Somo kwa watumiaji Facebook wote

NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,461
2,267
Ujinga mtaji, na na wajinga hua wanaliwa siku zote.. Kwa watumiaji Facebook napenda kutoa somo baadhi ya vitu wasivovifahamu kuhusu Facebok ambavyo inatakiwa kuvijua...

1. Kila picha unayopost Facebook si mali yako tena ni mali ya Facebook na wanaweza kuifaya wanavotaka,
Asilimia 99.99% ya watu hua hawasomi "terms and conditions" ila kwa mtu aliyesoma terms na conditions hizi atajua wameandika vizuri kabisa kua kila picha utakayopost pale ni mali yao..
Sasa effects zake ni zipi??
- Kwa wale wadada wanaopenda kuweka vipicha skirt fupi siku hizi kuna ka-mtindo kamezuka kwenye website za ngono kutumia picha za wadada kutoka facebook kama matangazo kwenye sites zao, na mdada hana uwezo wa kuwafunga sababu ile picha sio mali yake tena, ni hadi aombe facebook wenyewe wampe onyo mwenye site afute which is a process si rahisi Facebook wana watu bilioni hadi usumbuke kidogo hadi hilo liwe solved...

2. Zile posts unaona ati click "like" kumsaidia mtu flani hua ni fix tu, like hako yaina msaada wowote kwa yule ambaye picha yake wameiweka pale, ile hua ni njia tu ya kukusanya likes nyingi kutangaza page, biashara nzuri sana ipo watu wanafanya wanakusanya likes nyingi afu wanauza page kwa watu wanaohitaji kutangaza vitu vyao online.

3. Kila picha unayopost na message ambazo ziko kwenye account yako ukifuta unakua umevifuta kwako tu, ila kwenye server za facebook zile data zote wanabaki nazo, hakifutwi kitu hata kimoja, kwa hiyo usikae ukajidanganya hiyo "delete" button unayobonyeza ukahisi umemaliza kila kitu. Kua makini kwa kila unachofanya kwenye mtandao, kitu unaweza ukakoksea leo kiikaja kukucost miaka ya mbele sana....
 
Nadhani kuna vitu haviko sawa hapa mkuu !
Zaidi zaidi utawaogopesha tu kina dada wa watu !
 
hebu endelea kudadavua mkuu,wenye macho wasom,wenye maskio waelewe,ijapokuwa nilifunga akaunt yangu miaka mbili ilyopita
 
Nadhani kuna vitu haviko sawa hapa mkuu !
Zaidi zaidi utawaogopesha tu kina dada wa watu !
Kuhusu namba moja kasome terms and conditions za facebook uprove mwenyewe, kuhusu namba mbili hata haihitaji akili timamu kujua kua like yako haimsaidii either mgonjwa au mtu mwenye shida, we ushawahi pewa like ukapata hela?, khs namba tatu kua data hua hawazifuti, mtu yoyote aliyesoma comouter science atajua umuhimu wa data, mtu anaweza akaweka delete sema makampuni haya hua yanajua some day hizo data zaweza kuhitajika kufanya kitu flani, na kwa kua wao ni wa miliki maana we ulikubali conditions zao basi hawazifuti, kila siku wanaongeza server mpya tu, ukifuta inafutika kwako sio kwao...
 
Na vile T&c zao zilivyo nyingi lazima upate uvivu kusoma na tunakimbilia pale kwenye
'agree/accept'
 
Back
Top Bottom