Somaliland imeapa kuisaidia Kenya iwapo Vita Vitazuka baina ya Somalia na Kenya

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
23,017
2,000
Raisi wa jamhuri ya watu wa Somalilland ambae pia ni Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Nchi hiyo yenye Amani na Utulivu.
Rais Musse Biihi Abdi
Ameapa kulisaidia taifa la Kenya iwapo litavamiwa na Majeshi ya nchi ya Somalia alisema "tutawasaidia Ndugu zetu Wakenya kwa mbinu na tutalituma jeshi letu kupambana bega kwa bega na Majeshi ya Kenya".

Raisi Mussa Biihi Abdi alisema Taifa la Somalia huwa halielewi lugha nyingine mpaka nguvu itumike ndio huwa wanaelewa .

Pia amemuondoa hofu Raisi Uhuru Kenyatta kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili hautayumbishwa.
 
sundoka

JF-Expert Member
Oct 9, 2011
1,693

Sijaelewa hapa. Yaani rais wa Somalia ataisaidia Kenya kupigana na Somalia?? Ama ndo ukilaza wangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
23,017
2,000
Raisi wa Somalia anakusanya kundi kubwa la Vijana kutoka Djibouty na Ethiopia ambao ni makabila yaliyo karibu na Kabila lake lwa Usiri mkubwa.

Na ameshaongea na Raisi wa Djibouty kwa msaada wa kijeshi na inasemekana maongezi hayo yalifanywa huku milango ikiwa imefungwa.

Leo Asubuhi Jenerali wa majeshi ya Sudani aliwasili mjini Mogadishu kwa maongezi na Utawala huo wa Somalia.

Pia kuna habari zinazosambaa mitandaoni kuwa Askari wenye asili ya Kisomalia walio ndani ya Jeshi la Kenya wanapangwa ili kufanya hujuma na kutoa habari za siri za jeshi la Kenya
Kuna hatari vita hii ikachukua msimamo wa kidini pia ili Qatar na Turkey kusaidia kijeshi
Sisi kama Watanzania tusikubali kuona mwenzetu akinyolewa.
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
23,017
2,000
downloadfile-10.jpg

Mussa Biihi Abdi Raisi wa Somaliland

DCd98HOUQAAv1V4.jpg

Mohamed Farmaagio Raisi wa Somalia
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,213
2,000
Sijaelewa hapa. Yaani rais wa Somalia ataisaidia Kenya kupigana na Somalia?? Ama ndo ukilaza wangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Somalia baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe wakagawanyika yaani North na South Somalia
Somaliland ni self declared state na waliamua kujitenga na Mogadishu
Kwa hiyo kwa miaka kadhaa waliamua kujijenga kwa serikali yao na kuwa na serikali kamili ikiwa na Rais wao ambae ndiyo huyu anaetaka kuisaidia Kenya

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
23,017
2,000
Somalia baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe wakagawanyika yaani North na South Somalia
Somaliland ni self declared state na waliamua kujitenga na Mogadishu
Kwa hiyo kwa miaka kadhaa waliamua kujijenga kwa serikali yao na kuwa na serikali kamili ikiwa na Rais wao ambae ndiyo huyu anaetaka kuisaidia Kenya

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Na pia waliungana kwanza ndio kutengeneza jamhuri ya Somalia
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
10,754
2,000
Hawa hawa Somaliland ambao wapo kwenye mgogoro na Puntland kwasababu ya mpaka? Wana uadui mkali sana na Somalia pia. Hivi karibuni kutaibuka vita vya aina yake kati ya Somaliland na Puntland na nadhani wao ndio wanataka tuwasaidie kumnyoosha adui yao Somalia. Puntland ni eneo ambalo linajitawala pia, ila lipo ndani ya Somalia tofauti na Somaliland ambayo ni nchi kivyake.
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
23,017
2,000
Hawa hawa Somaliland ambao wapo kwenye mgogoro na Puntland kwasababu ya mpaka? Wana uadui mkali sana na Somalia pia
Huu mkoa wa Puntland umetengenezwa maalum Mwaka 1998 ili kutengeneza mgogoro ila Mpaka uko palepale na OAU ilikaa Mkutano na kuamua Mipaka iloyowekwa na Wakoloni iheshimiwe. Laa sivyo ingekuwa Vurugu mechi wamasai wote wangesema wanataka mpaka uhamishwe ili wao wote wawe eidha Kenya au Tanzania
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,213
2,000
Na pia waliungana ndio kutengeneza jamhuri ya Somalia
Kilichowaudhi upande wa somaliland ni Barre (late) kuishambulia wakati ule
Wewe unaonaje kuachana au kuwa nchi moja ipi bora
Maana upande mwingine hawataki kuwasikia kabisa Mogadishu
Kwa kweli inasikitisha sana maisha yao yalivyoharibika

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom