Somo la Historia ya Tanzania: Baada ya Rais kutishia kumfukuza Waziri, Ndalichako atoa ufafanuzi hatua zilizofikiwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Salaam Wakuu,

Baada ya Rais Magufuli kutilia Mkazo Somo la Hisitoria, na kutishia kumfukuza kazi Waziri, Leo hii Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameita waandishi wa habari na kuelezea hatua zilizofikia katika kuandaa somo la Historia.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na Wanahabari amesema kwamba Wizara ilichukulia kwa uzito mkubwa maelekezo ya rais, Amesmea Baada ya rais kutoa hayo Maelekezo, Wizara ilipitia Mitaala ya Tanzania na kuona kitu kilichokuwa kinafundishwa kuhusu Historia ya Tanzania ni kidogo Mno. Historia yetu ulikuwa haijajikita katika mlengo ambao Rais alielekeza.

Wizara ilianza kutekeleza maelekezo ya rais Mara moja na Wizara imeaandaa Mihitasari ambayo itawezesha somo hilo kufundishwa kuanzia Elimu ya Awali mpaka Kidato cha Sita kwa lugha ya Kiswahili.

Mihitasari hiyo imelenga katika kuhakikisha kwamba inaamusha na kujenga moyo wa Uzalendo kwa kuwafanya watanzania kuifahamu nchi yao, kuithamini kuipenda na kujenga moyo wa Kulinda raslimali katika nchi yao.

Mihitasari ambayo imeshakamilika ni wa darasa la kwana mpaka la saba, Kidato cha kwanza mpaka cha nne na Kidato cha tano mpaka cha sita.

Tumeshirikiana na Wanahistoria, na watu waliobeba katika Historia na tumeshirikiana na Taasisi za Elimu ya Juu.

Somo la Historia la Tanzania litakuwa la lazima kwa Wanafunzi wote vile vile somo la Histori lililokuwepo litaendelea kama kawaida.

Ndalichako Amesema amemsikia rais akiwa Morogoro, amesema atawaiwa radhi kwa ukimya kwani walikuwa wanaendelea na kazi. Sasa kazi inayoendelea ni ya Uandishi wa Vitabu kuanzia darasa la kwanza hadi Kitado cha Sita.

Leo rais Magufuli akiwa Morogoro amesikika akisema: “Nasisitiza sana somo la Historia ya Tanzania lifundishwe Mashuleni, namshangaa Waziri mpaka leo hajatoa statement au labda aje atoe statement akiwa sio tena Waziri ndio ataelewa, historia ya Tanzania ni muhimu sana, waliobaki na historia ni Wamasai”

Prof. Ndalichako. Wizara ya elimu imekushinda, hakuna jipya wala hakuna mabadiliko. Pisha hiyo nafasi unatumbuliwa soon. Bodi ya mikopo imekushinda, mitaala ya elimu imekushinda, mafunzo ya VETA yamekushinda, elimu inayotolewa vyuo vikuu hsiwasaidii Watanzania, hili hujaliona bali spika alikukumbusha juzi. Wizara ya elimu imekushinda.
 
Prof. Ndalichako. Wizara ya elimu imekushinda, hakuna jipya wala hakuna mabadiliko . Pisha hiyo nafasi unatumbuliwa soon. Bodi ya mikopo imekushinda,mitaala ya elimu imekushinda, mafunzo ya veta yamekushinda, elimu inayotolewa vyuo vikuu hsiwasaidii watanzania,hili hujaliona bali spika alikukumbusha juzi. Wizara ya elimu imekushinda.
Bado Mathematics inaongoza watu kufeli
 
Prof. Ndalichako. Wizara ya elimu imekushinda, hakuna jipya wala hakuna mabadiliko . Pisha hiyo nafasi unatumbuliwa soon. Bodi ya mikopo imekushinda,mitaala ya elimu imekushinda, mafunzo ya veta yamekushinda, elimu inayotolewa vyuo vikuu hsiwasaidii watanzania,hili hujaliona bali spika alikukumbusha juzi. Wizara ya elimu imekushinda.
Wizara zilizoko na zinakoelekea kubaya 1. Wizara ya elimu 2. Wizara ya afya 3. Wizara ya viwanda 4. Wizara ya mali asili na utalii 5. Wizara ya kilimo 6.wizara ya uwekezaji.
 
Prof. Ndalichako. Wizara ya elimu imekushinda, hakuna jipya wala hakuna mabadiliko. Pisha hiyo nafasi unatumbuliwa soon. Bodi ya mikopo imekushinda, mitaala ya elimu imekushinda, mafunzo ya VETA yamekushinda, elimu inayotolewa vyuo vikuu hsiwasaidii Watanzania, hili hujaliona bali spika alikukumbusha juzi. Wizara ya elimu imekushinda.
Tatizo liko kwa huyo huyo Magufuli. Matatizo yanayoikumba elimu yetu solution siyo kutoa matamko na amri majukwaani.
 
Back
Top Bottom