Somalia iko Chini yaTawala za Koo,CCM ni kama Somalia?

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Somalia ni taifa ambalo huendeshwa na kutawaliwa kivipande vipande chini ya koo tangu rais mwasisi wao Siad Baleh afariki. CCM inaelekea huko huko kama chama tangu mwasisi na kiongozi mkuu Mwl. Nyerere afariki.

Uchaguzi wa ndani ya chama kuanzia kwenye taasisi na jumuiya zake hadi taifa. CCM kimeonesha dhahiri kwamba kinagawanywa vipande vipande kila ukoo ukijizatiti kuwa na sauti ya kuamua mustakabali wake. Ndani ya uchaguzi huo tumeshuhudia majina ya koo za vigogo zikishika nyadhifa kubwa kubwa. Mathalan, hadi sasa ukoo wa Kikwete unaonesha ndio umetia fora, umepenyeza viongozi wengi zaidi.

Jumuiya ya vijana ya CCM inamajina ya kina Membe, Sita, Wasira, Ndugai, Malecela, Lowassa,Mkama na wengine wengi. Kwa wale wasio na koo imara kwa ufisadi ndani ya CCM wao wamejikombakomba kwa wakuu wa koo hizo. Hawa wako wengi hata humu JF wakijikomba komba na kulamba viatu vya watoto wa wazee wa koo hizo ili yamkini baadaye waonwe.

Hofu inayojitokeza hapa ni kuona historia ikijirudia. Huko Somalia baada ya kila koo kuona usalama na maslahi yake yanatishiwa ikazuka vita kati ya ya koo na koo nyingine. Wakuu wa koo hizo wanaitwa wababe wa kivita (War-lords). Kwa mwonekano huo, yamkini CCM ikawa na vita vya koo na koo nyingine.Hapo watazuka war-lords in CCM.

Dalili ya war-lords ndani ya CCM inajionesha kupitia mnyukano unaoendelea ndani ya chama. Kundi (koo) hili likilituhumu lingine kwa rushwa,ufisadi na kuendekeza siasa za makundi. Ni mnyukano huu ambao umeiathiri nchi. Kila sekta imejaa minyukano. Nishati na Madini, Utalii na Maliasili, Elimu na Utamaduni, Uchukuzi na Mawasiliano, Usalama wa Taifa na Majeshi nk nk. Kote ni minyukano.

Kwa wapenda demokrasia, je hatuelekei Somalia nyingine ndani ya chama na kisha kutoka nje kwa wanachama na mashabiki wa hizo siasa za koo>
 
Mtoa mada uko sawa kabisa;
Hata tabia za wasomali za fujofujo ndo tabia ya wanaccm kwa sasa; ila wakumbuke kuwa siku ya siku wanayoyatenda yatawarudia wenyewe. Hata Ghadaf hakuwai kuwaza kwamba ipo siku wananchi watamgeuka na kumfanya kitu mbaya. Utekaji nyala wanaharakati na mengine mengi ndo vinachochea hasira za hawa watanzania mbumbumbu.
 
Asante bana kwa kuwapa somo ingawa nahisi bado halijasomeka kabisa katika vichwa vyao. Majuto ni mkujuuu tusubiri atufikie kwani bado hajafika na hayuko mbali saana na hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom