jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,052
- 28,242
Mwaka huu wa uchaguzi ni wa kijinga sana.
Ni mwaka wa wajinga kuambiana ujinga na kukubaliana katika ujinga.
Mbaya zaidi wajinga hawakai kimya kwa kuwa werevu hawataki kuwaambia wajinga kama wanafanya ujinga kwa kufanya ujinga.
kuna mjinga mmoja alifanya ujinga akidhani werevu na wajinga wote ni wajinga.
kuna werevu wakajitahidi kuwaeleza wajinga ingawa walieleza kijinga kuwa kuna mjinga alifanya ujinga kijinga sana.
Basi werevu na wajinga wakaamka kwa hamaki na kujidai kukataa ujinga na kulazimisha mjinga ajione mjinga na kusema huu ulikuwa ujinga wa wajinga wenzangu lakini sitaki kuuelezea sana kwani wajinga hamtakiwi kuujua ujinga huu na mjinga mwengine huku akifikiria mjinga mwenzake akiondoka ataendelea kuwafanya wajinga waendelee kuwa wajinga.
Kumbe yule aliyeonekana mjinga alijanjaruka na kuamua kuwa mwerevu hata kama ni kijinga.
Huyu mjinga mwingine alihisi mjinga mwenzake bado ataendeleza ujinga waliokubaliana kumbe mwenzake alishatoka kwenye ujinga na kuamua kuwa mjanja.
Wajinga na werevu walikuwa wakiangalia tu michezo ya kijinga inayoendelea huku wakipiga kelele za kiwerevu.
kumbe kwenye group la waliodhaniwa kuwa werevu kuna wajinga wengi waliokuwa wakicheza na akili za wajinga na werevu.
Ujinga ukaendelea mpaka 2015 mpaka pale mjinga na mjanja walipofanyiana ujinga.
Ebo...! Katika kundi la wale waliodhaniwa kuwa werevu pakaibuka mjinga mmoja au wawili hivi wakaamua kukubaliana na mjinga ili aje kuendeleza ujinga kwenye Taifa la werevu,wajanja na wajinga.
He...mjinga huyu akaamua kumpaisha mjinga mzoefu ili awasimamie werevu,wajanja na wajinga katika kutupeleka kwenye nchi ya kijinga.
mbaya zaidi kuna wajinga wanataka kukubaliana na ujinga kisa mjinga kazidiwa kete na mjanja.Hapa mwerevu ameshtuka sana na kamwe hataki kuona wajinga wakiendelea kufanya ujinga na wajanja wakiendeleza ujanja!
Kazi ya mwerevu itakuwa moja tu mwaka huu...kukataa ujinga ushike nafasi.
werevu wawe tayari kuukubali ujanja kwa mara nyingine kuliko ujinga!!
Hili somo ni gumu sana kwa mjinga,mwerevu na mjanja.
Tunasubiri mtihani wa mwisho ambapo mwerevu atakuwa namba moja akifuatiwa na mjanja(huyu ataigiliza kwa mweravu) na mjinga atashika mkia tu na ujinga wake.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!