Somo la kijinga kutoka kwa mjinga kwenda kwa wajinga!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,239
Mwaka huu wa uchaguzi ni wa kijinga sana.

Ni mwaka wa wajinga kuambiana ujinga na kukubaliana katika ujinga.

Mbaya zaidi wajinga hawakai kimya kwa kuwa werevu hawataki kuwaambia wajinga kama wanafanya ujinga kwa kufanya ujinga.

kuna mjinga mmoja alifanya ujinga akidhani werevu na wajinga wote ni wajinga.

kuna werevu wakajitahidi kuwaeleza wajinga ingawa walieleza kijinga kuwa kuna mjinga alifanya ujinga kijinga sana.

Basi werevu na wajinga wakaamka kwa hamaki na kujidai kukataa ujinga na kulazimisha mjinga ajione mjinga na kusema huu ulikuwa ujinga wa wajinga wenzangu lakini sitaki kuuelezea sana kwani wajinga hamtakiwi kuujua ujinga huu na mjinga mwengine huku akifikiria mjinga mwenzake akiondoka ataendelea kuwafanya wajinga waendelee kuwa wajinga.

Kumbe yule aliyeonekana mjinga alijanjaruka na kuamua kuwa mwerevu hata kama ni kijinga.

Huyu mjinga mwingine alihisi mjinga mwenzake bado ataendeleza ujinga waliokubaliana kumbe mwenzake alishatoka kwenye ujinga na kuamua kuwa mjanja.

Wajinga na werevu walikuwa wakiangalia tu michezo ya kijinga inayoendelea huku wakipiga kelele za kiwerevu.

kumbe kwenye group la waliodhaniwa kuwa werevu kuna wajinga wengi waliokuwa wakicheza na akili za wajinga na werevu.

Ujinga ukaendelea mpaka 2015 mpaka pale mjinga na mjanja walipofanyiana ujinga.

Ebo...! Katika kundi la wale waliodhaniwa kuwa werevu pakaibuka mjinga mmoja au wawili hivi wakaamua kukubaliana na mjinga ili aje kuendeleza ujinga kwenye Taifa la werevu,wajanja na wajinga.

He...mjinga huyu akaamua kumpaisha mjinga mzoefu ili awasimamie werevu,wajanja na wajinga katika kutupeleka kwenye nchi ya kijinga.

mbaya zaidi kuna wajinga wanataka kukubaliana na ujinga kisa mjinga kazidiwa kete na mjanja.Hapa mwerevu ameshtuka sana na kamwe hataki kuona wajinga wakiendelea kufanya ujinga na wajanja wakiendeleza ujanja!

Kazi ya mwerevu itakuwa moja tu mwaka huu...kukataa ujinga ushike nafasi.

werevu wawe tayari kuukubali ujanja kwa mara nyingine kuliko ujinga!!

Hili somo ni gumu sana kwa mjinga,mwerevu na mjanja.

Tunasubiri mtihani wa mwisho ambapo mwerevu atakuwa namba moja akifuatiwa na mjanja(huyu ataigiliza kwa mweravu) na mjinga atashika mkia tu na ujinga wake.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Ni kweli kabisa lakini rudi kwenye hoja ndugu yangu.kama ni mjinga jadili kijinga.
kama ni mwerevu jadili kwa werevu na kama ni mjanja jadili kijanja

Watu sasa hivi tunajipanga jinsi ya kumsindikiza rais wa watanzania mh lowasa mara baada ya kuapishwa hapo novemba
 
Kaka nitaisoma hii post yako kwa mara nyingine tena baada ya uchaguzi kwa ajili ya reference. Inawezekana ikawa na maana. Soma hii yangu;

" Mjinga amejiunga na wajinga na wajinga wanamfuata mjinga bila ya wao kujua wanafanya mambo ya kijinga"
 
Watu sasa hivi tunajipanga jinsi ya kumsindikiza rais wa watanzania mh lowasa mara baada ya kuapishwa hapo novemba
Wajinga wanajipanga kijinga kumsindikiza mjinga kula kiapo cha ujinga baada ya ujinga kufanyika?
 
Kaka nitaisoma hii post yako kwa mara nyingine tena baada ya uchaguzi kwa ajili ya reference. Inawezekana ikawa na maana. Soma hii yangu;

" Mjinga amejiunga na wajinga na wajinga wanamfuata mjinga bila ya wao kujua wanafanya mambo ya kijinga"
Mkuu hii post yako iko wapi hebu nipe link!
 
Ni kweli kabisa lakini rudi kwenye hoja ndugu yangu.kama ni mjinga jadili kijinga.
kama ni mwerevu jadili kwa werevu na kama ni mjanja jadili kijanja

safi sana

mimi ni jinga sana lakini nikielevuka oktoba 25 mjanja aanze kuhama nchi
 
Aisee jingalao mbona kila uzi unaweka humu huwa unakuwa na upinzan mkali ushawahi fikiria juu ya hili.... Hebu fukiria zaid alafu utagundua shida iko wap hoja yako inaweza kuwa nzur ila unakosea namna ya kuiweka!!!
 
Jingalao kweli kuna mambo mengi ya kijinga ambayo yanaendelea hapa nchini.Ila kuelewa kuwa ni ujinga tusubiri baada ya October tuombeane uzima.
 
jingalao

bado wewe ni pumbavu 1000000 na kabla hujaandika nilishajua mawazo yako ya nini kutujazia uchafu gumu.
 
Last edited by a moderator:
Werevu walidhani werevu kumbe werevu wao ulikuwa mkubwa kwenye ujinga na aliyedhaniwa mjinga alijifanya mjinga ili wale waliojiona werevu wasimtambue kuwa ni mwerevu.
 
Werevu walidhani werevu kumbe werevu wao ulikuwa mkubwa kwenye ujinga na aliyedhaniwa mjinga alijifanya mjinga ili wale waliojiona werevu wasimtambue kuwa ni mwerevu.

Nimependa unavyojibu hoja hii.
what if kama werevu nao wamejifanya wajinga ili mjinga ajione mwerevu?
 
Back
Top Bottom