Somo hili ni mkombozi wa umaskini kwa Mtanzania

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
7,759
10,607
Nakumbuka kipindi nasoma shule ya msingi nilikuwa nikiambiwa na wazazi wangu pia na waalimu wangu soma ili upate kazi, nikitoroka shule na kwenda kucheza mpira nilichapwa sana na kuambiwa nacheza na shule maisha yatakunyoosha, nikionekana naimba mziki naonekana mtukutu nacheza na shule maisha yataninyoosha, hakika kila Jambo nililofanya tofauti na masomo ya darasani nilionekana nacheza na elimu.

Hakika tulisisitizwa kwamba soma uje kuwa rubani, daktari, mwalimu, nesi ,mhandisi, mwanajeshi, polisi,mfamasia hakika sikuwahi sikia mwalimu au mzazi wangu akiniambia soma uje kujiajiri na kufanya biashara zako mwenyewe. Labda familia za wafanyabiashara waliambiwa haya.

Dhumuni la bandiko hili ni kuomba kuanzishwa kwa somo ambalo litafungua milango ya fahamu kwa vijana tangia wakiwa wadogo ili watambue vipaji vyao na wakati wao ujao umewandaa kuwa wakina nani?

Mada ambazo inatakiwa ziwepo katika somo ili ni kama zifuatavyo:-
1) Sheria za uanzishaji wa kampuni na usajili wa kampuni nchini..
2) Ujasiliamali.
3)Biashara.
4) kazi unazoweza kufanya na kujiajiri kutokana na taaluma uliyosomea.
5) Jinsi ya kupata mtaji wa biashara.
6) Jinsi ya kutafuta soko na wateja.
7) Michezo , muziki na burudani.

Elimu yetu inatuandaa vijana wengi kutegemea ajira ambazo zinatengenezwa na serikali, ambapo serikali ya awamu ya tano imefeli kutengeneza ajira ni wakati sasa wa kuwaandaa vijana tokea wadogo na masomo ambayo yatatanua fikra zake katika soko la ajira na kujiajiri.
Karibu kwa mawazo yenu,
 
Kizazi hiki!?
Nimemsikia mtoto wa kike wa darasa la pili kwenye daladala jana anaimba (kwa sauti ya kike) njoo nikuchumie mchicha mie, ghafla akaimba kwa sauti ya kiume (...nikukamulie mafuta) abiria wakacheeeeeka mimi sikuelewa, mtoto aliposhuka ndipo mjadala ukaanza nami ndipo nikapata picha ya mazingira anayotoka yule mtoto.

Kwanini hakuimba tambarare kwa Yesu tambarare au kaswida
 
Angeimba niacheni nionje utamu wa yesu au ilr ya shetani na mama mkwe wake wamekalia misumari

Hideen codes zilizopo kwenye hizo punchline hadi marapa bado zimewaacha hoi
 
Angeimba niacheni nionje utamu wa yesu au ilr ya shetani na mama mkwe wake wamekalia misumari

Hideen codes zilizopo kwenye hizo punchline hadi marapa bado zimewaacha hoi
🤣
 
hio namba 1 ndyo kila kitu, mashuleni tulijifunza namna ya kuandika barua ya kazi. daah🤦🏿‍♂️
Ndo ivyo shule zote mwalimu anakwambia jifunze kuandika barua ya maombi ya kazi, kwa kiswahili na kingereza bila kujua ivyo utakosa kazi ya kufanya ukimaliza shule
 
Kizazi hiki!?
Nimemsikia mtoto wa kike wa darasa la pili kwenye daladala jana anaimba (kwa sauti ya kike) njoo nikuchumie mchicha mie, ghafla akaimba kwa sauti ya kiume (...nikukamulie mafuta) abiria wakacheeeeeka mimi sikuelewa, mtoto aliposhuka ndipo mjadala ukaanza nami ndipo nikapata picha ya mazingira anayotoka yule mtoto.

Kwanini hakuimba tambarare kwa Yesu tambarare au kaswida
😄😄😄😄 Amchumie mchicha , au ndo Yale mambo ya popo kanyea mbingu.
 
Angeimba niacheni nionje utamu wa yesu au ilr ya shetani na mama mkwe wake wamekalia misumari

Hideen codes zilizopo kwenye hizo punchline hadi marapa bado zimewaacha hoi
Scars naona siku izi unaniogopa kwenye Yale mambo yetu, code za malavidavi.
 
hio namba 1 ndyo kila kitu, mashuleni tulijifunza namna ya kuandika barua ya kazi. daah🤦🏿‍♂️
Katika kusoma kwangu masuala ya uanzishaji wa kampuni nimeyakuta mtaani navyo fanya bidii ya kusambaza baasha ya kaki, Ujasiliamali nimesoma shalo in deep Tena mwaka wa mwisho chuoni. Nasoma uku nawaza kuja kuajifiwa na Tanesco, TPA,
 
Mpaka sasa hajatokea kiongozi yeyote mwenye Nia ya kumsaidia mwananchi.

Tunahitaji mfumo Bora wa elimu na viongozi wetu hawako tayari kibadilisha mfumo maana wananchi wataendelea na kiwazidi akili.
 
Mpaka sasa hajatokea kiongozi yeyote mwenye Nia ya kumsaidia mwananchi.

Tunahitaji mfumo Bora wa elimu na viongozi wetu hawako tayari kibadilisha mfumo maana wananchi wataendelea na kiwazidi akili.
Na ambaye akitokea na kutaka kumsaidia mwananchi ujue anataka atawale milele na kujificha kwenye kivuli Cha uzalendo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom