Somalia Taifa Lisilotakiwa Kuwa Na Amani Na Mataifa Makubwa

Mafuta sio dili tena Mkuu; wanapaswa kujua hilo. Mwaka 2030 (13 yrs ahead) Paris na miji mingine mikubwa Ufaransa wanaondoa magari yote ya mafuta barabarani na 2040 yanaondolewa Ufaransa yote. Plan ni hiyo hiyo kwa mataifa mengine ya Ulaya, Uchina na kwingineko.

Hata Uganda wanapaswa kuchangamka na mafuta yao kupitia Tanga maana miaka michache ijayo yatapigwa marufuku duniani kote kama "kitu hatari" kwa usalama wa mazingira, viumbe, na dunia kwa ujumla.
viwanda si bado vitayahitaji mkuu?
 
viwanda si bado vitayahitaji mkuu?
Swali zuri sana Mkuu. Sekta ya usafiri (magari, reli, ndege, meli, n.k.) hutumia 69.8% ya mafuta yote; (Source: Oil | Center for Climate and Energy Solutions). Viwanda hutumia 25.1% na nyinginezo ni 5.1%. Unaweza kuona mchango wa sekta ya usafiri kwa matumizi ya mafuta ni mkubwa kuliko sekta nyingine zote zikiunganishwa kwa pamoja. Hata hivyo, viwanda havitabaki nyuma; navyo vitatafuta nishati mbadala. Vyovyote iwavyo, soko la mafuta litaporomoka vibaya na hatimaye kwisha kabisa pengine ndani ya miaka 75 ijayo (utabiri wangu).
 
Baada ya kutokea mauaji makubwa huko Mogadishu kwa Bomu la kujitoa mhanga ambapo zaidi ya watu 300 wamepoteza maisha, hiyo imeonyesha kuwa nchi hiyo ipo mbali sana kuwa na amani. Kikundi cha kigaidi cha Alshaabab mpaka sasa hakijakiri kuwa kimehusika na shambulizi hili. Kitu cha kushangaza sana hiki kikundi cha Alshaabab kwa zaidi ya miaka 10 kimeendesha vita dhidi ya serikali kwa udhamini wa nani na kwa maslahi gani na kwanini kifanye mauaji makubwa kiasi hicho ambayo ni kinyume na mafundisho ya dini ya kiislam.
Ethiopia ni mojawapo ya nchi ambayo haitaki kuona Somalia likisimama kama taifa kwasababu mwaka1977 Ethiopia na Somalia walipigana vikali kugombea jimbo la Ogaden ambalo wakazi wake wengi ni watu wenye asili ya kisomali na jimbo hilo mpaka leo lipo chini ya nchi ya Ethiopia. Serikali ya Ethiopia inaamini kuwa kuwepo kwa taifa la Somalia kunauwezekano wasomali wakaanzisha vita vya kudai jimbo hilo, jeshi la Ethiopia ilishavamia nchi ya Somalia mara kadha toka mwaka 1991,
Kenya ina majeshi kusini mwa Somalia kwa muda wa miaka 6 na kuna tatizo la mpaka baina ya Somalia na Kenya, kuna dalili ya mafuta mengi kuwepo kwenye mpaka wa Somalia na Kenya upande wa Somalia, serikali ya Kenya kwa kutumia udhaifu wa kutokuwepo kwa serikali kuu ya Somalia imejaribu kubadilisha ramani ya huo mpaka ili ile sehemu kubwa yenye mafuta upande wa Somalia uhamishiwe upande wa Kenya lakini serikali ya Somalia imepeleka kesi kuhusu suala hilo mahakama ya kimataifa, moja ya sababu ya kinara wa chama cha upinzani NASA Raila Odinga kupingwa na mataifa za magharibi katika uchaguzi mkuu wa Kenya ni alipotoa kauli kuwa pindi akishinda urais wa Kenya ataondoa majeshi ya Kenya huko Somalia, mpaka sasa uvamizi huo umesababisha askari wengi wa Jeshi la Kenya kupoteza maisha huko Somalia.
Uturuki na Uganda ndio nchi pekee zinazotaka kusaidia serikali ya Somalia iwe imara, Serikali ya Uturuki imejenga kituo kikubwa cha chuo cha kijeshi Mogadishu ili Jeshi la Somalia lipate mafunzo mazuri chuo hicho kimegharimu serikali ya Uturuki dola milioni 50 na kuna wanajeshi zaid ya 300 kutoka Uturuki kama walimu, serikali ya Uturuki imetoa misaada mikubwa sana kwa nchi ya Somalia katika ujenzi wa taifa hilo kwa kujenga mashule na hospitali. Jeshi la Uganda limefanya kazi kubwa kuwadhibiti hawa Alshaabab na Jeshi hilo lipo Somalia kuleta amani.
Marekani ilivamia Somalia mwaka 1992 na baada ya vita vya wa wasomali dhidi ya wamarekani mwaka 1993 (Blackhawk Down) ambapo zaidi ya wamarekani 20 waliuawa serikali ya Marekani iliondoa Jeshi lake. Toka Rais Donald Trump aingie madarakani Marekani imerudisha majeshi yake Somalia na kwasasa wamefungua kituo kikubwa cha kijeshi pale uwanja wa ndege Mogadishu na kuna mpango wa Marekani wa Kujenga kituo kikubwa cha kijeshi nje ya Mogadishu ambayo zaidi ya Askari laki moja watawekwa standby kwa vita mashariki ya Kati.
Somalia Ina utajiri mkubwa wa aina tofauti za madini,mafuta na Gesi na hapa unaona picha kamili maslahi za nchi hizi kwa Somalia. Alshaabab ni kikundi ukiangalia wanatumiwa kwa kupitia Ideology ya Dini ya Kiislam lakini hawapo kwa maslahi ya dini ni maslahi kuona Somalia haipati amani. Ni mengi ya kujiuliza nani ama nchi gani inayofadhili kikundi hiki cha kigaidi na kwa manufaa gani.

Wasomali wana laana tu walianza kupigana kabla ya Alshabab. Tokea mwaka 1991 ile nchi haina utawala wa kueleweka. Ukiacha dini kuna vita vya ukabila ndani ya hao wasomali wenyewe.
Watu tumezoea kutafuta mchawi. Kwenye hili mchawi ni wasomali wenyewe, full stop.
 
Soma historia ya Somalia vizuri before putting poor comments
 
Hukutaja makundi zaidi ya manne ya somalia ambayo hayaelewani wala hukutaja kuwa kuna nchi ndani ya Somalia inayodai uhuru. Hawa ni kama wamesomewa albadir, tuombe kina nanihii wasitufikishe huko.

Wala hukutaja mgawanyiko wa clans/ukoo wa Somalia.
 
dd2c11655ceb377e13cbdec4ec78cb5a.jpg
 
Sasa Bongo tukiwa na Arushaland utawezaje kusema mataifa ya nje hayataki Tanzania iwe na amani.
 
Kanchi kadogo kuna wanaopigana kwa udini, kuna wanaopigana kwa ukabila na kuna kina mtemi Mirambo (war loads) hawa hawataki serikali yeyote. Ni kama ambavyo Afghanistan serikali imeishia Kabul tu.
 
Baada ya kutokea mauaji makubwa huko Mogadishu kwa Bomu la kujitoa mhanga ambapo zaidi ya watu 300 wamepoteza maisha, hiyo imeonyesha kuwa nchi hiyo ipo mbali sana kuwa na amani. Kikundi cha kigaidi cha Alshaabab mpaka sasa hakijakiri kuwa kimehusika na shambulizi hili. Kitu cha kushangaza sana hiki kikundi cha Alshaabab kwa zaidi ya miaka 10 kimeendesha vita dhidi ya serikali kwa udhamini wa nani na kwa maslahi gani na kwanini kifanye mauaji makubwa kiasi hicho ambayo ni kinyume na mafundisho ya dini ya kiislam.
Ethiopia ni mojawapo ya nchi ambayo haitaki kuona Somalia likisimama kama taifa kwasababu mwaka1977 Ethiopia na Somalia walipigana vikali kugombea jimbo la Ogaden ambalo wakazi wake wengi ni watu wenye asili ya kisomali na jimbo hilo mpaka leo lipo chini ya nchi ya Ethiopia. Serikali ya Ethiopia inaamini kuwa kuwepo kwa taifa la Somalia kunauwezekano wasomali wakaanzisha vita vya kudai jimbo hilo, jeshi la Ethiopia ilishavamia nchi ya Somalia mara kadha toka mwaka 1991,
Kenya ina majeshi kusini mwa Somalia kwa muda wa miaka 6 na kuna tatizo la mpaka baina ya Somalia na Kenya, kuna dalili ya mafuta mengi kuwepo kwenye mpaka wa Somalia na Kenya upande wa Somalia, serikali ya Kenya kwa kutumia udhaifu wa kutokuwepo kwa serikali kuu ya Somalia imejaribu kubadilisha ramani ya huo mpaka ili ile sehemu kubwa yenye mafuta upande wa Somalia uhamishiwe upande wa Kenya lakini serikali ya Somalia imepeleka kesi kuhusu suala hilo mahakama ya kimataifa, moja ya sababu ya kinara wa chama cha upinzani NASA Raila Odinga kupingwa na mataifa za magharibi katika uchaguzi mkuu wa Kenya ni alipotoa kauli kuwa pindi akishinda urais wa Kenya ataondoa majeshi ya Kenya huko Somalia, mpaka sasa uvamizi huo umesababisha askari wengi wa Jeshi la Kenya kupoteza maisha huko Somalia.
Uturuki na Uganda ndio nchi pekee zinazotaka kusaidia serikali ya Somalia iwe imara, Serikali ya Uturuki imejenga kituo kikubwa cha chuo cha kijeshi Mogadishu ili Jeshi la Somalia lipate mafunzo mazuri chuo hicho kimegharimu serikali ya Uturuki dola milioni 50 na kuna wanajeshi zaid ya 300 kutoka Uturuki kama walimu, serikali ya Uturuki imetoa misaada mikubwa sana kwa nchi ya Somalia katika ujenzi wa taifa hilo kwa kujenga mashule na hospitali. Jeshi la Uganda limefanya kazi kubwa kuwadhibiti hawa Alshaabab na Jeshi hilo lipo Somalia kuleta amani.
Marekani ilivamia Somalia mwaka 1992 na baada ya vita vya wa wasomali dhidi ya wamarekani mwaka 1993 (Blackhawk Down) ambapo zaidi ya wamarekani 20 waliuawa serikali ya Marekani iliondoa Jeshi lake. Toka Rais Donald Trump aingie madarakani Marekani imerudisha majeshi yake Somalia na kwasasa wamefungua kituo kikubwa cha kijeshi pale uwanja wa ndege Mogadishu na kuna mpango wa Marekani wa Kujenga kituo kikubwa cha kijeshi nje ya Mogadishu ambayo zaidi ya Askari laki moja watawekwa standby kwa vita mashariki ya Kati.
Somalia Ina utajiri mkubwa wa aina tofauti za madini,mafuta na Gesi na hapa unaona picha kamili maslahi za nchi hizi kwa Somalia. Alshaabab ni kikundi ukiangalia wanatumiwa kwa kupitia Ideology ya Dini ya Kiislam lakini hawapo kwa maslahi ya dini ni maslahi kuona Somalia haipati amani. Ni mengi ya kujiuliza nani ama nchi gani inayofadhili kikundi hiki cha kigaidi na kwa manufaa gani.

Kwa hiyo alshabaab wanatumiwa na taifa Gani kubwa mkuu
 
usilaumu mmataifa mengine kwa matatitizo ya somalia wao wenyewe ndio atizo
uandishi wako unajulisha IQ yako, acha nikuelimishe kidogo, je! unahakika mashambulizi yote yanayotokea Somalia yanafanywa na wasomali? majeshi ya U S yapo Somalia kwa kazi ipi?, kila majeshi ya U S yakiongezeka Somalia na mashambulizi ya kigaidi yanaongezeka, hii inaashiria nini?, all shabab ni mawakala tu wa U S, .
 
Kumbe
Kazi ipo hata Saudi Arabia haipendi wasomali wawe huru kwa kuwa eneo la Puntland ndani ya Somalia ndipo kuna mkondo wa mafuta mengi sana kwenda Saudi Arabia hivyo Somalia ikiwa huru na amani serikali itahitaji kujenga uchumi na kuchimba mafuta puntland, wakichimba puntland mafuta Saudi Arabia hayatakuwepo mafuta tena , na kwa kuwa Marekani na nchi nyingi za Ulaya zimewekeza Saudi Arabia nao hawatakubali Somalia iwe na amani, Wenyewe wanasema Somali Shall Never be Settled Again, Never on Earth for the better World. hahahahahahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom