SOFTWARE Soma vitabu vya kiswahili kwenye hii app

Jamaa yetu ameandika hiki kitabu. Ametumia Pen name ya Pete McGregor. Kinahusu safari ya nyumbu mdogo wakati wa ukame mkali huko Serengeti na jinsi maajabu ya Serengeti yalivyoanza. Ni kitabu cha watu wa rika zote.

Ofa ni kupakua bure hadi ijumaa tarehe 12/2. Ukikisoma tunaomba maoni yako kukihusu. Ingia kwenye link hapo juu uinstall app toka playstore.
1612290659832.png
1612289074883.png
 
Kufikirika cha Shaaban Robert. Unaweza kukipakua bure mpaka jumamosi saa kumi na mbili jioni. Pakua hapo kwenye link iliyo kwenye post ya kwanza ujisomee.

1614008580310.png
 
Vazi jipya la mfalme.

Muandishi: Hans Christian Andersen, 1837
Kimetafsiriwa na Pictuss.

Email: pictuspublishers@gmail.com.

Pictuss2021.

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli(photocopy), kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mmiliki.


VAZI JIPYA LA MFALME

Hapo zamani za kale kulikuwa na mfalme aliyependa sana mavazi na kuvaa. Alitumia pesa zake zote kununulia nguo. Hakujali kuhusu wanajeshi wake wala kwenda kwenye matamasha ya maonyesho kama wafalme wengine. Alienda iwapo tu alikuwa na nguo mpya za kuonyesha kwa watu.

Alivaa nguo tofauti kila saa ya siku. Wafalme wengi walitumia muda wao mwingi kwenye mabaraza ya kuhukumu na kushauriana lakini yeye almu ya ikuwa akishinda kwenye kabati la nguo.

Siku moja matapeli wawili wakijiita washonaji waliingia kwenye nchi hiyo. Walisema wanaweza kushona nguo nzuri yenye rangi na mapambo ya kupendeza sana. Walisema nguo hiyo itatengenezwa na kitambaa ambacho hakitaonekana na yeyote yule aliye mjinga au asiyefaa kitu. Kifupi, mtu mwenye uelewa mdogo asingeweza kuiona nguo hiyo.

" Bila shaka itakuwa nguo nzuri sana" aliwaza mfalme.

" Kama nikiwa na nguo kama hiyo nitajua mara moja watu gani hawanifai kwenye uongozi wangu. Nitakuwa na uwezo wa kutofautisha wajinga na werevu, inabidi nishonewe nguo hii mara moja".

Akawaita wale washonaji na kuwapa pesa nyingi sana ili wamshonee nguo ile mara moja.
Wale matapeli wakaunganisha mashine ya kufumia vitambaa mara moja. Walifanya kazi kwa bidii sana, japo kiukweli walikuwa hawafanyi kazi yeyote. Waliomba kupewa nyuzi bora za hariri na nyuzi bora za dhahabu. Wakaziweka kwenye mikoba yao.

Wakaendelea kufanya kazi kwenye mashine ya kufumia usiku na mchana lakini hakukuwa na nyuzi zozote kwenye machine.
 
"Nahitaji kujua wale mafundi wamefikia wapi na nguo yangu" alijisemea mfalme siku moja. Akakumbuka kuwa mtu mwenye uelewa mdogo au ambaye hafai hawezi kuona kitambaa hicho, akaanza kuwa na wasiwasi. Lakini akajipa moyo kuwa haiwezekani yeye akawa mjinga na mtu asiyefaa kitu, pamoja na hilo akaona ni salama akimtuma mtu mwingine.
Watu wote kwenye ufalme ule walikuwa wamesikia kuhusu nguo yenye kitambaa cha ajabu. Wote walisubiri kwa hamu kujua iwapo majirani zao ni werevu au wajinga.

"Nitamtuma mtu wangu muaminifu na mwenye busara kwa wafumaji" mfalme alisema peke yake."

Huyu ni mtu mwerevu na hakuna anayeweza kufanya kazi kwa ufanisi kama yeye".
Kwahiyo huyu mzee wa busara akatumwa kwa wale mafundi matapeli ambao walikuwa wakifanya kazi kwa bidii kwenye mashine ya kufumia isiyo na nyuzi hata moja. Alipofika alipatwa na mshangao mkubwa. " Hii inamaanisha nini!?" Aliwaza yule mzee huku macho yakimtoka. " Siwezi kuona hata nyuzi moja!" Hata hivyo hakusema mawazo yake kwa sauti.
Wale matapeli wakamkaribisha kwa bashasha akaribie mashine ya kufumia. Baada ya kukaribia wakamuuliza iwapo amependezwa na kitambaa kinachofumwa? Wakamuuliza iwapo rangi zinapendeza huku wakimuelekeza kwa vidole sehemu tupu za mashine ya kufumia. Mzee yule alijitahidi kuangalia lakini hakuona kitu.
"Hiki nini!" Akawaza " kuna uwezekano mimi ni mjinga! Sijawahi fikiria hilo! Mtu yeyote hatakiwi kujua kuwa mimi ni mjinga na sifai kitu".

"Hapana, hapana, mfalme hapaswi kujua hili, sitamwambia yeyote kwamba siwezi kuona kitambaa kinachofumwa"
" Mzee haujatuambia iwapo umeridhika na kitambaa hiki?" aliuliza mfumaji mmoja huku akijidai kufanya kazi ya kufuma kwa bidii.
"Oh! Ni kizuri sana" alijibu yule mzee huku akiangalia mashine ya kufumia. " Rangi na urembo vinavutia, nitaenda kumjulisha mfalme mara moja jinsi kilivyo kizuri".
" Tutashukuru sana" walisema wale matapeli. Wakaanza kumuelezea kuhusu rangi na urembo huku wakimuonyeshea kwenye kitambaa ambacho hakipo. Mzee yule alisikiliza kwa makini maelezo yao ili aweze kumueleza mfalme. Wale matapeli wakaagiza waongezewe dhahabu na hariri ili waweze kukamilisha kazi yao. Walipopewa, vyote wakaweka kwenye mikoba yao kisha wakaendelea kufanya kazi kwa bidii kwenye mashine tupu ya kufumia.
 
Baada ya muda mfalme akamtuma mtu mwingine kutoka kwenye baraza lake akaangalie wale wafumaji walipofikia. Alitaka kujua kama nguo itakuwa tayari hivi karibuni. Huyu naye ilikuwa vilevile kama yule mzee mwenye busara. Hakuona chochote bali mashine tupu ya kufumia.
"Unaonaje kitambaa hiki, kizuri eeh? Mzee wa busara alikipenda sana" wale matapeli walimwambia yule mzee wa baraza.
"Nina hakika mimi siyo mjinga" aliwaza yule mzee wa baraza "inawezekanaje nikawa sifai kitu? Mtu yeyote hatakiwi kujua hili jambo". Naye akaanza kusifia kile kitambaa ambacho hakioni akisema amependezwa na rangi na urembo wake. Akarudi na kumwambia mfalme kuwa kitambaa kinachofumwa ni bora sana.
Mji wote ulikuwa unazumgumza kuhusu nguo hiyo.

Mwishowe mfalme mwenyewe akatamani kuona nguo hiyo jinsi inavyofumwa, akachukua watu wengi kutoka kwenye baraza lake na wale wazee wawili aliowatuma mwanzo.
Wafumaji wale walipomuona mfalme wakaongeza kasi ya kazi na bidii japokuwa hakukuwa na nyuzi zozote kwenye mashine ya kufumia.
"Hiki kitambaa ni bora sana" wakasema wale wazee aliowatuma mwanzo. "Hizi rangi ni bora na mapambo ni mazuri" wakaendelea kusema huku wakionyesha kwenye mashine ya kufumia, waliamini wale wengine walikuwa wakikiona kitambaa.
"Nini hiki" aliwaza mfalme "sioni chochote". " Hii haiwezi kuwa sawa, mimi si mjinga. Inamaana sifai kuwa mfalme!?". " Ooh! Kitambaa hiki ni bora sana" akasema mwishowe . "Nimekikubali" akasema huku akitabasamu na kuangalia ile mashine ya kufumia kwa karibu. Akaona haiwezekani aseme hajakiona kitambaa wakati washauri wake wawili wamekiona. Watu wengine waliokuja na mfalme wakatumbua macho kuangalia hicho kitambaa lakini hawakuona kitu lakini wote walisifia uzuri wa kitambaa kile." Hiki kitambaa kizuri sana, inabidi wakushonee vazi kwaajili ya gwaride lijalo" wakamshauri mfalme.

Mfalme akafurahi na kuwapa wale wafumaji nishani ya ushujaa. Siku moja kabla ya gwaride wale matapeli walikesha usiku kucha, waliwasha taa nyingi ili kila mmoja aone jinsi wanavyofanya kazi kwa bidii kushona nguo ya mfalme. Walijidai wakikata kitambaa na mkasi kwa kukata hewani , walijidai kukikunja, na kushona kwa kutumia sindano zisizo na nyuzi zozote. Mwishowe wakasema " tazama! Nguo ya mfalme ipo tayari".
 
Mfalme na baraza lake lote wakatoka kwenda kuona. Wale matapeli wakainua mikono kama vile wameshika kitu kisha wakasema. "Hii hapa suruali yako mfalme! Scafu hii hapa na hiki hapa kizibao! Hili vazi ni jepesi kama utando wa buibui, hata ukivaa unaweza hisi hujavaa kitu"
" Kweli kabisa" wakaitikia wale watu waliokuja na mfalme japo hakuna hata mmoja aliyeona hilo vazi.
Mfalme akavua nguo zake na wale matapeli wakajidai wakimvalisha nguo mpya. Mfalme akasimama mbele ya kioo huku akigeuka huku na huku kujitazama.
" Mfalme hizi nguo zimekupendeza na zimekukaa vema sana"kila mtu akasema kwa sauti" huu urembo , rangi na mapambo yamekaa vizuri sana, hakika hili ni vazi la kifalme"

"Niko tayari" akasema mfalme huku akiwa kama anakaguakagua vazi lake. Maofisa wa mfalme ambao walikuwa na kazi ya kushikilia joho lisiburuzike chini wakainama na kujifanya kama wamebeba kitu na kukishikilia. Hawakutaka kuonekana wajinga wala watu wasiofaa kitu.

Mfalme akaanza kutembea kwa maringo huku akiwa anafuatwa na maofisa wengi. Akaanza kupita kwenye njia za jiji. Watu wote waliosimama barabarani na wale waliokuwa wakiangalia kupitia madirishani wakasema " mfalme una nguo nzuri ajabu, scafu na joho vinavutia sana". Hakuna aliesema kuwa vazi halionekani. Kila mtu aliogopa kuonekana mjinga na asiyefaa kitu.

"Mbona mfalme hajavaa kitu!" alisikika akisema mtoto mmoja. " Msikilizeni mtoto anachosema" akakazia baba yake. Watu wakaanza kuongea chinichini kuhusu alichosema yule mtoto kisha wakapayuka! " Mbona mfalme hajavaa kitu chochote!?" Mfalme alijisikia vibaya kwasababu alijua kuwa wananchi wapo sahihi lakini akaona ni bora mambo yaendelee kama yalivyopangwa. Wale wabeba joho wakajikaza ili waendelee kuonekana kuwa bado wamelishikilia. Hakukuwa na joho lolote la kushikilia na mfalme alikuwa anatembea na nguo ya ndani tu.
 
Soma kitabu cha Mashimo ya mfalme Suleiman ndani ya hii app. Ni kitabu cha bure kabisa. Ingia kwenye link iliyo post No 1 uinstall app.

1617639640537.jpg
 
Habari wandugu. App yetu tumeibadilisha kidogo. Badala ya kununua kitabu kimojakimoja sasa utasubscribe kwa Tsh 6000 na kuweza kusoma vitabu vyote kwa mwaka mmoja. Hii itapunguza gharama ambayo bei ya kitabu ilikuwa ni 2,200. Ingia link kwenye post ya kwanza uupdate mabadiliko.

IMG_20210501_163905_363.jpg
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom