hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,539
Hata mie najiuliza endapo waliochukua pesa watawajibika je kwa upande wa watumishi.wa mungu itakuwaje?? Mtumishi wa mungu Pengo chukua hatua na wewe kuhusu hawa watumishi kwani ni hatari pia, pia natoa ushauri kuhusu bank ya mkombozi kwa kuonekana ni bank inayotumia fedha chafu nayo meneja mkuu achukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wafanyakazi wengine.
Mkuu, kuna sheria za nchi na taratibu za dini husika..hata kama ni kiongozi wa dini akiua, akibaka, akifanya utapeli asihukumiwe kwa sababu ya dini?! Kusiwe na double standards..endapo inathibitika wao(Viongozi wa dini wachukuliwe hatua pia(kidini na kikatiba pia)...Hakuna aliyejuu ya sheria ('Sheria ni msumeno'). Shida ni kwamba msumeno huu hukata wanyonge tu na mafisadi wako juu ya sheria.
Hebu imagine fedha hizi angekuwa amekula mwalimu mkuu pengine fedha kwa ajili ya kutengeneza "maabara" madawati, au diwani n.k. Hii ungeisikia katika vyombo vya habari na kusimamishwa kazi mara moja na hukumu yake ingepitishwa right away. Lakini mafisadi tunawabembeleza na hadi leo wako kazini, yaani mwisho wa mwezi huu watalipwawa mshahara na bado watapokea marupurupu, hao viongozi wa dini walivyo wanafiki(No offence to their followers) wako kimya kama magogo tu na wao.
Wonderful enough watu wanategemea the highest/Worst adhabu watakayopata ni kusimamishwa kazi. Hivi kungekuwa na sera(kwa mfano) Anayethibitika ni mwizi/mbadhirifu n.k anyongwe(kama China kama sijakosea) au afungwe maisha baada ya kurudisha fedha na kufilisiwa unadhani upuuzi huu tungekuwa tunajaza thread hapa za ESCROW ESCROW ESCROW?..Hapana. Lakini kutokana na mazoea toka katika familia(mkubwa wa familia akikosea anajipa msamaha lakini watoto au wengineo wapate adhabu kali ili iwe fundisho) ndiyo hii inayotokea (mkubwa yuko juu ya sheria) ingawaje haipaswi kuwa hivyo.