Somo: Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho ni mwisho upi tunaoutazamia?

mhugo hantish

Senior Member
Apr 21, 2015
137
36
Kila nikitazama ulimwengu ninaona tuna deni kubwa sana kwa Mungu wetu. Tuliopewa uwakili wa kuisimamia ardhi, wanyama, mimea, ndege, bahari pamoja na kila kitambaacho ardhini tumekwenda tofauti kabisa na mapenzi yake yeye aliye tuumba. Kiburi, majivuno na majigambo vimetawala kwa WANADAMU wa leo, mtu kupewa kacheo kama uwenyekiti wa familia zenye watu sita tu unaanza kujitutumua.

Ungepewa kijiji kizima si ungeuza hadi watoto wa shule kwa kupenda mali? Dhambi ya uzinzi, na uasherati ndio sasa imefikia robo fainali, yaani bado kidogo tu kama sio tayari kuonana baba na mwanae. Ee Mungu Turehemu ukabaji na utekwaji pamoja na ujambazi umeanza kushika patamu.

Najiuliza swali, je, ni kwamba sisi waimbaji hatuombi, tunategea kuomba, au tunaomba pasipo Roho na kweli? Au na waimbaji nao wanatafuta kiki badala ya kuomba kwa Roho na kweli? Any way. Let me leave them. How about wahubiri na MANABII (prophets)? Siku hizi wahubiri tumekua tukizungumza siasa, tukizungumza pesa na utajiri kwa wingi, sio mbaya kuzungumzia fedha na utajiri ila shida ni kwamba tumejikita kutafuta sana pesa zilizo mikononi mwa waumini wetu na sio kuokoa Roho za waumini wetu wanaotaka kupoteza maisha ya ukristo kamili.

Nasema hivi... Ipo siku Mungu ataidai talanta yake aliyokukabidhi na atahitaji umpe mahesabu ya talanta jinsi ulivyoitumia (wafanya biashara wanaita MAUZO). Ulimwengu huu wote kwa ujumla hauwezi kwenda salama kama Usipo Pata waombaji, waimbaji, wahubiri, wainjilist, manabii lakini wawe na Nguvu ya Kristo Yesu aliye hai, na sio vinginevyo. Laa sivyo wachungaji na wengine waenda kwa mazoea tutaishia kulaumiana Sisi kwa Sisi.Najaribu kufikiri pia jambo hapa.

Biblia yangu IMEANDIKWA maneno haya NIWAPATE WAPI WANAWAKE WANAOJUA KUOMBOLEZA.? Leo hii WANAWAKE wanaotegemewa kufanya kazi ya maombi ndio wao wamekua wakijiuza, wasengenyaji, wengine wamekua wakimsahihisha Muumbaji wao kwa kujipodoa na kujichunua ngozi zao, wengine wameenda mbali na kuona kana kwamba hawakustahili kubeba ujauzito wameona ni bora kuzitoa na wengine wanazaa na kuwatupa nje, mambo mengine ni ya kigaidi sana ambayo nayo yanamkasirisha hadi Mungu aliye waumba. Hayo yote yana Mwisho wake.
Lakin je, ni mwisho upi unaoutazamia wewe?

By Ev Mhugo Hantish
 
Ndugu yangu mpendwa kwanza kabisa nikutakie baraka na rehema za MUNGU zizidi kuwa juu yako,maana hiki ulicho kiandika hapa ni dhahiri yakuwa ndio mambo yanayotokea hivi leo ktk kizazi/vizazi vyetu.Hakika ni hali ya kuhuzunisha sana lakini nadhani ni vyema sote tukatambua yakuwa tumekosa na kutubu mbele za Mungu wetu.Eeeeeeh MUNGU uliye mkuu utuhurumie sisi sote maana tu wakosaji mbele zako.

Barikiwa sana ndugu kwa kuliona hili na kutushirikisha.
 
  • Thanks
Reactions: cdc

Mungu akubariki wewe pamoja na jamaa zako
 
Kila nikitazama ulimwengu ninaona tuna deni kubwa sana kwa Mungu wetu. Tuliopewa uwakili wa kuisimamia ardhi, wanyama, mimea, ndege, bahari pamoja na kila kitambaacho ardhini tumekwenda tofauti kabisa na mapenzi yake yeye aliye tuumba. Kiburi, majivuno na majigambo vimetawala kwa WANADAMU wa leo, mtu kupewa kacheo kama uwenyekiti wa familia zenye watu sita tu unaanza kujitutumua.

Ungepewa kijiji kizima si ungeuza hadi watoto wa shule kwa kupenda mali? Dhambi ya uzinzi, na uasherati ndio sasa imefikia robo fainali, yaani bado kidogo tu kama sio tayari kuonana baba na mwanae. Ee Mungu Turehemu ukabaji na utekwaji pamoja na ujambazi umeanza kushika patamu.

Najiuliza swali, je, ni kwamba sisi waimbaji hatuombi, tunategea kuomba, au tunaomba pasipo Roho na kweli? Au na waimbaji nao wanatafuta kiki badala ya kuomba kwa Roho na kweli? Any way. Let me leave them. How about wahubiri na MANABII (prophets)? Siku hizi wahubiri tumekua tukizungumza siasa, tukizungumza pesa na utajiri kwa wingi, sio mbaya kuzungumzia fedha na utajiri ila shida ni kwamba tumejikita kutafuta sana pesa zilizo mikononi mwa waumini wetu na sio kuokoa Roho za waumini wetu wanaotaka kupoteza maisha ya ukristo kamili.

Nasema hivi... Ipo siku Mungu ataidai talanta yake aliyokukabidhi na atahitaji umpe mahesabu ya talanta jinsi ulivyoitumia (wafanya biashara wanaita MAUZO). Ulimwengu huu wote kwa ujumla hauwezi kwenda salama kama Usipo Pata waombaji, waimbaji, wahubiri, wainjilist, manabii lakini wawe na Nguvu ya Kristo Yesu aliye hai, na sio vinginevyo. Laa sivyo wachungaji na wengine waenda kwa mazoea tutaishia kulaumiana Sisi kwa Sisi.Najaribu kufikiri pia jambo hapa.

Biblia yangu IMEANDIKWA maneno haya NIWAPATE WAPI WANAWAKE WANAOJUA KUOMBOLEZA.? Leo hii WANAWAKE wanaotegemewa kufanya kazi ya maombi ndio wao wamekua wakijiuza, wasengenyaji, wengine wamekua wakimsahihisha Muumbaji wao kwa kujipodoa na kujichunua ngozi zao, wengine wameenda mbali na kuona kana kwamba hawakustahili kubeba ujauzito wameona ni bora kuzitoa na wengine wanazaa na kuwatupa nje, mambo mengine ni ya kigaidi sana ambayo nayo yanamkasirisha hadi Mungu aliye waumba. Hayo yote yana Mwisho wake.
Lakin je, ni mwisho upi unaoutazamia wewe?

By Ev Mhugo Hantish
Mungu atuhurumie,
 
  • Thanks
Reactions: cdc
Ndugu yangu yote haya usimfikirie mwanadamu, uyaonayo ndio mpango kamili wa Mungu!

Hakuna mwenye kujitengenezea kitu kikamshangaza Mungu, ufundi wote, wema na ubaya vyote kavifanya Mungu ili kutimia kwa malengo yake!

Haijalishi mwisho wako utakuwaje, mwisho ukifika huna uwezo wa kuuepuka, hiyo yote ipo nje ya uwezo wa viumbe!
 
Back
Top Bottom