kosa au usahihi wa jambo analotaka watu waliamini

Sasa sijui anataka watu wakae upande upi na waamini nini?

Hii ndio Tanzania nchi ya Viwanda!

Ikiwa umekosoa mtu bila kuweka sababu basi wewe hujui bali utakuwa M'bishi tu!
ndio viwanda hivyo mkuu.
 
Habari wakuu Leo naomba nitoe somo kidogo kuhusu maana ya neno FREE STYLE...Kwa wachache Wasiojua,

FREE STYLE ni neno linalotokana na Bleending word formation fomular,

Yaani ni neno linalotokana na muungano wa maneno mawili tofauti, yanayoungana na kuunda neno moja, kwa kiswahili mfumo huu tunauita njia ya "kuambatanisha maneno"

Yaani neno FREE lenye maana ya huru, na

STYLE lenye maana ya Mtindo..

ambapo kijumla tunaweza kuita ni mtindo huru (free style)

Ambapo mtindo huru katika swala la uandishi wa ushairi,

ambao wimbo ni moja ya kipera cha ushairi, Mtindo huru hutumika (Free style) Maana halisi ya Mtindo huru (Free style) inamaanisha mtindo wa kutunga shairi ambalo halifungamani na kanuni na sheria pamoja na taratibu za uandishi wa ushairi na ndio maana halisi ya neno Mtindo huru (free style)...

Nimeamua kutoa somo hili baada ya kusikia Mtangazaji mmoja akipotosha umma kuhusiana na Dhana ya Free style, akiwa na maana kuwa free style huimbwa na wana hip hop tu!

Pia wengi hapa wanachanganya mambo kwani wanaamini kuwa free style ni Uimbaji unahusisha tungo za papo kwa papo kitu (Mceiing) ambacho si kweli...

Ukweli nikwamba unaweza kuandika wimbo wako na bado ukawa umetumia mtindo huru yaani (free style) pale tu utakapokuwa hujazingatia sheria, kanuni na taratibu za uandishi wa Shairi/ wimbo ambazo zinafahamika kuwa ni utosherevu na uzingatiaji wa vina na mizani,

Naomba ifahamike kuwa waimbaji karibia wote wa nyimbo za kizazi kipya wanaimba mziki wa Free style....

Mfano nyimbo nyingi za Msanii Diamond ni za aina ya Free style na pia ni miongoni wa Wasanii wanaoimba free style...

Naomba atakaepinga aje na vigezo vya kiisimu katika lugha,..

Hivyo ni vyema tukatambua kuwa wasanii wanaotunga nyimbo zao papo kwa papo hatuwaiti magwiji wa free style, maana ikiwa ametunga papo na kwa papo na amezingatia sheria za utunzi wa shairi basi utenzi huo hautoitwa Free style wala yeye hawezi kuitwa mtunzi wa Free style...

Kiisimu inaruhusiwa kukopa neno kama lilivyo katika lugha moja na likatumiwa katika lugha nyingine ila neno hili la Free style lina maaana katika kiswahili hivyo haliwezi kusimamia maana ya utunzi wa papo kwa papo.

Somo la leo By Mwl Youngtozy!
 
Back
Top Bottom