Soma jinsi wazazi wako wanavyokwamisha au kufanikisha maendeleo yako, muhimu sana

Mikael P Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,933
0
Je, umewahi kuwashukuru wazazi wako kwa kuwa tu ni wazazi wako?

Miaka michache iliyopita nilikutana na mtu moja Mjini Dsm. Tulikutana kwenye foleni ya kuingia kwenye ofisi mojawapo na kukawa na foleni kubwa. Yeye ni mwongeaji kidogo, kwa hiyo tukaanza kuulizana kwa lengo la kufahamiana huku tukisubiri muda wetu wa kuingia ofisini ufike. Yeye akaniuliza wewe ni nani na unafanya nini – nikajieleza.

Kisha mimi nikamwuliza yeye pia. Baada ya mimi kumwuliza swali lile lile aliloniuliza yeye, nikaona yeye ameshtuka sana – akavuta pumzi. Kisha akasema mimi kujibu swali lako kuhusu jina langu na ninakotoka ni historia ndefu na ngumu kidogo. Ni kama sauti yake na sura yake ilibadilika – akajikaza sana. Baadaye akaniambia mimi bwana jina langu... (Jina kapuni) huwa najiita tu mtu wa Morogoro lakini sijui kwa kweli asili yangu hasa ni wapi.

Akaendelea. Mimi nilitupwa na wazazi wangu nikiwa na wiki moja karibu na Nyumba ya masista wa kanisa katoliki Pale Morogoro. Kwa hiyo,masista walinilea mpaka nikakua na sasa nimeanzisha taasisi ya kulelea watoto Yatima. Kwa maana hiyo, mimi sijui mama halisi, sina baba, sina shangazi wala mjomba, sina ukoo wala kabila, … sina ndugu yo yote. Na jina lake la pili ni la kutunga. Hivi kama wewe ndo ungekuwa yeye ungejisikiaje? Bila shaka ungejisikia vibaya.

Swali langu kwako, je, umeshawahi kumshukuru wazazi wako kwa jinsi walivyohangaika na wewe tangu tumboni hadi leo? Hivi umesha wahi kumwambia baba au mama uso kwa uso kuwa nashukuru kwa kuwa wewe ni baba/mama yangu na asanteni kwa matunzo yenu? Maana hata kama baba na mama hawajakufanyia mambo Fulani Fulani uliyoyataka lakini wewe unaitwa Fulani bin Fulani – wengine hawana koo wala majina ya baba zao – hawana wazazi kama hao ulionao wewe. Nina maanisha umewahi kumwambia uso kwa uso mama/Baba asanteni kwa kuwa wazazi wazuri? Au ndo una miezi 6 hadi mwaka hata simu yenyewe hupigi?

Inawezekana wazazi wako hawajakuachia Mali au ghorofa, lakini una jina la pili, wamekuachia ukoo na kabila. Inakupasa kuwashukuru kwa hilo.

Je, unajua kwa nini biblia inasema; WAHESHIMU BABA NA MAMA ILI SIKU ZAKO ZIPATE KUWA NYINGI KATIKA NCHI UPEWAYO NA BWANA MUNGU WAKO? Kinyume chake, wadharau mama na baba ili siku zako ziwe chache katika nchi upewayo na Bwana Mungu wako.

Nilimsikia Mhubiri moja wa kimarekani kwenye TV siku moja (Joyce Mayer?) alisema, Mtu asiyemjua Mungu, mwenye dhambi, mlevi,mwizi nk anayewajali wazazi wake atafanikiwa hapa duniani mara mia kuliko Mchungaji, askofu, Padre au kiongozi wa dini yo yote aliyewasahau wazazi wake.
Mtume Paulo kwa Timotheo anasema, Heri wasioamini kuliko wamini wasiowatunza wa kwao.

Mwl Christopher Mwakasege (Mtz) aliwahi kutoa ushuhuda wa vijana watatu wa mama moja mtanzania waliokwenda majuu wakasahau nyumbani na hasa mama yao. Mtoto moja yuko Marekani, mwingine Uingereza na Ujerumani huko mama anakaa kwa njaa– wasikilizaji wa kanda za mwakasege watakuwa wamewahikukutana na ushuhuda huu. Siku moja mama akaamua kuwalaani wanawe. Jambo la kushangaza ni kwamba, wote watatu walikutwa na matatizo yanayofanana ya uhamiaji kwa wakati moja. Na wote wakarudishwa Tanzania ndani ya mwezi moja kila moja na tatizo tofauti lakini la uhamiaji.

Niwape siri marafiki zangu.. kuna uhusiano wa karibu kati ya mafanikio yako kazini na kwenye biashara na jinsi unavyowatunzaji wako. Mzazi akiwa na kinyongo na wewe hata kama hamjagombana – watoto wa mjini wanasema- hutoki. Mgawie kidogo ulicho nacho uone Baraka zitakazo kufuata.

Mama yangu hajui tarehe yake halisi ya kuzaliwa kwa hiyo, leo nimeamua kumkumbuka na kumshukuru kwa staili hii. Nawe fanya hivyo na kama wazazi wako wako mbali kwa kuwapigia simu nawe utabarikiwa na Mungu.

Usiku mwema wapendwa.
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,969
2,000
Sometimes stress huwa zinasababisha mtu anaanzisha mada nzuri yenye mantiki.
Big up mwanzisha mada.
 

LebronWade

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,615
2,000
Mkuu kuwasaidia ni jambo la heri...lakini ukisema eti uende kuwapa props kwa kufanya vitu ambavyo essentially ni majukumu ya asili tuliyoletewa hapa binadamu tufanye..kwani na wewe unawajibika kwa wanao

In the same token,huwezi sema kukuzaa ni favour wamekupa,ni wajibu wa asili na hamna mjadala...wakikufanyia vibaya there is a price to pay kutoka kwa muumba,na mtoto timiza wajibu kama mungu alivoelekeza,baaasii

Haya mengine ya kulamba binadamu miguu kwa kutimiza wajibu wao kwa nafasi zao ni ukichaa

Cha msingi ni kila mtu atimize wajibu wake,asietimiza moto utamuwakia,no matter who he/she is,iwe mtoto au mzazi...haya mambo ya kusema ukasujudi mtu ni ushen.zi ulipitiliza kabisa
 

Chagga King

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
1,770
2,000
Mkuu kuwasaidia ni jambo la heri...lakini ukisema eti uende kuwapa props kwa kufanya vitu ambavyo essentially ni majukumu ya asili tuliyoletewa hapa binadamu tufanye..kwani na wewe unawajibika kwa wanao

In the same token,huwezi sema kukuzaa ni favour wamekupa,ni wajibu wa asili na hamna mjadala...wakikufanyia vibaya there is a price to pay kutoka kwa muumba,na mtoto timiza wajibu kama mungu alivoelekeza,baaasii

Haya mengine ya kulamba binadamu miguu kwa kutimiza wajibu wao kwa nafasi zao ni ukichaa

Cha msingi ni kila mtu atimize wajibu wake,asietimiza moto utamuwakia,no matter who he/she is,iwe mtoto au mzazi...haya mambo ya kusema ukasujudi mtu ni ushen.zi ulipitiliza kabisa
...even the person uliyemuweka katika avatar, hakuwa na mawazo kama yako, unajua ni kwann watu wanamshukuru Mungu, je waache kumshukuru Mungu kwa madai kuwa kuumba ni wajibu wa Mungu???

think both sides before you open your mouth.
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,448
2,000
Suala la uumbaji ni fumbo moja gumu sana. Wazazi kama wazazi wanayo nafasi ila si wale wenye mlengo wa kishetani. Ndiyo maana hata Yesu Kristu alipata kusema hakuja kuleta amani bali ni mafarakano (moja wapo ni kati ya wazazi na watoto). Hivyo mzazi ni wajibu wake kukuzaa, ila hana mamlaka ya kukuamulia au kukuongoza maisha yako kwa remote control. Kwa hiyo mimi nawapenda wazazi wangu na ninawaheshimu sana. Ila huyo jamaa ajue Mungu anampenda kwani usikute wazazi wake walimtupa wakijua Mungu mkuu yupo ambaye ndiye Baba na Mama halisi na ndiyo maana akalelewa na masista na sasa anaishi vizuri. Pia haijalishi eti maendeleo yako yanategemea wazazi, hilo nakataa.

Juhudi zako binafsi bila kujali wazazi wako wanasemaje, na mzazi hana mamlaka ya kuzuia maendeleo yako. Nasema hivyo kwa sababu kuna watu ambao wanamaendeleo wakati huo huo ni wauji, wachawi, hawana maelewano na wazazi wao. Mbegu ya maendeleo imependikizwa sawa kwa kila mwanadaamu ni wewe kuamua tu kama unataka kuwa masikini au tajiri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom