Somo la TEHAMA linafundishwa shule za Msingi, kwa nini Sekondari halifundishwi?

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,121
2,064
Hapa kuna mkang'anyiko wa Malengo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Shule za Msingi wanafunzi wanafundishwa somo la TEHAMA. Angalau nadharia wanayotoka nayo huko Msingi ingeliendelezwa pale wanapofika Sekondari lakini ukweli ni kwamba Shule nyingi za Sekondari, hasa za SERIKALI hakuna hata dalili za kuanza mchakato wa kufundishwa Somo hilo.

Masuala mengine kama haya ni ubunifu tu wa kujiongeza. Sio mpaka Rais aseme ndo Mawaziri na Makatibu wakuu wazinduke usingizini. Ulimwengu wa Sasa ni ajabu sana mtu kujifunza BASIC COMPUTER SKILLS/KNOWLEDGE akiwa mwaka wa kwanza Chuo kikuu. Mhitimu wa Kudato cha Sita wa sasa anafika chuo mwaka wa kwanza ndo anashangaa kusikia kwamba kuna kitu kinaitwa HARDWARE & SOFTWARE halafu anaenda kuyachanganya na softcopy & hardcopy.

Huyo ni mwanafunzi wa University level. Kimsingi mambo haya ya basic knowledge of computer yalitakuwa kuishia kwenye elimu ya Msingi. Huko ndo mwanafunzi ajifunze kutambua components of computer.

Ni wakati sasa Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Wizara ya Technology wajitafakari kuhusu mustakabali wa wanafunzi hasa kwenye masuala ya TEHAMA.
 
Magufuli kasema wanafunzi wa PCM na PCB wasome history tena kwa kiswahili alafu wewe unataka kuleta mambo ya computer! Utakua umetumwa na mabeberu wewe...

(Mkuu hii nchi ukiiwaza sana utachanganyikiwa).
 
Back
Top Bottom