real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Rais wa Somalia ametaka kuwepo kwa njia mwafaka ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi kutoka taifa lake,huku Kenya ikisisitiza kuwa itaendelea na mpango wake ya kuifunga kambi kubwa duniani.
Kambi ya Dadaab inawahifadhi zaidi ya raia 300,000 wa Somalia.
Rais Hassan Sheik Mohamed aliambia BBC kuondolewa kwa lazima kwa wakimbizi hao hakutasaidia maslahi ya taifa lolote.
Kenya inasema kuwa inataka kufunga kambi hizo kutokana na wasiwasi wa kiusalama ,ikidai kuwa mashambulio katika ardhi yake hupangwa katika kambi hiyo.