Somo kuhusu viatu vya ngozi, ni watanzania wachache sana wanaovaa viatu vya ngozi vipya

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
6,653
20,966
Tanzania ni moja ya wazalishaji wakubwa wa ngozi duniani ila ni watanzania wachache sana wanavaa viatu VIPYA vya ngozi Original,
Uandaajia wa ngozi(hide) mpk ije kua leather nzuri inapitia hatua nyingi, zinazohitaji utaalam na gharama,
View attachment 984771 hapa si tii neno ila hii ni moja ya pure leather,


duniani ni waitaliano tuu ndio wanaaminika kwa processing nzuri ya ngozi(hide) to leather zilizoiva vzr,
View attachment 984773 hao wengne wanaiga
NOTE: nimesema processing sio uzalishaji na hapo ndio shughuli ilipo,

Hatua kuu za uandaaji wa ngozi(hide) to leather

1. Soaking, fleshing
Hapa ngozi inadumbukizwa kwenye maji kwa ajili ya kuondoa uchafu, damu na mafuta.

2. Un-hairing, pickling na de-peckling,
Hapa ngozi inatolewa nywele halaf inadumbukizwa tena kwenye acid(cacl2)/salt(Nacl) na sulphuric acid(H2SO4) ili ku lower au ku neutralize PH(chemistry) lengo ni kuzuia wadudu wanaosababisha uozaji endapo acid au base itazidi.

3. Liming, de-liming na Bating,
Hii liming inasaidia ile acid au base iliyowekwa kunywea vizuri maana hii liming(Ca & Mg) inafanya ile ngozi kua loose ili maji maji kupenyeza(infiltration) na kukausha mafuta, halaf ngozi inaoshwa tenaa kwa maji na NH4cl, pia huondoa kamba kamba zisizohitajika na kuifanya ngozi iwe laini


4. Tanning,
Hii ndio hatua ya mwisho na muhim sana, hapa ngozi inafanyiwa processing kuhakikisha hakuna kitu chochote kinachoweza sababisha uozaji kinabaki hivyo kunatakiwa kubaki kamba kamba za protein tuu, na hapa ndio wataliano wanachukulia point.


MADA KUU,

Kwa tujue ya kua Ubora wa leather unategemea vitu vifuatavyo,
1. Aina ya mnyama
2. Mnyama alipoishi na hali ya hewa(jua sana sio zuri)
3. Sehemu ilipotoka ngozi katika mwili wa mnyama
View attachment 984863
4. Layer ipi ya ngozi iliyotumika, juu, kati au chini, (juu ndio bora)
5. Ubora na maarifa katika processing( hapa italy ndio wenyewe)

Pia Utunzani wa kiatu cha ngozi unategemea vitu vifuatavyo
-Kisiingie maji na yakakaa kwa mda mrefu
-kisiwe kikavu sana na ndio maana tunapiga kiwi(kiwi nzuri zinakua na unyevu unyevu unaopenyeza ndani) ili kiatu kisikakamae
-kisiingie mafuta
AINA YA LEATHER ORIGINAL,
Unapoenda dukani kununua kiatu cha ngozi n vizuri ukajua je ni aina gani ya lether imetumika kutengenezea kiatu hicho, wengi wetu ukisikia tu ni kiatu cha ngozi basi unadhani vyote vinafanana ubora, kumbe kuna aina zaid ya nne


4. BONDED LEATHER,,
Hii ni leather ya mwisho kbsa kwa ubora katika hizi top 4, hii hutengenezwa kwa kukusanya mabaki ya vipande, kamba kamba au unga unga wa ngozi na kuanza kuvifanyia processing za kuunga, aina hii ya leather kwa jina lingine wanaita GENUINE leather(wazungu ni wajanja sana, hapa wametumia bussines trick)
Kwaio ukienda dukani muuzaji akakuambia hii ni genuine leather kama ANAMAANISHA jua umeliwa hio ni grade ya nne kwa ubora lakini still ni imara na kwa makadirio ukifuata matumizi mazuri ina uwezo wa kudumu kuanzia miaka 5-8, hii ukiikuta dukani mpyaa na well processed ni kuanzia 250,000/tsh kwenda juu
View attachment 984839


3.CORRECTED LEATHER,
Hii inatengezezwa kwa kuondoa ile layer ya juu yote iitwayo collagen(hapa kuna upper and lower collagen) ambayo hua na mikunjo kunjo, LABDA mikwaruzo(kama mnyama aliipata), vimelea au rangi tofauti tofaut(ngozi haiwezi kua na rangi moja mwili wote, lets say km mnyama alipata jeraha au mgongoni kunakopigwa na jua sana kunakua na rangi tofauti na tumboni) inabaki layer iitwayo CORIUM, lengo la kuondoa layer hii n kua na uniform leather mwanzo misho, sio kiatu hapa ni cha brown pale n cheusi, au sehm hii ina tundu pale hamna, mara nyingi hua very smooth kwa sbb ile grain yenye rafu surface imeondolewa, hiki kiatu ukifuata ule utunzaji mzuri kwa matumizi ya kawaida kina uwezo wa kudumu kuanzia miaka 8-12, haina tena ila natural texture/feel unapoishika, hua ngumu sanaa, kwaio ukiona kiatu ngozi yake ni ngumu sanaa jua n corrected na ni grade C/3, pia ukikivaa kwenye joto hutokwa na jasho sana maana yale matundu/vimelea vya nywele vilivyokua kwenye ile ngozi vimeharibiwa hivyo upumuaji ni mdg, na dukani huu mzigo ukiupata wa kitaliano uliokua well processed ni kuanzia 250,000-350,000/tsh,
View attachment 984892

2. TOP GRAIN LEATHER,
Hii hutengenezwa kwa kuondoa ile layer ya juu ya collagen(upper collagen tuu), hii hua nyembamba na mara nying huwekwa layer juu kufanya kiatu kiwe smooth, water resistance na kuondoa pia imperfections, ngozi yake inakua imara na nyepesi kukunjika, dukani kipya kinaanzia 350,000-450,000/tsh na ukifuata mashart mazuri ya utumiaji na km processing n nzuri kitadumu kuanzia miaka 12-20.
71Cz+GSwycL._UX500_.jpeg
Screenshot_20190103-182654.jpeg




1. FULL GRAIN LEATHER,
Hii ndio first class of leather, hakuna kinachoondolewa kingne zaidi ya nywele,
Kinakua kizitoo,
Kadiri unavyokitumia kikawa kinapigwa na jua na unyeve kiasi ndio kinazidi kua imara,
Kadiri unavyokitumia kikipigwa na mwanga kinaform kitu kinaitwa patina, yaani kinatengeneza rangi ya brown, grey , green n.k kulingna na mazingira mnyama alipokua akiishi pamoja na reactions,
Kina matundu madg sana ya hewa sbb vile vimelea havijaharibiwa hvyo kutotoa jasho ukivaa,
Kina harufu nzuri ya asili ya kuvutia na sio ya plastic au chemical, finishing yake inaweza kua Aniline= kinadumbukizwa kwenye maji ya rangi kukia rangi uionayo, hii ndio njia bora kwa uimara
Chunky-Combat-Full-Grain-Leather-Boots-2018-High-Quality-Men-Mid-Calf-Lace-Up-Military-Footwe...jpeg
au Sem-Aniline kinawekwa layer ya rangi ambayo unaweza kua na mchanganyiko wa plastic au chemical na hv ndio ving vinakuaga vya kiwi
rBVaWVwUVfOAb-ZzAAB-MrCCRBQ631-1.jpeg

Huu mzigo ukiwa well processed na all material yaliyotumika kukiunda yakawa natural( kumbuka hata soli ya kiatu inatakiwa itengenezwe kwa leather) dukani kipya ni kuanzia 450,000-700,000/tsh na kinadumu kwa takriban miongo mitatu km processing ilikua nzuri na utunzaji ukawa mzuri pia
Hivyo ndio viatu original vya ngozi ambapo kwenye maduka yetu ya kibongo si rahisi labda kdg pale service limited au

Wengi wanavaa plastick
s-l300-1.jpeg


Wengine mtumba


Wachache sythentic/faux/man made/artificial leather


Jinsi ya kutambua leather fake
1. Haipitishi maji hata kdg wala kuloana
2. Ukiikunja ukaachia inaacha mikunjo
3. Ina harufu ya plastic au chemicals
4. Ukubwa na uzito wake haviendani(chepesi)
5.


NITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app

71Cz+GSwycL._UX500_.jpeg


Screenshot_20190103-182654.jpeg


Piel-Top-Grain-Leather-Shoe-Travel-Bag-109fdc34-d373-4f80-8648-c6a2bca3aad8.jpeg


Piel-Top-Grain-Leather-Shoe-Travel-Bag-109fdc34-d373-4f80-8648-c6a2bca3aad8.jpeg


Chunky-Combat-Full-Grain-Leather-Boots-2018-High-Quality-Men-Mid-Calf-Lace-Up-Military-Footwe...jpeg


downloadfile-10.jpeg


rBVaWVwUVfOAb-ZzAAB-MrCCRBQ631-1.jpeg


Brand-Men-Dress-Shoes-High-Quality-Full-Grain-Leather-Shoes-Mens-Fashion-Point-Toe-Ankle-Boot...jpeg


6e19860354de1ba82f8c3d263d689296a9a07dcd.jpeg


6e19860354de1ba82f8c3d263d689296a9a07dcd.jpeg


downloadfile-10.jpeg


downloadfile-10.jpeg


Brand-Men-Dress-Shoes-High-Quality-Full-Grain-Leather-Shoes-Mens-Fashion-Point-Toe-Ankle-Boot...jpeg


downloadfile-18.jpeg


68856439-shop-of-second-hand-leather-shoes-many-used-shoes-for-sale-.jpeg
 
Wengine tumezoea vile viatu pure leather vya SIDO/wajasiriamali. Bei 30,000/= mguu unang'aa kuliko hata wa injinia msoma namba.
Vinapatikana wapi hivi mkuu? Kuna pair niliinunua nanenane arusha ilikuwa hain'gai ila ni imara haswa! Nimevaa hadi nikaichoka na kuigawa kwa mtu mwingine huku bado ikionekana mpya!
 
Na kama vipo dukani basi hatuwezi kumudu bei zake! Mitumba for life!!

Ndio maana nikafupisha maelezo kwa kusema wengi wetu tutavifaidi viatu halisi vya Ngozi mtumbani tu, dukani unaweza kupigwa bei mbaya na bado sio Ngozi halisi.

Ngozi yenyewe yenyewe inaonekana bei yake sio Rafiki kwa walio wengi.
 
Vinapatikana wapi hivi mkuu? Kuna pair niliinunua nanenane arusha ilikuwa hain'gai ila ni imara haswa! Nimevaa hadi nikaichoka na kuigawa kwa mtu mwingine huku bado ikionekana mpya!
Mafundi wapo wengi tu mtaani japo wanatofautiana kwa ubora. Mimi nilivipata Sabasaba kwa 40,000/= kwa kila pair na wasiofahamu wanadhani ni vile vya 120,000/= hadi 150,000/= maana pamoja na kwamba ni locally made lakini viko bomba sana.
 
Kuna wale wanaonunua makoti ya mtumba ya leather wanatengenezea viatu..
Kwani hapa tanzania ngozi inapatikana kwa gharama sana?
 
Leather inshu haipo kwenye ngozi , inshu kubwa n procesing yake ndio shughuli na ndio tunapofeli, chukulia mf wa sendo za kimasai, unakuta sendo imekakamaa kama ukuko wa pilau ya dua, halaf bd inatoa harufu ya uvundo, sisi uwezo wetu unaushia pale, wataalam wa processing ya ngozi duniani ni italy tuu, ile sendo umpe muitaliano akutengeneze utabaki kinywa wazi halaf anakuambia vaa utakavyo na aprox kima cha chini anakupa 15 yrs
Kuna wale wanaonunua makoti ya mtumba ya leather wanatengenezea viatu..
Kwani hapa tanzania ngozi inapatikana kwa gharama sana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom