Somalia: Watu 300 wafariki kwenye mlipuko wa bomu mjini Mogadishu, 300 wajeruhiwa

Observer

Senior Member
Oct 18, 2006
188
290
_98322007_a38ec495-26df-47ce-a9af-e2e657364aa5.jpg


_98322006_ba4ea0b6-d8d8-4493-b663-defae5914170.jpg


Sasa imebainika kuwa idadi ya watu waliouawa katika mashambulio mawili ya mabomu mjini Mogadishu, Somalia, imepanda na kuwa 276

Mamia ya watu wengine wanaripotiwa kujeruhiwa.

Hilo ndilo shambulizi baya zaid kuwahi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.

Haijulikani nani alihusika, lakini kwa idadi ya maafa, hayo yalikuwa kati ya mashambulio makubwa kabisa nchini Somalia, tangu kundi la wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabab, kuanza mapigano yao mwaka 2007.

Katika shambulio la kwanza, bomu lilokuwa kwenye lori, lililipuka kwenye njia panda, iitwayo Kilomita-5, ambapo kuna ofiisi za serikali, mahoteli na maduka, vyote viliporomoka katika mlipuko huo.

Saa mbili baadaye, bomu jengine lilikalipuka katika mtaa wa Medina.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Madina, Mohamed Yusuf Hassan, anasema, alishtushwa na ukubwa shambulio hilo.

Waziri wa habari wa nchi hiyo Abdirahman Osman amesema nchi za Ethiopia, Uturuki na Kenya zimeahidi kutoa msaada wa kimatibabu kwa waliojeruhiwa na shambulio hilo

Rais Mohamed Abdullahi Mohamed alitangaza siku 3 za maombolezo siku ya Jumapili na bendera zitashushwa nusu mlingoti na kuwaasa raia waende kujitolea damu

Shambulio hilo limetokea masaa 48 baada ya Waziri wa Ulinzi na Kiongozi Mkuu wa majeshi kujiuzulu bila maelezo yoyote

CHANZO: BBC Swahili

=========

UPDATE:

Mogadishu, Somalia. Idadi ya watu waliouawa katika mlipuko mkubwa wa bomu Jumamosi iliyopita katika eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara mjini hapa imefikia watu 300 huku wengine 300 wakiwa majeruhi.

Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab lenye mafungamano na al-Qaeda kwa kuhusika na shambulizi hilo baya zaidi kutokea nchini tangu kundi la al-Shabab lilipoanzisha harakati zake mwaka 2007.

"Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mlipuko huo. Idadi ya watu waliokufa huenda bado ikaongezeka kwa kuwa bado wengi hawajulikani waliko," Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia shiria la Reuters.

Mashirika ya habari ya kimataifa yameripoti kuwa mkasa huo ulitokea wakati lori lililokuwa limejazwa milipuko lilipolipuka karibu na lango la hoteli.

Shirika la habari la Reuters lilimnukuu Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa kwa kuwa ilichomeka vibaya hivyo ilizikwa na serikali jana na miili mingine iliziwa na jamaa zao.

Wafanyakazi wa idara ya afya wanahangaika kutambua na kutibu majeruhi wa shambulizi hilo la kikatili zaidi kwani watu 100 hawajulini walipo.

Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezekana kwani wengi inaaminika wamefukiwa kwenye vifusi vya jingo hilo lililoharibiwa.

"Tunatarajia idadi ya vifo itaongezeka," alisema Abdirahman Omar Osman akiongeza kwamba wafanyakazi wa uokozi wanahitaji msaada kwa sababu vifaa walivyonavyo haviwezi kuondoa kifusi.

"Bado tunaendelea kukusanya habari kutoka hospitali mbalimbali na ndugu wa marehemu. Wengine wamefikishwa hospitani wakiwa na majeraka makubwa. Pia tumearifiwa kuna ndugu wengine wanawaondoa hospitalini jamaa zao majeruhi,” aliongeza.

"Baadhi ya majeruhi wanahitaji uangalizi maalumu kwa vile hawawezi kutibiwa hapa. Wengi watasafirishwa leo kwenda Uturuki baada ya kuitikia ombi letu la msaada," alisema Osman.

Alisema timu ya madaktari kutoka Uturuki ikiongozwa na Waziri wa Afya, Ahmet Demircan wamewasili leo asubuhi mjini Mogadishu kwa ajili ya kusaidia kusafirisha watu zaidi ya 70 wanaohitaji matibabu ya ziada.

Chanzo: Mwananchi

 
R.I.P RAIA WA KAWAIDA TUOMBEE SANA YASIJE KWETU HAYA MAMBO MAANA PALE
MTAA WA KONGO LILE NYOMI NI BALAA.
 
Until the people learn to love themselves society won't be happy.

Inasikitisha sana
 
Dhambi ya ubaguzi ni mbaya mno,Leo utawaona hawa ni wabaya na kuwabagua na unafanikiwa kwa kuwa una nguvu lakini hutabaki salama,mtakapobaki peke yenu,mtagundua ninyi si wamoja kama mlivyodhani mwanzo,ndipo mtakapoanza kuuana tena.Ni hali hii inayowakuta wasomali.Hawakujua kama hali itafikia hapo.
 
jamanii..
hivi kwanini mataifa tusiungane kusaidia somalia na congo...juhudi bado ni ndogo ..
Shida ni uroho wa madaraka kwa viongozi hasa waafrika , so kila mtu akiji angalia anagundua kuwa naye simsafi ndipo anagundua kuwa hawezi kumgusa dictator mwenzie ,wazungu wakiingilia kati wana ambiwa wachochezi na wasiwangilie Afrika. Tupambane sisi wenyewe waafrika kukomesha ujinga huu kwanza wa uroho wa madaraka na mali na mengine yata nyooka.
 
Kumtumikia Shetani ni kazi sana! Wafuasi wa Shetani hao wakimtumikia mungu wao.
 
Jamii moja, Lugha moja, Dini moja nchi moja....
Still bado wanauana....
 
Back
Top Bottom