SOME BODY HELP: Mpenzi wangu anakoroma mno nsaidien jaman!

mbona unabahati jamani?kuna mwenzako wake anajamba usiku mzima tena mume wa ndoa sio mpenzi
 
pole huo ni ugonjwa, mbaya zaid hupunguza siku za kuishi
Ntacheki dawa yake ngoja niingie library.
 
Du aisee kazi kwelikweli Jf!! mpaka raha weekiend inakaribia kuanza sasa!
 
ajaribu kulala ubavu. Tatizo likiendelea aonane na daktari
 
Ila anae lala na kujamba usiku mzima ni hatari hewa yaweza kosekana yakawa ya Tabora kwenye disco toto msimu wa idd
 
Ulitakiwa kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuuvaa mkenge....kwa vile sasa inakula kwako fuata ushauri wa kumpeleka hospitali...mie wangu akikoromo huwa najisikia burdan kama nasikiliza muziki wa 'blues'.
 
Pole sana.
mme wangu alikuwa anakoroma mtaa mzima ulikuwa unamtambua si mchana si usiku.mwenzangu adi nilinunua kifaa cha kuweka masikioni nisisikie sauti ili walau nilala na mie.Ndo nikapata ushauri nikamwelekeza adi leo ni mwaka wa pili sijamsikia kukoroma tena.

Mkilala usiku mwambie awe anatoa hulimi wake nje anarudisha tena ndani awe anautoa wotee mara kumi.
Kwa mda mwa wiki mbili anaacha kukiroma misuli ilelegea anatakiwa kuifanyia mazoezi.
 
Angalizo!

Makala hii nimeinakili kutoka katika blogu ya ISSA MICHUZI, kwa hiyo mwanzilishi wa mada sio mimi.
Endelea.......

Habari za kazi mheshimiwa Michuzi,
nilipitia hapa kwenye blog yako nikakuta bwana Chumaka wa Korogwe akiomba msaada wa namna ya kutatua tatizo lake la kukoroma ambalo linamnyima mkewe usingizi.Majibu mengine niliyoyasoma yalikua ya ajabu na pia hayakuweza kumsaidia bwana Chumaka.

Na vifaa vingi vilivozungumzwa kwa mtu aliyopo Korogwe sidhani angevipata kwa urahisi. Kwakua kulikua na comments zaidi ya 35 nikahisi nikiweka na yangu pale wengi hawataiona,naomba uiweke peke yake ili iweze kusaidia watu kama mimi ilivyonisaidia.

Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao.

Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20.

Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma.Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.

Mzee huyu aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake.

Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.
Mdau Ibrahim,D'salaam.

Chanzo: MICHUZI
 
Mwambie aende hosptal acheck septum yake inawezekana inacheza, septum ni ukuta unaotenganisha pua, wakati mwingine hauko wima kwa hiyo unasababisha kukoroma
 
Kama unampenda kweli basi hata kukoroma kwake kutakuwa kama muziki wa zumari mororo unaokubembeleza.

La, ukiona karaha, jua mapenzi yako hayajatimilika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom