Soma Utafakari . . . . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soma Utafakari . . . . .

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CPU, Jan 18, 2011.

 1. CPU

  CPU JF Gold Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nachunguza maisha yangu nilipofikia na nilikotoka. Baba na Mama wamehangaika sana kutulea. Pengine wamefanya hivyo kwa sababu walituleta duniani na hivyo hawana budi kututimizia yote tuliyostahili katika malezi yetu. Lakini lililo kubwa zaidi ni kwa sababu ya upendo waliokuwa nao kwetu sisi watoto wao. Kwa ajili yetu walijinyima hata waliyostahili kuyapata ili mradi watufurahishe. Kwa ujumla bila ubishi wamechangia sana maendeloe yetu hapa tulipo.

  Wamepata shida wakati wa kutulea, Kukosa usingizi wakati tuna njaa, tunaumwa, na hata wakati tulipokuwa tunalia bila sababu.Leo nimejiuliza sana ni zawadi gani nimewapa. Tumepata kazi zenye kutupa kipato tulichonacho, tuna uhakika wa kula na kunywa, tunalala pazuri, tunaoga kwa sabuni na tunavaa nguo safi , tunaburudika na maisha.

  Je wazazi wetu wanafaidi chochote kutoka kwetu? Hata kama wana uwezo tumewahi kuonyesha upendo huo kwao hata kidogo? Tunapotumia laki moja, hamsini elfu, Ishirini elfu, kumi elfu, elfu tano,elfu tatu ,soda, juice au pipi, tunatumia nao? Je tangu mwaka uanze tumewapelekea chochote? Mwezi uliopita tumewatumia hata salamu? Je leo tumewakumbuka hata kuwaombea maisha marefu? Au sasa nisomapo haya ndipo nakumbuka?

  Sioni kama wao wamenisahau jinsi mimi nilivyowasahau. Maana salamu zao nazipata kila wapatapo nafasi ya kunitumia.Wazazi wakipewa chochote hata kidogo kutoka kwetu hushukuru na mwisho wa shukrani husema mwanangu Mungu akubariki? Tujiulize tunasababu gani ya kukosa baraka hizi kutoka kwa wazazi wetu? Ni ajabu hatukumbuki kuwapa salamu tu au hata shati la shilingi elfu tano? Au pair ya khanga ya shilingi 3,500/= Je hatuna uwezo? Elfu mbili au tatu tunaziona kuwa nyingi na kuwanyima wazazi wetu. Lakini mbona kwa brother, kwa Sister au kwa pombe ni kidogo sana . Ndugu zangu kama tumesahau basi leo tukumbuke.
  Watumie hata elfu moja na Mungu atakubariki sana kama watakavyosema. Jiulize ni mara ngapi tumekosa bahati ya kuombewa baraka na wazazi wetu. Neno la mzazi ni tendo katika maisha yetu. Maana yake linafanya kazi kubwa katika maisha yetu. Tunaikosaje bahati hii?
   
 2. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Amen!
   
 3. CPU

  CPU JF Gold Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Ndaga mama
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Majukumu ya familia yametuzidi,kadi za michango kibao,bidhaa zimepanda bei hata wazazi hatuwakumbuki
   
 5. CPU

  CPU JF Gold Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Utashangaa hela za bia na vimada zipo kibao
   
Loading...