Elections 2015 Soma uchambuzi wa Humphrey Polepole juu ya mafanikio mgombea wa CCM John Pombe Magufuli

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA UJENZI: UWEZO NA KASI YA MAGUFULI KULETA MABADILIKO YA KWELI
Ni vigumu sana kuzungumzia sekta ya ujenzi na mafanikio yaliyofikiwa na wizara ya ujenzi katika kipindi cha miaka takribani ishirini iliyopita bila kutaja Jina la Dkt John Pombe Magufuli mgombea urais wa CCM. Dkt Magufuli amekuwa naibu waziri na waziri katika wiraza ya ujenzi katika serikali ya awamu ya tatu na ya nne. Ni dhahiri pia kwamba kutokana na umahiri wake katika kusimamia sekta hii nyeti kwenye maendeleo ya taifa lolote duniani, Dkt. Magufuli aliaminiwa na kupewa dhamana ya kutoa mchango wake katika ujenzi wa taifa letu kwenye sekta nyingine.

Hata pale alipohamishwa kupelekwa katika sekta nyingine kama vile ardhi na baadae mifungo na uvuvi bado alidhihirisha uwezo wake katika kujenga na kusimamia mifumo na taasisi za utendaji wa serikali katika sekta husika. Pengine msomaji utajiuliza ni kwanini Dkt. Magufuli alirejeshwa tena kwenye wizara ya ujenzi baada ya kuhamishiwa sekta ya ardhi na baadae mifugo na uvuvi katika serikali ya awamu ya nne? Je ni nini hasa mafanikio katika sekta ya ujenzi chini ya uongozi wa Dkt Magufuli?

Hebu tutathmini uwezo na dhamira ya kiongozi huyu katika kujenga na kubadili mifumo ya utendaji wa kitaasisi kwa kupitia baadhi tu ya mafanikio yaliyofikiwa kwenye sekta ya ujenzi nchini. Ni muhimu sana kuweka bayana vielelezo vinavyompambanua Dkt. Magufuli kuwa mgombea pekee anaekidhi vigezo vyote vinavyohitajika katika kuleta mabadiliko ya kweli ambayo ndio kiu ya Watanzania kupitia uchaguzi mkuu 2015.

Miaka kumi na tano tu iliyopita haikuwa rahisi kusafiri kwa gari dogo kutoka nchini Tanzania kwenda nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia au Msumbiji. Vilevile ilikuwa ni vigumu kutumia gari dogo kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, kutoka wiaya moja kwenda nyingine nchini Tanzania.

Hata magari makubwa ya abiria na mizigo yalitumia muda mrefu sana kuliko ilivyo hivi sasa kusafiri ndani na nje ya nchi kwa kutumia usafiri wa barabara. Maana yake ni kwamba muda wa kusafiri ulikuwa mwingi na gharama kusafiri au kusafirisha zilikuwa juu. Kinyume chake, unapoboresha mtandao wa barabara nchini zikiwemo zile zinazoiunganisha Tanzania na nchi nyingine kunapunguza gharama na muda wa kusafiri, kunafungua fursa za biashara za ndani na nje na kurahisisha upatikanaji wa masoko na huduma za jamii.

Wizara ya Ujenzi chini ya uongozi wa Dkt Magufuli ndio yenye jukumu la kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara na madaraja kwenye mtando wa barabara ambao umeendelea kupanuka hadi kufikia urefu wa kilometa 35,000 nchi nzima. Kwa mujibu wa Takwimu za mwaka huu zilizotolewa na Wizara ya Ujenzi, katika katika mtandao mzima wa barabara kiometa 12,786 in barabara kuu wakati kilometa 22,214 in barabara za mikoa. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita peke yake (2005-2015) jumla ya kilometa 17,762 zimekuwa katika hatua mbalimbai za ujenzi wa barabara ambapo mafanikio yake yamekuwa ni pamoja kukamilika kwa jumla ya kilomet 5,568 kwa kiwango cha rami. Aidha jumla ya kilometa 3,873 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha rami wakati barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 4,965 zimefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na serikali iko mbioni kuzijenga kwa kiwango cha rami.

Mafanikio katika ujenzi wa barabara chini ya usimamizi wa Dkt Magufuli yamekwenda sambamba na ujenzi wa madaraja. Kwa mfano kabla ya ujenzi wa daraja la Mkapa ilikuwa huwezi kusafiri kwa barabara kwenda Lindi na Mtwara wakati wa msimu wa mvua. Kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita peke yake jumla ya madaraja 12 yamekamilika kujengwa likiwemo daraja la umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji. Mengine ni daraja la Kikwete lililopo mkoni wa Kigoma, na daraja la waenda kwa mguu la mabatini jijini Mwanza.

Aidha, madaraja madogomadogo zaidi ya 7,200 yamejengwa na kukamilika. Madaraja makubwa 7 likiwemo daraja la Kigamboni yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Pia madaraja makubwa 16 yapo kwenye maandalizi ya kujengwa yakiwemo ya Ubungo na TAZARA interchange mkoani Dar es Salaam pamoja na Interchange tano (5) katika barabara ya Dar es Salaam-Chalinze ambazo zitajengwa maeneo ya Charambe, Kisarawe, Kibamba, Mlandizi, na Chalinze.
Hapa ni vigumu kupinga ukweli kwamba Dkt magufuli ndiye aliyeleta mabadiliko na maboresho katika sekta ya Ujenzi hususani wa miundo mbinu ya barabara.

Taswira ya sasa ya sekta ya ujenzi ambayo sio tu kwamba ina mifumo bayana na thabiti licha ya changamoto kadhaa. Sekta ya ujenzi inasimamiwa na taasisi madhubuti ambazo zinalenga kutafsiri dira na mikakati ya sekta katika uhalisia na vitendo.

Akiwa Naibu wa waziri wa ujenzi katika serikali ya awamu ya tatu, ni Dkt. Magufuli ndie alibadilisha mfumo wa kutegemea wahisani kwa asilimia miamoja katika sekta ya ujenzi wa barabara.

Mfumo huu umefanikiwa kwa kiwango kikubwa. Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya Ujenzi, takribani asilimia sabini (70%) ya miradi yote ya ujenzi wa barabara inchini inajengwa kwa kutumia fedha za serikali.

Ni asilimia thelasini (30%) pekee ya miradi yote ya ujenzi inafadhiliwa na wahisani. Swali la kujiuliza ni je nini kimefanikisha utelekezaji wa mfumo huu? Swali hili huwezi kulijibu bila kuweka bayana uwezo na uzoefu wa mgombea huyu wa uraisi kupitia CCM katika kubadili mifumo kwa kujenga taasisi zinazotakiwa ili kusimamia na kuendeleza mifumo.

Ni Dkt. John Pombe Magufuli ndie alieanzisha harakati za maboresho katika usimamizi, utekelezaji na uendelezaji wa sekta ya ujenzi nchini.
Kiongozi huyu amesimamia kuanzishwa kwa taasisi kadhaa muhimu katika sekta ya ujenzi. Hizi ni pamoja na Mfuko wa barabara (Road Funds) ambao mapato yake yameongezeka kutoka shilingi bilioni 73.08 mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 751.7 mwaka 2014/15.

Hili ni ongezeko la asilimia 928.6. Taasisi nyingine ni Wakalawa barabara (TANROADS) inayosimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara na madaraja. Pia zipo taasisi kama Wakala wa Majengo Tanzania (TBA); Board ya Usajili wa Wahandisi (ERB); Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRD na Bodi ya Usajili wa Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB).

Taasisi zote hizi zinalenga kutelekeza majukumu tofauti lakini yanayotegemeana katika ustawi wa sekta ya ujenzi. Hapa unaweza kuona mantiki ya ujenzi wa mfumo sio porojo.

Watu wengi ikiwa ni pamoja na wafuasi wa vyama vya upinzani vya UKAWA wamekuwa wakikiri kuwa wanafurahishwa na utendaji wa Dr. Magufuli na kwamba ni kiongozi shupavu mchapakazi na mwenye uwezo mkubwa kiutendaji. Hata hivyo watu hawa wanahofia kwamba kiongozi huyu akiingia madarakani utendaji wake utakwamishwa na kile wanachokiita mfumo mbovu wa chama chake cha CCM. Hoja hii imejengeka kwenye nadharia finyu kuhusu mfumo na mabadiliko.

Nadharia hii inaamini kwamba mfumo huzalisha watu wa aina moja kifikra, mtazamo na uzoefu wa maisha ndani ya mfumo. Hoja hii inakinzana na uhalisia wa maisha ya kila siku unaodhihirisha kwamba licha ya mfumo kutaka kuzalisha watu wa aina fulani binadamu wana utashi wa kupima faida na hasara ya kufuata au kutofuata mfumo fulani.

Mara nyingi wale wanaonufika na mfumo husika wangependa kuona mfumo unaendelea hivyo watu hawa hupambana kutimiza matakwa ya mfumo husika ili kulinda maslahi yao.

Katika hili hakuna asiefahamu kuwa Dkt. Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia kile anachoamini kuwa ni haki na wajibu wa kiongozi kwa maslahi ya Watanzania hata kama ni kinyume cha mfumo wa kisiasa ndani ya chama chake. Ifahamike kuwa msimamo huu ndio hasa chanzo cha wananchi wengi kumkubali Dkt. Magufuli kuwa ni kiongozi mchapaka kazi, mahili, na shupavu asieogopa kutekeleza matakwa ya kisheria. Ni dhahiri pia watu waliozoea ubabaishaji, ufisadi na matumizi mabaya ya nafasi walizonazo ndani ya CCM au serikalini au hata kwenye mashirika yasiyo ya serikali pamoja na sekta binafsi wanahofia kuvurugwa kwa mifumo iliyokuwa ikiwanufaisha endapo Dkt.

Magufuli atakuwa raisi wa Tanzania. Hofu na wasiwasi wa makundi tajwa inatokana na rekodi ya utendaji wa Dkt Magufuli. Hivyo anaposema ataondoa ubabaishaji, rushwa, na ufisadi, sio hadithi wala propaganda bali ni jambo ambalo ameshalifanya katika sekta ya ujenzi na wahusika wanaelewa vema kuwa Dkt Magufuli akichaguliwa kuwa raisi mwisho wa mifumo ya kifisadi utakuwa umefika.

Nilipata fursa ya kuongea na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Ujenzi ili kujua staili ya utendaji kazi ya mgombea huyu anejipambanu kwa kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu. Huku wakijivunia kufanya kazi chini ya uongozi wa Dkt Magufuli baadhi ya watendaji walibainisha kuwa mgombea huyu anamaanisha anachokisema kwenye majukwaa maana ni mtu anaependa kuona mipango inatafsiriwa katika vitendo.

Wengine alikwenda mbali na kusisitiza kuwa yale ambayo Dkt Magufuli anaahidi kufanya sio propaganda bali mengi tayari misingi yake ya kisera imeshaandaliwa katika muktaza wa Mpango wa maendeleo wa muda mrefu (Long Term Perspective Plan (LTPP 2011/12-2025/26).

Mfano mzuri ni suala la kujenga na kufufua viwanda ambalo kimsingi lipo kwenye mpango miaka mtano (2016/17-2020/21) ambao utajikita zaidi kwenye maendeleo ya sekta ya viwanda.

Ilielezwa pia na watendaji wizarani hapo kuwa Dkt. Magufuli ni kiongozi ambae ukiwa makini na bidii katika kazi yako utamfurahia lakini ukiwa mzembe, mbabaishaji, na ukakosa uadilifu hawezi kukuvumilia.

Watendaji pia wanakiri kwamba Dkt Maguli amebadilisha kwa kiwango kikubwa utamaduni wa utendaji na uwajibikaji katika wizara ya Ujenzi kiasi kwamba watendaji hawa wanaona tofauti ya kiutendaji kati yao na watendaji katika wizara nyingine za serikali. Ikiwa Dkt Magufuli amethubutu kufanya mabadiliko katika sekta ya ujenzi na nyingine alizowahi kuziongoza akiwa ni waziri wa wizara tu wala sio hata waziri mkuu, nini kitamzuia kubadili mifumo kwenye sekta na idara zote za serikali akiwa raisi wa nchi hii?
 
Uchafu mtupu. Polepole alikuwa wapi kuyaandika hayo yote kabla ya Magufuli hajateuliwa?
Kijana anatafuta dume.
 
Huo ni uchambuzi au uchafuzi???? Kweli njaa za watu kali sana, hii ccm tutaing'oa tu. Huyu hawezi hata kutofautisha kazi ya uchambuzi na uchafuzi!!! Lowasa anasema elimu ni bure hadi chuo kikuu, mtaelimika tu hata kwa fimbo lowasa akichukua madaraka
 
Polepole yuko mahali anaota, anasikiliza Redio Uhuru _ "Rais Magufuli amemteua Bw Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba…….." Bado yuko ndotoni.
 
Magufuli ndiye raid wetu ajaye,kama hutaki wewe Ni lofa na unapaswa kuchapwa viboko hadhalani.
 
Lowasa akiwahinda makanali wawili wa jeshi, kinana na Kikwete basi yeye atakuwa meja general. Lowasa hachomoki kwa mbinu za kirai na medani za porini.
 
Huyu kijana ni mnafki sana hafai na nilishawahi kusema kama yeye anadhani ccm hii ni kama ya mwalimu Nyerere basi agombee uongozi ndani ya ccm kama atapata.Chezea ccm wewe walimtupia Nyerere virago na azimio lake la arusha kabla hajafa na kuanzisha azimio la zanzibar itakuwa huyu pondaponda???haijui ccm na kama hatabadilika hataijua kamwe.Nyerere aliishia kulalamika tu kwenye tv wala hakuwa na uwezo wa kuwafanya chochote rejea hutuba zake za mwisho.Huko kwenye maadili ya uongozi na miiko yake walishaondoka miaka mingi sana wanaelekea kuleeeeeeee wanaitafuta kaanani ya ccm.teh,teh..
 
Looking for cheap popularity. Kati ya watu wapuuzi kabisa Tanzania ni Polepole.
Mtu asiyekuwa na msimamo, kabisa na sina uhakika kama anajielewa.
Angekuwa wa maana kama angetwambia kuwa Magufuli na Lowassa wote ni walewale kwa sababu wote waliipinga katiba ya Walioba.

Shida amejiingiza kwenye kampeni za wazi kwa ccm na bahati mbaya kuna vitu anaeleza kama sisi tunaomwangalia hatuna akili kabisa!

Mie nimemdharau na kumpuuza kabisa. Kwa sasa nikishamuona kwenye Tv nabadilisha chanel haraka sana!!
Polepole anachambua mambo kishabiki sana jambo lililomwondolea sifa ya kuwa mchambuzi kwa kuwa anapiga Kampeni za CCM kwenye Tv.
 
MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA UJENZI: UWEZO NA KASI YA MAGUFULI KULETA MABADILIKO YA KWELI
Ni vigumu sana kuzungumzia sekta ya ujenzi na mafanikio yaliyofikiwa na wizara ya ujenzi katika kipindi cha miaka takribani ishirini iliyopita bila kutaja Jina la Dkt John Pombe Magufuli mgombea urais wa CCM. Dkt Magufuli amekuwa naibu waziri na waziri katika wiraza ya ujenzi katika serikali ya awamu ya tatu na ya nne. Ni dhahiri pia kwamba kutokana na umahiri wake katika kusimamia sekta hii nyeti kwenye maendeleo ya taifa lolote duniani, Dkt. Magufuli aliaminiwa na kupewa dhamana ya kutoa mchango wake katika ujenzi wa taifa letu kwenye sekta nyingine.
Hata pale alipohamishwa kupelekwa katika sekta nyingine kama vile ardhi na baadae mifungo na uvuvi bado alidhihirisha uwezo wake katika kujenga na kusimamia mifumo na taasisi za utendaji wa serikali katika sekta husika. Pengine msomaji utajiuliza ni kwanini Dkt. Magufuli alirejeshwa tena kwenye wizara ya ujenzi baada ya kuhamishiwa sekta ya ardhi na baadae mifugo na uvuvi katika serikali ya awamu ya nne? Je ni nini hasa mafanikio katika sekta ya ujenzi chini ya uongozi wa Dkt Magufuli?
Hebu tutathmini uwezo na dhamira ya kiongozi huyu katika kujenga na kubadili mifumo ya utendaji wa kitaasisi kwa kupitia baadhi tu ya mafanikio yaliyofikiwa kwenye sekta ya ujenzi nchini. Ni muhimu sana kuweka bayana vielelezo vinavyompambanua Dkt. Magufuli kuwa mgombea pekee anaekidhi vigezo vyote vinavyohitajika katika kuleta mabadiliko ya kweli ambayo ndio kiu ya Watanzania kupitia uchaguzi mkuu 2015.
Miaka kumi na tano tu iliyopita haikuwa rahisi kusafiri kwa gari dogo kutoka nchini Tanzania kwenda nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia au Msumbiji. Vilevile ilikuwa ni vigumu kutumia gari dogo kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, kutoka wiaya moja kwenda nyingine nchini Tanzania. Hata magari makubwa ya abiria na mizigo yalitumia muda mrefu sana kuliko ilivyo hivi sasa kusafiri ndani na nje ya nchi kwa kutumia usafiri wa barabara. Maana yake ni kwamba muda wa kusafiri ulikuwa mwingi na gharama kusafiri au kusafirisha zilikuwa juu. Kinyume chake, unapoboresha mtandao wa barabara nchini zikiwemo zile zinazoiunganisha Tanzania na nchi nyingine kunapunguza gharama na muda wa kusafiri, kunafungua fursa za biashara za ndani na nje na kurahisisha upatikanaji wa masoko na huduma za jamii.
Wizara ya Ujenzi chini ya uongozi wa Dkt Magufuli ndio yenye jukumu la kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara na madaraja kwenye mtando wa barabara ambao umeendelea kupanuka hadi kufikia urefu wa kilometa 35,000 nchi nzima. Kwa mujibu wa Takwimu za mwaka huu zilizotolewa na Wizara ya Ujenzi, katika katika mtandao mzima wa barabara kiometa 12,786 in barabara kuu wakati kilometa 22,214 in barabara za mikoa. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita peke yake (2005-2015) jumla ya kilometa 17,762 zimekuwa katika hatua mbalimbai za ujenzi wa barabara ambapo mafanikio yake yamekuwa ni pamoja kukamilika kwa jumla ya kilomet 5,568 kwa kiwango cha rami. Aidha jumla ya kilometa 3,873 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha rami wakati barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 4,965 zimefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na serikali iko mbioni kuzijenga kwa kiwango cha rami.
Mafanikio katika ujenzi wa barabara chini ya usimamizi wa Dkt Magufuli yamekwenda sambamba na ujenzi wa madaraja. Kwa mfano kabla ya ujenzi wa daraja la Mkapa ilikuwa huwezi kusafiri kwa barabara kwenda Lindi na Mtwara wakati wa msimu wa mvua. Kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita peke yake jumla ya madaraja 12 yamekamilika kujengwa likiwemo daraja la umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji. Mengine ni daraja la Kikwete lililopo mkoni wa Kigoma, na daraja la waenda kwa mguu la mabatini jijini Mwanza.
Aidha, madaraja madogomadogo zaidi ya 7,200 yamejengwa na kukamilika. Madaraja makubwa 7 likiwemo daraja la Kigamboni yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Pia madaraja makubwa 16 yapo kwenye maandalizi ya kujengwa yakiwemo ya Ubungo na TAZARA interchange mkoani Dar es Salaam pamoja na Interchange tano (5) katika barabara ya Dar es Salaam-Chalinze ambazo zitajengwa maeneo ya Charambe, Kisarawe, Kibamba, Mlandizi, na Chalinze.
Hapa ni vigumu kupinga ukweli kwamba Dkt magufuli ndiye aliyeleta mabadiliko na maboresho katika sekta ya Ujenzi hususani wa miundo mbinu ya barabara. Taswira ya sasa ya sekta ya ujenzi ambayo sio tu kwamba ina mifumo bayana na thabiti licha ya changamoto kadhaa. Sekta ya ujenzi inasimamiwa na taasisi madhubuti ambazo zinalenga kutafsiri dira na mikakati ya sekta katika uhalisia na vitendo.
Akiwa Naibu wa waziri wa ujenzi katika serikali ya awamu ya tatu, ni Dkt. Magufuli ndie alibadilisha mfumo wa kutegemea wahisani kwa asilimia miamoja katika sekta ya ujenzi wa barabara. Mfumo huu umefanikiwa kwa kiwango kikubwa. Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya Ujenzi, takribani asilimia sabini (70%) ya miradi yote ya ujenzi wa barabara inchini inajengwa kwa kutumia fedha za serikali. Ni asilimia thelasini (30%) pekee ya miradi yote ya ujenzi inafadhiliwa na wahisani. Swali la kujiuliza ni je nini kimefanikisha utelekezaji wa mfumo huu? Swali hili huwezi kulijibu bila kuweka bayana uwezo na uzoefu wa mgombea huyu wa uraisi kupitia CCM katika kubadili mifumo kwa kujenga taasisi zinazotakiwa ili kusimamia na kuendeleza mifumo. Ni Dkt. John Pombe Magufuli ndie alieanzisha harakati za maboresho katika usimamizi, utekelezaji na uendelezaji wa sekta ya ujenzi nchini.
Kiongozi huyu amesimamia kuanzishwa kwa taasisi kadhaa muhimu katika sekta ya ujenzi. Hizi ni pamoja na Mfuko wa barabara (Road Funds) ambao mapato yake yameongezeka kutoka shilingi bilioni 73.08 mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 751.7 mwaka 2014/15. Hili ni ongezeko la asilimia 928.6. Taasisi nyingine ni Wakalawa barabara (TANROADS) inayosimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara na madaraja. Pia zipo taasisi kama Wakala wa Majengo Tanzania (TBA); Board ya Usajili wa Wahandisi (ERB); Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRD na Bodi ya Usajili wa Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB). Taasisi zote hizi zinalenga kutelekeza majukumu tofauti lakini yanayotegemeana katika ustawi wa sekta ya ujenzi. Hapa unaweza kuona mantiki ya ujenzi wa mfumo sio porojo.
Watu wengi ikiwa ni pamoja na wafuasi wa vyama vya upinzani vya UKAWA wamekuwa wakikiri kuwa wanafurahishwa na utendaji wa Dr. Magufuli na kwamba ni kiongozi shupavu mchapakazi na mwenye uwezo mkubwa kiutendaji. Hata hivyo watu hawa wanahofia kwamba kiongozi huyu akiingia madarakani utendaji wake utakwamishwa na kile wanachokiita mfumo mbovu wa chama chake cha CCM. Hoja hii imejengeka kwenye nadharia finyu kuhusu mfumo na mabadiliko.
Nadharia hii inaamini kwamba mfumo huzalisha watu wa aina moja kifikra, mtazamo na uzoefu wa maisha ndani ya mfumo. Hoja hii inakinzana na uhalisia wa maisha ya kila siku unaodhihirisha kwamba licha ya mfumo kutaka kuzalisha watu wa aina fulani binadamu wana utashi wa kupima faida na hasara ya kufuata au kutofuata mfumo fulani. Mara nyingi wale wanaonufika na mfumo husika wangependa kuona mfumo unaendelea hivyo watu hawa hupambana kutimiza matakwa ya mfumo husika ili kulinda maslahi yao.
Katika hili hakuna asiefahamu kuwa Dkt. Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia kile anachoamini kuwa ni haki na wajibu wa kiongozi kwa maslahi ya Watanzania hata kama ni kinyume cha mfumo wa kisiasa ndani ya chama chake. Ifahamike kuwa msimamo huu ndio hasa chanzo cha wananchi wengi kumkubali Dkt. Magufuli kuwa ni kiongozi mchapaka kazi, mahili, na shupavu asieogopa kutekeleza matakwa ya kisheria. Ni dhahiri pia watu waliozoea ubabaishaji, ufisadi na matumizi mabaya ya nafasi walizonazo ndani ya CCM au serikalini au hata kwenye mashirika yasiyo ya serikali pamoja na sekta binafsi wanahofia kuvurugwa kwa mifumo iliyokuwa ikiwanufaisha endapo Dkt.
Magufuli atakuwa raisi wa Tanzania. Hofu na wasiwasi wa makundi tajwa inatokana na rekodi ya utendaji wa Dkt Magufuli. Hivyo anaposema ataondoa ubabaishaji, rushwa, na ufisadi, sio hadithi wala propaganda bali ni jambo ambalo ameshalifanya katika sekta ya ujenzi na wahusika wanaelewa vema kuwa Dkt Magufuli akichaguliwa kuwa raisi mwisho wa mifumo ya kifisadi utakuwa umefika.
Nilipata fursa ya kuongea na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Ujenzi ili kujua staili ya utendaji kazi ya mgombea huyu anejipambanu kwa kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu. Huku wakijivunia kufanya kazi chini ya uongozi wa Dkt Magufuli baadhi ya watendaji walibainisha kuwa mgombea huyu anamaanisha anachokisema kwenye majukwaa maana ni mtu anaependa kuona mipango inatafsiriwa katika vitendo. Wengine alikwenda mbali na kusisitiza kuwa yale ambayo Dkt Magufuli anaahidi kufanya sio propaganda bali mengi tayari misingi yake ya kisera imeshaandaliwa katika muktaza wa Mpango wa maendeleo wa muda mrefu (Long Term Perspective Plan (LTPP 2011/12-2025/26). Mfano mzuri ni suala la kujenga na kufufua viwanda ambalo kimsingi lipo kwenye mpango miaka mtano (2016/17-2020/21) ambao utajikita zaidi kwenye maendeleo ya sekta ya viwanda.
Ilielezwa pia na watendaji wizarani hapo kuwa Dkt. Magufuli ni kiongozi ambae ukiwa makini na bidii katika kazi yako utamfurahia lakini ukiwa mzembe, mbabaishaji, na ukakosa uadilifu hawezi kukuvumilia. Watendaji pia wanakiri kwamba Dkt Maguli amebadilisha kwa kiwango kikubwa utamaduni wa utendaji na uwajibikaji katika wizara ya Ujenzi kiasi kwamba watendaji hawa wanaona tofauti ya kiutendaji kati yao na watendaji katika wizara nyingine za serikali. Ikiwa Dkt Magufuli amethubutu kufanya mabadiliko katika sekta ya ujenzi na nyingine alizowahi kuziongoza akiwa ni waziri wa wizara tu wala sio hata waziri mkuu, nini kitamzuia kubadili mifumo kwenye sekta na idara zote za serikali akiwa raisi wa nchi hii?

Naamini hakuna kazi bila malipo kalipwa shilingi ngapi ya kuandika haya madudu
 
Back
Top Bottom