Somo la demokrasia gumu

Novatus

JF-Expert Member
Jul 28, 2007
330
37
wana JF ukiuliza nini maana ya demokrasia walio wengi watajibu kuwa ni uamuzi wa walio wengi kwa kuwazidi wale wenzao ambao ni wachache. kimanti sio sahihi maamuzi kama hayo kuwa ni sawa kwani mara nyingi ushabiki unatumika. ifuatayo ni mifano michache naomba muongeze mingine kwa manufaa ya kuelelimisha walio wengi

1. Mwalimu Nyerere alitoa mfano wa mradi wa ng'ombe wa maziwa kwa wanakijiji fulani kuwa lengo la kufuga lilikuwa ni kupata maziwa kwa ajili ya wanakijiji lakini ilipofika siku ya Christmas wanakijiji wakakaa na kutoa hoja kuwa hawajala nyama siku nyingi hivyo wachinje wale ng'ombe wapate kitoweo cha sikukuu. kura zilipigwa wanaotaka nyama wakashinda mradi ukafa.

2. Wayahudi walipiga kura Yesu auwawe wamwachie jambazi Baraba wakati Yesu hakuwa na hatia.

3. maamuzi ya Bunge letu mara nyingi ni potofu lakini kwa kuwa CCM ni wengi yanapita sababu tu ya ushabiki wa chama wala sio kwa maslahi ya taifa.

hiyo ni mifano michache naomba muiongeze mingine wanachi wapate elimu
 
Demokrasia ni Utawala wa watu kwa manufaa ya watu wenyewe, hivyo basi maamuzi ya wengi yasiyokuwa na manufaa kwa watu hao siyo demokrasia.
Demokrasia lazima iendane na mazingira na uelewa wa watu wenyewe.
Demokrasia ya nchi zilizoendelea hawezi kulinganishwa na demokrasia katika nchi zinazoendelea, tofauti ni kubwa mno kifkra,kielimu, kiuchumi nk.
Demokrasia ni zaidi ya uamuzi wa wengi wape!
 
Back
Top Bottom