Soma taratibu kisa hiki kilichonitokea kisha nishauri

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
6,600
2,000
Wakuu,

Mwezi mmoja uliopita nilikuja nyumbani (kwa wazazi) kwa ajili ya Pasaka, hapa nyumbani pia nilijumuika na mdogo wangu wa mwisho (anasoma chuo) hapa nitamwita Denis (sio halisi) na mtoto wa Bro wangu (form two) hapa nitamwita Rama.

Namshukuru Mungu Tumesherehekea vizuri Pasaka na kila mtu akawa anasubiri tu siku zake ziishe akaendelee na majukumu yake.

Kilichonifanya niandike hiki kisa hapa ni hiki tukio ambalo linanifikirisha sana.

Hapa nyumbani wanamiliki duka la la Dawa (lipo mbali kidogo na nyumbani) ambalo Mama yetu ndio huwa anauza,Katika kukaa kwetu hapa nyumbani Mara kadhaa huwa tunamsadia Bi Mkubwa kuuza hasa anapokuwa na ratiba zinazombana.Sasa katika kukaa kwetu hapa dukani huyu Rama amekuwa akijumuika na rafiki zake kadhaa hapa dukani ambo huwa anapiga stories za hapa na pale.Mara nyingi mimi huwa nawaacha hapo nje mimi nakuwa ndani dukani lakini kwa sababu huwa wanakuja Mara kwa mara nami wametokea kunifahamu japo ila hawajanizoea sana nadhani pia sababu mimi sio rika lao na Mara nyingi sichangamani nao.

Kadri muda ulivyozidi kwenda hawa washikaji wa Rama walizidi kupungua nadhani shule zilianza kufunguliwa,hivyo akabaki mmoja ambaye ndie aliendelea kuja hapa dukani.

Kuna siku Rama na Denis walitangulia badae na mimi nikajumuika nao,nilipofika dukani Denis alikuwa amekaa kwa nje Rama na rafiki walikuwa wamekaa kwa ndani wanapiga stori.Nilipoingia huyu rafiki yake Rama(tumwite Dogo) akanisalimia nikakaa nikaanza kuperuzi kwenye simu.Baada ya muda huyu Dogo akaniita bro nikasema nambie,akasema bro uko vizuri sana,nikamuuliza kwanini akajibu "unajua huwa nina tatizo la kutotulia yani moyo unakuwa haujatulia ndio maana umenikuta nimesimama hapa mara nikae"(ni kweli alikuwa amesimama mbele ya hizi kabati za za kioo dukani),akaendelea" lakini tangu ulipoingia tu hapa moyo wangu umetulia kabisa sisikii hiyo hali tena uko vizuri bro" na aliongea tukiwa wote watatu(Mimi,Rama na yeye Dogo).Kwa haraka sikumwelewa anamaanisha nini nikamuuliza huo ni ugonjwa gani? Akasema ndio hivyo tu huwa inatokea,basi mi nikamjibu tu aisee sijawahi kuusikia nikaamua kupotezea wakaendelea kupiga stori na Rama.

Baada ya muda akanirudia tena akauliza bro umeoa?nikamwambia nimeoa,akauliza watoto wako ndio wale mapacha wa kike?nikamuuliza unawafaham?akajibu nilishawahi kuwaona hapa dukani,basi nikamwambia wale sio mapacha labda wanafanana tu.,basi nikatoka nje maana nikaona maswali ya Dogo yamekuwa personal sana.

Siku ya Jumatano iliyopita Rama akaenda shule kwakuwa shule yao ilishafunguliwa hivyo nikabaki mimi na Denis hapa Shop lakini Denisi Mara nyingi huwa hakai sana, hapa akikaa sana ni saa moja na hapo atakuwa bize na simu au laptop anaangalia movie mara atanambia ngoja nimcheki mshikaji fulani ataondoka hapo atakuja kunipitia muda wa lunch,kwahiyo muda mwingi nipo mwenyewe tu.

Baada ya kuondoka Rama bado huyu Dogo ameendelea kuja hapa dukani(nilikuja kujua kwamba yeye alimaliza form four mwaka Jana anasubiri kupangiwa shule) na mara nyingi anakaa muda mrefu anaweza asiongee mwanzoni kama dakika 10 baada ya hapo ataanza maswali yake ambayo kwangu mimi ni 'personal' sana kwa mfano juzi aliniuliza mke wako yupo wapi?nikamwambia nimemwacha mara akaomba simu yangu mara moja nikamwambia siwezi kukupa,wewe simu mtapeana na na wenzako wa saizi yako,akaniliuliza kwani una umri gani nikamwambia,baada ya kuona labda nimemzidi sana sijui hakuamini au vipi akasema mi muongo,akaanza kunitajia umri ambao anahisi ninao wa kuzaliwa miaka ya tisini sijui mara akauliza chuo nimemaliza lini,nimeoa lini,nikachoka maswali yake maana nikaona kama anavuka mipaka hivi nikamwambia hebu tulia usiniulize maswali tena kuna kitu nafanya,nikaweka simu kwenye chaji,sasa wakati simu haijajifunga akaona picha ya mwanamke kwenye scrini,akaanza ndio wife wako huyu,mara mzuri sjiui naomba nimuone basi nikamwambia acha hio simu nikaenda nikaifunga akakaa akatulia.

Sasa nikawa natafakari huyu Dogo ni wa aina gani maana kiumri yeye ni mdogo sana kwangu,yeye amezaliwa 2004,(nilimuuliza)lakini naona anataka kujenga mazoea na mimi ya haraka nikawa sipati jibu nikaamua kupotezea tu,wakati mwingine akianza kuongea namkatisha namwambia tulia kuna kitu nafanya hapa kwenye simu ili tu asilete stori zake. Kimuonekano ana sura ya 'mama'ila yupo kawaida tu.

Sasa tangu juzi nikaanza kupata wasiwasi huenda hayuko sawa maana amejenga mazoea kila akija akishanisalimia tu ataanza kunisifia mara "uko vizuri bro" uko smart,you are so super,mi nampotezea namwambia kawaida tu,anasema sio kawaida bro, you are so super nk.

Juzi jioni alikuja anaanza kunisifia kama kawaida yake ila safari hii akawa kwa mfano tukikaa kwenye benchi akisifia viatu atajitahudi avishike mara,atashika suruali atasema nzuri mara shati mi namwambia za kawaida tu.Au wakati mwingine akiongea atanishika bega ilimradi mikono yake haitulii.

Jana mchana amekuja ila safari hii kaenda mbali zaidi maana kila akianza kuongea kwanza ananiangalia sana machoni halafu kwakua tulikaa kwenye viti katikati kuna meza kila akiongea lazima huku chini anikanyange halafu akianza kunisifia mara una vidole vizuri akaanza kunishika vidole vya viguu,nikarudisha miguu nyuma,akaanza tena una ngozi laini huku ananishika vidole vya mikono,sasa mpaka hapo nikahisi hizi huyu dogo labda 'sio rizki'ila nikasema ngoja nimwache ili nipate uhakika wa ninachofikiria,basi nilikuwa naperuzi humu JF simu nimeshika mkononi nikaamua kuwasha 'sound recorder' on halafu nikaendelea kuperuzi.

Nikamuuliza Dogo mbona kila ukija unanisifia sana halafu huwezi kukaa bila kunishika una maana gani?

Mazungumzo niliyorekodi yalikuwa hivi;

Mimi; Mbona kila ukija unanisifia sana na kupenda kunishika?

Dogo; Uko super bro kila nikikuangalia ulivyo,ngozi yako akaanza kunishika vidole vya mikononi nikamwacha tu akawa kama kainuka kainamia mezani,akaendelea akasema bro mi nimekupenda,napenda kukushika tu

Mimi: Kwanini unapenda kunishika?

Dogo; Bro napenda kukushika tu kuna raha fulani napata nikikushika,nikishika hivyo vinyweleo nasisimka sana,nahisi utakuwa mtamu sana wewe.

Mimi:Kwanini unapata raha kumshika mwaume mwenzio na sio mwanamke?

Dogo; Mwanamke nikimshika sisikii raha,wewe una vinyweleo vingi mwanamke hana,wanaume mna vinyweleo vingi na ndevu sio kama wanawake

Mimi; Basi utakuwa una matatizo kwanini upate raha kumshika mwanaume mwenzio na sio mwanamke?

Dogo; Ni kweli bro ila ndio udhaifu wangu huo,ndio nimezaliwa hivyo sasa nifanyeje,kwani wewe nikikushika husikii raha yeyote?(hapo akataka aanze kunishika shingoni nikamzuia nikamwambia akae)

Mimi; Sisikii raha yoyote kushikwa na mwanaume wala sipendi

Dogo; Mimi napenda tu nimshike mwanaume kuanzia kichwani,kidevuni, nishuke hadi chini kule 'penyewe' hebu simama nione kama hujasisimka

Mimi; Penyewe wapi?

Dogo; Penyewe bro,jiongeze tu,mi nikimshika akishamwaga tu basi nami naridhika tu,

Kifupi nilimhoji sana akasema yeye ameanza kufanya hivyo akiwa shuleni huko anawashika wanaume wenzake, nilipomuuliza Je mtu unayemshika akisisimka unamfanyaje,akaishia kunambia jiongeze bro kwani we mke wako akikusisimua unamfanyaje basi nikapata jibu kuwa dogo atakua analiwa,anasema anademu ila anasema mademu wazinguaji tu.

Baada ya kuthibitisha hili nikaingiwa na wasiwasi asjie akawa alishamtega Rama pia(Mtoto wa bro),nikaamua kumhoji kiujanja janja kwamba kwanini asiwatafute marafiki zake aliokuwa nao kama kina Rama na wengine,akasema yeye hapendi kila mtu ila ana 'watu wake'anaowapenda hao niliomtajia eti damu zao haziendani.

Nikamuuliza wazazi wake wanajua?akasema hawajui.

Nilijaribu sana kumshawishi amwambie baba yake au mama kwamba anatatizo hilo akasema hawezi kufanya hivyo,nikamwambia nenda basi kwa dokta mwambe najisikia kupenda wanaume wenzangu dokta atakusaidia akasema hawezi kwenda kwakua yeye haumwi ni udhaifu tu alionao,ni homoni tu zinamsumbua na mimi pia nina udhaifu wangu kwahio dokta hawezi kumsaidia chochote.

Mwisho nikamwambia haoni kwamba akiendelea ipo siku wazazi wake watajua tu?akakaa kimya baadae nikamuuliza Je utaoa,akasema ataoa tu Mungu atamsaidia,nikamwambia sasa ukioa halafu uendelee kupenda wanaume huoni kwamba mkeo atajua,akasema we achana nayo hata hivyo hii tabia ilishawai kumletea matatizo japo hakusema ni matatizo gani.

Baadae Denis alipitia tukale na yeye akainuka akaondoka lakini,hili suala lilifikirisha na kunihuzunisha sana na kwa sababu inawezekana wazazi wake hawajui chochote kwamba mtoto wao ameshaharibika inaumiza sana.

Usiku mida ya saa 1 alikuja tena yupo na haraka akasema wazazi wake wamesharudi ila anaomba nimpe Condom ataniletea hela kesho ana kazi nayo,nikamuuliza ya kazi gani,hakusema,nikamwambia siwezi kukupa bila hela akaniambia basi usifunge narudi na hela sasahivi,kweli baada ya dk kumi akarudi na hela nikampa akasema amewaambia kwao kwamba anaenda kanisani asubuhi sana saa 12 kasoro lakini haendi kanisani kuna mahali anaenda,akaondoka zake.

Wito wangu kwa wazazi,Tufuatilie sana mienendo ya watoto wetu wa kiume,tusihangaike na watoto wa kike peke yake tukaamini wa kiume wapo salama,tuwachunguze sana,dunia umebadilika mno.

Kuhusu Ushauri;

Kwangu mimi naweza kumdhibiti vizuri tu hata nikilazimika nitampiga marufuku kufika hapa kwahio ushauri ninaoomba ni huu;

1. Je nimuulize Rama(Mtoto wa Bro)kama anajua kuhusu tabia za rafiki yake au nimkataze tu waache kabisa urafiki bila kumweleza sababu?

2. Je nimweleze pia Denis (Mdogo wangu) kwamba huyu Dogo ana tabia hizi ili ajue?maana pia huwa anapiga nae stori japo kwa muda mfupi(maana kuna mahali kwenye audio amekiri kumkubali pia).

3. Je mnahisi huyu Dogo anaweza kusaidiwa kwa namna gani ili aachane na huu ushoga?ni kweli homoni ndio zinamuendesha au ni tabia tu aliyojizoeza/kuzoeshwa?
 

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
5,648
2,000
Daahhh double trouble... kwanza umefanya jambo jema sana hukukurupuka kuongea na dogo na ukamskiliza hujataka kumnyanyapaa!ila nikwambie kitu hakuna mtu anajua kusaundisha km shoga mchekee kidogo akija mara y pili na ya tatu sijui km utasalimika..
wana mdomo sukari sana
 

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
6,600
2,000
Wewe uje Mda mfupi ujue
Asijue Rama anaeishi nae? Pengine ndo boyfriend wake .. umewahi fikiria?
Ndio hicho pia nilikiwaza,lakini nimeeleza huko juu kwamba nilimchomekea kijanja kumuuliza kwamba kwanini asipende rafiki zake kama kina Rama akasema hawamvutii,

Kingine Rama hawapo nae mtaani muda wote sababau Rama anasoma shule ipo mkoa mwingine kabisa Bording huwa anakuja likizo tu na huyu nae alikuwa bording mkoa tofauti kwahio wanakutana hapa hom seasonally tu,ndio maana nina asilimia fulani labda naye hajui
 

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
6,600
2,000
Moyo wangu unafukuta kwa uchungu.
Pekee yetu kama wazazi hatuwezi kabisa..tufanye yatupasayo na yaliyondani ya uwezo wetu kama wazazi..mengine tuyakabidhi mikononi mwa Mungu.

Nasikia uchungu mnooooo ni huzuni sana
Inatia uchungu sana,ila kama ulivyosema tuwe makini sana ila pia tumwombe Mungu awalinde,Maana huwa nikiwaona wazazi kina kitu moyoni huwa kinanihuzinisha
 

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,307
2,000
Inasikitisha sana

Kwakuwa wewe upo hapo kwa muda tu, yaache yalivyo. Ama ikikugusa sana basi andaa ujumbe wa siri(barua) au jitahidi upate namba ya baba yake umtumie ujumbe unaoeleza kama ulivyotueleza hapa. Huku ukimshauri baba yake achukue hatua atazoona zinafaa kumsaidia mwanaye
 

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
6,600
2,000
Wazazi wa huyo mtoto mwenye na huo mchezo mchafu.anza na baba mzazi kwanza yeye baba atamweleza mkewe.

Usiishie kusikitika tu mkuu..fanya kitu ndugu yangu.ukijaribu kuvaa Viatu vya mzazi..unaweza ukajikuta unaua...huu uchungu hauelezeki
Kuwaeleza wazazi wake kwangu ni ngumu sana kwanza sio watu ninaofahamiana nao ziadi ya kuwaona tu wakipita,pili Mimi huku ni kama mgeni tu maana huwa sikai hapa,halafu sasa tuhuma zenyewe nitakazopekeka kwao ni nzito mno,sijui kama kuna mzazi ataamini kirahisi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom