Somo la ujasiriamali mali lipewe kipaumbele mashuleni pamoja na vyuoni nchini Tanzania ili kupunguza changamoto za ajira kwa vijana

Livingson1

Member
Jul 13, 2021
30
26
Ujasiriamali ni jinsi ya kubaini matatizo au changamoto zilizopo kwenye jamii husika na kuzitatua changamoto hizo kwa kubuni mbinu ama vitu ambavyo vitapunguza ama kumaliza kabisa changamoto hizo kwenye jamii mfano kuchimba visima kuanzisha kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa kuku, mbuzi , n.k

Somo hili likianzishwa shuleni ama vyuoni linaweza kusaidia vijana wanaomaliza vyuo kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa
Ajira.

Mjasiriamali anaweza pia kutoa ajira kwa wananchi wa sehemu husika mfano mfugaji wa kuku anaweza kutoa ajira kwa vijana mahali husika

Elimu kwa vitendo. Baada ya kijana kupata elimu chuoni na kuweza kujiajiri anaweza kuanza kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watu wanaomzunguka

Kuongezeka kwa pato la mtu binafsi na serikali kwa ujumla. Hii ni baada ya mjasiriamali kuuza bidhaa zake atapata faida lakini pia atalipa kodi hivyo kusaidia serikali kupata kipato kupitia kodi


Kupungua kwa njaa. Baada ya kuzalisha bidhaa hizo mfano mifugo mazao watu watajipatia chakula lakini pia baada ya kupata kipato mtu ataweza kununua chakula kwaajili yake yeye na familia yake
 
Back
Top Bottom