Somo la nchi ya China kwa maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,919
2,000
Baada ya chama cha Kikomunisti cha China kushindwa kutimiza ndoto za Wachina baada ya kukumbatia sera za Mzee Mao kwa muda mrefu bila mafanikio, chama kilijikuta kimegawanyika katika kambi mbili, Moja ikiwa ni kambi ya Zidumu fikra za Mwenyekiti Mao, na kambi nyingine ikiwa ni wana mageuzi.
Miongoni mwa matokeo ya mnyukano huo ni uamuzi wa kuhakikisha kuwa hapana mtu mmoja ndani ya China ambaye yeye ndiyo kila kitu, kwa hiyo chama kikaanza kusambaza madaraka makubwa ya chama na serikali kwa mtu watu tofauti tofauti. Matokeo yake Mzee Deng Xiaoping akajikuta ana dhamana ya Kusimamia Jeshi la China, Wakati huo raisi alikuwa ni mtu mwingine, na Waziri mkuu alikuwa ni mtu mwingine.
Wazee wa chama hata hivyo waliamua kwamba Mzee Deng Xiaoping ndiye awe kiongozi mkuu wa nchi japo kuwa raisi na Waziri mkuu kwa mujibu wa chama cha Kikomunisti walikuwepo pia.

Miongoni mwa mambo aliyoyafanya Mzee Deng Xiaoping ni kumteua Mkuu wa Jimbo la Sichuan aitwaye Zhao Ziyan, mtu ambaye kwa mara ya kwanza na uthubutu wa kutosha aliruhusu katika jimbo hilo la Sicjuan baadhi ya sera zilizokuwa kinyume cha sera za Chama Chake cha CCP kwa mfano aliruhusu wachina kujilimia mashamba yao wenyewe, tofauti na awali walipotakiwa kulima kiujamaa, pia akaweka uwazi zaidi katika maamuzi ya serikali, Sera za huyu bwana Zhao Ziyang zikasababisha mazao ya kilimo baada ya miaka mitatu kukua kwa zaidi ya asilimia 50, na uzalishaji viwandani kukua kwa zaidi ya asilimia 81 ndani ya miaka hiyo.
Kutokana na mafanikio hayo ya Jimbo la Sichuan, Mzee Deng Xiaoping akaamua kuwa Model ya kiuchumi ya Sichuan ndo itakuwa njia ya kiuchumi ya nchi nzima!
Kwa hiyo Mzee Deng Xiaoping akaamua kumchukua bwana Zhao Ziyang na kumpa nyadhifa za Uwaziri mkuu ili awe msimamizi wa mabadiriko ya kiuchumi China, na kuachana na sera za kiuchumi zilizofeli za mzee Mao!. Bwana Ziyang hakumuangusha Mzee Deng, akaanzisha special economic zones katika miji ya mwambao, akaongeza uwazi serikalini, akahimiza kuchukua mazuri ya magharibi na kuyafanyia kazi, kiufupi alifikia hatua hata ya kujaribu kukitenganisha chama na serikali, kwamba chama kiwe chama na serikali iwe serikali japo hatua hii iliwakera sana wahafidhina hadi kufikia kumuundia zengwe la kisiasa!

Kwetu sisi hapa Tanzania tunaweza kujifunza kupitia China, ni lazima tuweze kuidentify watu wenye uweze wa kuturn around situation zetu!.

Mimi ninaamini kwa dhati kabisa kuwa inayohusika na Fedha uchumi na mipango inamfaa mtu wa Calibre ya Dr Dau. Huyu ni mtu aliyefanya kitu kinachoonekana, ni mtu mwenye vision na uwezo wa kudeliver. Naweza kusema kuwa Dr Dau anaweza kuwa Zhao Ziyang wa Tanzania.
Sote tulishuhudia namna ambavyo NSSF ilivyokuwa, na hadi pale alipoifikisha, miradi na vision aliyoiweka, ni dhahiri Dr Dau anafaa kuwa msaidizi mkuu wa Raisi wetu ili kumsaidia na kulisaidia Taifa kuimplement vision ya mheshimiwa raisi ktk viwanda.
Sipigi debe na wala simpigiagi mtu yeyote debe, bali nazungumza based on merit, based na uwezo wa kudeliver. Kama leo tunataka kucatapult nchi yetu kuingia zama mpya za uzalishaji basi tuwape nafasi watu ambao wamefanya kitu, kiaonekana, Dr Dau anafaa kumreplace Dr Mpango ASAP!
 

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,745
2,000
asante mkuu.
ila haujamalizia zhao ziyang aliishia jela hadi anakufa 2005 sababu kubwa zaidi ya kutofautina na wenzake juu ya waandamanaji kuuwawa lkn pia kichinichini alikuwa anatafutwa atolewe kwenye system maana alitaka kugusa maslahi ya wazee wachache pale chamani. ila atabaki kuwa role model wa mabadiliko duniani.
 

Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,629
2,000
Hivi Dr Dau si ana tuhuma nyingi tu za wizi, ubadhilifu na matumizi mabaya ya rasilimali!?
Je lengo la NSSF kulipa wastaafu lilikuwa linafanyika!? Au walijenga majengo tu wakati wenye pesa zao hawalipwi.
Pili at least angekuwa mkuu wa mkoa akaufanya mkoa wake uende mbele ingeweza kuwa kigezo cha kumpa sekta fulani, kuongoza tasisi moja ya watu ofisini ni tofaut na kuongoza wilaya tuu.
Sijakubaliana na hoja ya Dr Dau
 

lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,005
2,000
Maendeleo ya nchi yana msingi katika fikra za wananchi walio wengi na siyo viongozi. Utamaduni wa wachina wa kuwa aggressive na kufanya kazi kwa bidii na maarifa bila urasimu ndicho cha kuiga.
Nadharia nyingi za viongozi hazizai matunda kama wananchi wao hawajitumi kifikra na vitendo. Viongozi hupita lakini taifa huendelea kuwepo.
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,919
2,000
Mambo waliyoyafanya wachina ndani ya miaka 300 ni maajabu!
Lakini mafanikio hayo yalikuja baada ya mnyukano mkali wa kifikra ndani ya chama chao
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,406
2,000
Wachina hawana Huruma na watanzania kabisa, Tanganyika ni koloni la china na dampo la kutupa bidhaa zake feki

Example: Shati la Turkey ni elfu 30, na linadumu zaidi ya miaka 4 bila kufubaa rangi wala kuchanika

Shati la china ni linauzwa kati ya elfu 15 na 20...jepesi na mwaka mmoja tu limepauka,

Simu feki

pembe za ndovu

Na hawana misaada zaidi ya mikopo ambayo inarudi kwao.... Mfano...Bomba la gesi Mtwara hadi Dar, mkopo exim bank ya China...contract wamepewa wchina na pesa imerudi kwao

Nonsense
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom