Somo la uraia kufundishwa kwa kiingereza ni kupotoka au ni usanii?

Danyel

Member
Sep 2, 2011
10
4
nimesoma malengo ya somo la civics(uraia) kwa shule za sekondari na nimegundua hakuna sababu hata moja ya msingi ya kwanini somo hilo lifundishwe kwa kiingereza.zaidi ya 98% ya mambo yanayofundishwa ni ya kitaifa.huwa najiuliza, kwani somo hili ni kwa maslahi nani?kama ni kwa maslahi yetu,lugha yetu watanzania ni kiswahili.kwa kutumia kiingereza kamwe malengo ya somo hayatafikiwa!!
somo hili kufundishwa kwa kiingereza ni kutunyima wananchi haki yetu ya kujua mamba ya msingi ya taifa letu.lakini endapo litafundishwa kwa kiswahili ufaulu utaongezeka na wanafunzi watakuwa wanapata kitu cha kurudi nacho 'uswahilini'.
fikiria mambo kama haki na wajibu wa raia,umuhimu wa vitambulisho vya uraia,sheria na kanuni za uchaguzi,maswala ya vyama vingi,shughuli za serikali,bunge na mahakama yote ni kwa ajili yetu.ukweli ni huu,hata kama hawataki elimu ya sekondari ifundishwe kwa kiswahili,kwa somo la uraia sioni kama kuna mjadala kwani kwa kutumia akili za kawaida kabisa somo hili linastahili kufundishwa kwa lugha ya taifa(kiswahili).
Angalizo;kabla ya mfumo wa vyama vingi somo hili lilikuwa linaitwa siasa lilikuwa linafundishwa kwa kiswahili na lilikuwa na tija kubwa sana.nashawishika kuamini kuwa kama si kupotoka basi ni mpango wa kuichelewesha elimu ya uraia kwa raia ili wachelewe kutoka madarakani, kwani kadiri elimu ya uraia inavyoenea ndiyo hali yao inavyozidi kuwa mbaya.shukurani kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za jamii kwa kujitolea kutoa elimu ya uraia kwa kiswahili kwani yale ambayo tulikuwa hatuyaelewi tulipokuwa shuleni leo hii tunayaelewa tukiwa uswahilini!
elimu yenu ina tija kubwa kwa kuwa mnaitoa kwa lugha sahihi,siku hizi haki haziombwi zinadaiwa hadi vijijini,hakika ukombozi unakuja!
wakati umefika sasa somo la uraia litambuliwe rasmi kwenye katiba na lifundishwe kwa kiswahili(lugha ya taifa).
TAFAKARI!!!!!
 
Back
Top Bottom