thechosenone
Member
- Jan 10, 2016
- 17
- 5
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba ametoa ripoti yake ambayo ni mwanzo wa mwendelezo wa maandalizi yao katika kuukaribisha msimu wa 2017/18.
Aristica Cioaba ambaye ni raia wa Romania ametoa mapendekezo kadhaa kuelekea msimu huo mpya ambapo baadhi ya mambo yaliyomo kwenye ripoti yake ni haya yafuatayo:
Kwanza ni kuwepo na ongezeko la wachezaji wanne wazawa wasiozidi miaka 26.
Pili anahitaji kambi nzuri na tulivu ya siku zisizozidi 10 nje ya Chamazi, pia apate michezo sita ya kirafiki kabla ya ligi kuanza.
Aidha katika mapendekezo yake hayo amesisitiza kuwepo na chakula bora kwa muda wote.
Pia kuondoka kwa John Bocco, kumemfanya kocha huyo kupendekeza ongezeko la mshambuliaji mmoja mwenye uzoefu.
Ikumbukwe kuwa hadi sasa tayari Azam FC imepandisha wachezaji watano katika kikosi cha wakubwa kutoka kile cha vijana, wachezaji hao ni: Yahaya Zaidi, Stanley Stanslaus, Abbas Kapombe, Abdul Haji na Said Issa.
CHANZO: MZUNGU WA AZAM ANATAKA MRITHI WA JOHN BOCCO, RIPOTI YAKE HII HAPA…