Somo la Uraia kutofautisha ziara ya kichama na kiserikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Somo la Uraia kutofautisha ziara ya kichama na kiserikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiondoka Chakechake baada ya kuweka jiwe la Msingi
  katika Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga
  .

  Wananchi wengi hawafahamu tofauti ya ziara za viongozi ni ipi ya kichama na ipi ya kiserikali. Viongozi nao wanapaswa kubeba lawama kwa kutotoa elimu hiyo kwa wananchi na kubaki bubu hata mambo yanapokuwa hadharani ya kichama wakati ni ziara ya kiserikali inayowahusu wananchi wote. Ni busara ya kawaida tu ambayo viongozi wanapaswa kuifanya kutoa elimu hiyo lakini it looks like government officers are missing something in common sense.
   
 2. N

  Njele JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM siasa ya chama kote kote, vigumu kuelewa hawa waliotoka kwenye mfumo wa chama kimoja kushika hatamu za uongozi kutofautisha kwa kiwango unachofikiria wewe
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, hivyo hatushangai kuona mambo hayo kwa vile yameandaliwa na wanaCCM wenyewe, nguo zimegawiwa nao kabla ya mikutano sasa elimu gani ya uraia watayotoa inayopingana na ideology yao?
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Kwa vyo vyote mimi binafsi sipendezwi na hulka ya uchama tunapokuwa katika mikusanyiko inayowakutanisha watu wa itikadi mbalimbali na tofauti. Hapa tunahitaji kutanguliza utaifa ndio umoja utaimarika. Itikadi za kichama ni kipindi cha kampeni kwa vile ni wakati wa kunadi sera, kwa sasa ni utendaji unaohitajika.

  Kutanguliza uchama ni ufinyu wa upeo wa kufikiri. Ndio maana unaona uchama hauna manufaa zaidi ila sera kwani kwa sasa sera zinazotekelezeka ni za vyama vyote vya siasa kama Katiba mpya sera ya chama cha upinzani. Sasa tunatakiwa kuunganisha nguvu.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na hili ndilo linalo waua kisisa kila mara kiongozi mkuu wa serkali anapotembelea mahali lazima wavae manguo yao kijani mkutano mzima watu wengi tunashindwa kutofautisha ipi ni mikutano ya NAPE na ipi ya SERIKALI

   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wanachotakiwa ni viongozi wenyewe wa kitaifa kutamka hadharani ili kuwaelimisha wananchi, lakini kumezea ni dalili za wao kuandaa mazingira hayo ambayo yanafanya wasogelewe na wa kijani tu na wananchi walio wengi ambao hawana itikadi za kichama watasepa.
   
 8. k

  kipinduka Senior Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona humuuliz padri kila sehemu magwanda,
   
 9. k

  kipinduka Senior Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hv unajua itifak we
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nisingeifahamu ningekuwekea tathmini hyo ya upembuzi wangu kwa mwono wa kitaifa> Itifaki ni mlengo wa kimatabaka na mimi nipo katika mlengo wa umoja wa kitafia na mshikamano wa kitaifa.
   
Loading...