Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,796
- 12,239
Watanzania tuna jambo la kujifunza na kuchukua hatua sahihi hivi sasa kutokana na mgogoro wa mpaka wa baharini baina ya Kenya na Somalia. Tusijifanye vipofu hatuoni ukweli uliopo. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliopo hivi sasa ni wa muda tu kama katiba ya Serikali ya Muungano haitafanyiwa marekebisho makubwa au kutunga katiba mpya kabisa.
Vijana wa Tanganyika na Zanzibar wote kwa pamoja hawakubaliani na muundo wa Muungano uliopo, hivyo ni wazi nchi hizi zitakuja kutengana. Ni suala la muda tu.
Kwa kuwa ni dhahiri shahiri tutatengana lazima hivi sasa tuainishe na kuweka wazi mpaka wa baharini baina ya Tanganyika na Zanzibar, vinginevyo tutakuwa na mgogoro wa kudumu baina yetu na kusababisha vita.
Tunazo kero za Muungano na mojawapo ni ya mpaka wa baharini, hivyo ni busara ufumbuzi ukapatikana sasa tusisubiri Muungano kuvunjika!