Soma hiki kisa cha mtu aliewahi kuwaliza TAKUKURU pesa zao

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Miaka fulani kuna mzee mmoja alikuwa akifanya kazi taasisi moja ya umma, kama mnavyojua taasisi nyingi za umma ili upate tenda lazima utoe kitu kidogo au ili ulipwe madai yako baada ya kutoa huduma lazima utenge fungu kadhaa la wakubwa kula.

Basi huyo mzee kama kawaida akaomba kitu kidogo yake toka kwa mteja mmoja mwenye asili ya kiasia, yule mteja akaona hiyo kitu kidogo ni kubwa sana ikabidi aamue kwenda kumchoma mzee wa watu kwa watu wa TAKUKURU ili kumkomoa huyo kigogo wa Serikali.

Kweli m- asia akaenda kwa wabaya wa kigogo wa Serikali ya government, akawapa watu wa TAKUKURU mkanda mzima, ikapangwa mipango kabambe ya kumnasa mtumishi wa umma mpenda rushwa ili wamkomoe, basi m-asia akarudisha majibu kwa mtu jamaa kuwa kesho ataleta mpunga kama walivyokubaliana. Kwa bahati nzuri au mbaya wakati mipango inapangwa dhidi ya yule kigogo, mtonyaji mmoja ndani ya wanaopanga mipango akamstua yule kigogo kuwa hizo hela ulizoomba usizipokee, umetegwa. Jamaa akapokea ushauri akautafakari sana na akashukuru kwa kupewa nyeti na jamaa yake ila akadhamiria kuwa hizo hela lazima azile ni nyingi, hawezi kuziacha.

Basi jamaa ofisi yake ilikuwa ndani ya jengo la ghorofa ila ofisi ilikuwa ghorofa ya kwanza, jamaa akaenda ofisini akalisoma jengo zima lilivyo na kwa kuwa alikuwa kaambiwa namna atakavyoshikishwa mzigo, akaexploit weakness kwenye mchakato mzima na akawa ana uhakika kuwa hizo hela zinaliwa kabla jua halijachomoza.

Jamaa akachukua gari yake double cabin akaenda nayo ofisini, akaipaki nyuma ya ofisi upande wa dirisha la ofisi yake, akaenda na dereva wake, akamsomesha kuwa gari iwe silence muda wote na nikidondosha box kwenye gari wewe ondoka hapa fasta. Kweli bana mhindi akafika na box lake na watu wa TAKUKURU, kama ilivyo ada mhindi akatangulia na mzigo ili akamkabidhi jamaa na akitoka tu ndani ya dakika 3 jamaa wanavamia ofisi kumtia mtu hatiani.

Baada ya mhindi kuingia na kukabidi mzigo, akatoka na jamaa wakajua biashara imekwisha tunaenda kumkamata mtu na box lake bila kujua kuwa baada ya mhindi kufungua mlango tu anatoka jamaa akalirusha lile box kwa chini, likadondoka kwenye gari na dereva alikuwa tayari akaondoa gari kwenda nyumbani fasta. Kama movie hivi.

Baada ya dakika 3 hivi watu wa TAKUKURU wakavamia ofisi na mavitambulisho yao na mibastola juu wanataka box la hela, box halipo na hakuna mtu mwingine aliyetoka nje baada ya yule mhindi. Jamaa wakasema haiwezekani maana wana uhakika jamaa hajatoka nje na isingewezekana akatoka kwenda kuficha box la hela, ofisi ikapekuliwa mwanzo mwisho hakuna kitu na jamaa anawahakikishia kuwa huyo mhindi hajaja na kitu humu, jamaa wana uhakika mhindi kaingia na box la hela kwa macho yao kabisa halafu box halionekani, wakatoa bastola kumtishia, jamaa anawaambia niueni ila mimi sijapewa chochote na huyo mhindi.

Wakati wanaendelea kupekua hela zilishafika home na zimehifadhiwa mahala salama kwa ajili ya kuanza kutafunwa na watoto wazuri.

Jamaa akachukuliwa hadi polisi na yule mhindi akakamatwa aseme hela amampa nani, mhindi anasema hela kampa jamaa na jamaa anasema hela sijapewa, ikabidi jamaa aachiwe na mhindi akajambishwa hadi akalipa ule mpunga. Mhindi alikuja kumuomba jamaa radhi na bado jamaa akamkamua tena.

Hivyo ndivyo jamaa alikula hela za TAKUKURU. Asikwambie mtu simba ni mkali sana ila bado anapewa mimba.

Ndio maana unashangaa pamoja na Magu kuwa mkali balaa ila watu waloshamsoma na wanaendelea kupiga hela kama kawaida, kama wanakunywa juice.
 
Na sijajua hiyo miaka ya nyuma unayozungumzia ni ipi? Sheria ya Rushwa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2007 ht usipopokea hongo kitendo tu cha kushawishi na kuomba kukiwa na ushahidi wa kushawishi na kuomba unatiwa hatiani

Mkuu miaka ya nyumba haina maana lazima iwe ni miaka ya Nyerere, hata 2010 ni miaka ya nyuma, 2015 ni miaka ya nyuma

Ushahidi unautoa wapi, kama ingekua hivyo si kula mtu angefungwa, hnaenda tu TAKUKURU unasema nimeombwa rushwa na flani basi anakamatwa anafungwa.

Ushahidi wa rushwa ni lazima uwe na hard evidence kama hivyo kukamatishwa pesa za TAKUKURU au imefanyika wire transfer kwenda kwenye akaunti yako ya benki ila maneno tu hakuna kitu.
 
Na sijajua hiyo miaka ya nyuma unayozungumzia ni ipi? Sheria ya Rushwa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2007 ht usipopokea hongo kitendo tu cha kushawishi na kuomba kukiwa na ushahidi wa kushawishi na kuomba unatiwa hatiani
Ushahidi wa kushawishi unathibitishwaje?
 
Kuna Dr. Mmoja Alimfungia mgonjwa hela za takukuru kwenye kidonda wametafuta wapi siku ya dressing akazitoa kilaini
 
Miaka flanii kuna mzee mmoja alikua akifanya kazi taasisi moja ya umma, kama mnavyojua taasisi nyingi za umma ili upate tenda lazima utoe kitu kidogo au ili ulipwe madai yako baada ya kutoa huduma lazima utenge fungu kadhaa la wakubwa kula.

Basi huyo mzee kama kawaida akaomba kitu kidogo yake toka kwa mteja mmoja mwenye asili ya kiasia, yule mteja akaona hiyo kitu kidogo ni kubwa sana ikabidi aamue kwenda kumchoma mzee wa watu kwa watu wa TAKUKURU ili kumkomoa huyo kigogo wa serikali.

Kweli m- asia akaenda kwa wabaya wa kigogo wa serikali ya government, akawapa watu wa TAKUKURU mkanda mzima, ikapangwa mipango kabambe ya kumnasa mtumishi wa umma mpenda rushwa ili wamkomoe, basi m-asia akarudisha majibu kwa mtu jamaa kua kesho ataleta mpunga kama walivyokubaliana. Kwa bahati nzuri au mbaya wakati mipango inapangwa dhidi ya yule kigogo, mtonyaji mmoja ndani ya wanaopanga mipango akamstua yule kigogo kua hizo hela ulizoomba usizipokee, umetegwa. Jamaa akapokea ushauri akautafakari sana na akashukuru kwa kupewa nyeti na jamaa yake ila akadhamiria kua hizo hela lazima azile ni nyingi, hawezi kuziacha.

Basi jamaa ofisi yake ilikua ndani ya jengo la ghorofa ila ofisi ilikua ghorofa ya kwanza, jamaa akaenda ofisini akalisoma jengo zima lilivyo na kwa kua alikua kaambiwa namna atakavyoshikishwa mzigo, akaexploit weakness kwenye mchakato mzima na akaw ana uhakika kua hizo hela zinaliwa kabla jua halijachomoza.

Jamaa akachukua gari yake double cabin akaenda nayo ofisini, akaipaki nyuma ya ofisi upande wa dirisha la ofisi yake, akaenda na dereva wake, akamsomesha kua gari iwe silence muda wote na nikidondosha box kwenye gari wewe ondoka hapa fasta. Kweli bana mhindi akafika na box lake na watu wa TAKUKURU, kama ilivyo ada mhindi akatangulia na mzigo ili akamkabidhi jamaa na akitoka tu ndani ya dakika 3 jamaa wanavamia ofisi kumtia mtu hatiani.

Baada ya mhindi kuingia na kukabidi mzigo, akatoka na jamaa wakajua biashara imekwisha tunaenda kumkamata mtu na box lake bila kujua kua baada ya mhindi kufungua mlango tu anatoka jamaa akalirusha lile box kwa chini, likadondoka kwenye gari na dereva alikua tayari akaondoa gari kwenda nyumbani fasta. Kama movie hivi. Baada ya dakika 3 hivi watu wa TAKUKURU wakavamia ofisi na mavitambulisho yao na mibastola juu wanataka box la hela, box halipo na hakuna mtu mwingine aliyetoka nje baada ya yule mhindi. Jamaa wakasema haiwezekani maana wana uhakika jamaa hajatoka nje na isingewezekana akatoka kwenda kuficha box la hela, ofisi ikapekuliwa mwanzo mwisho hakuna kitu na jamaa anawahakikishia kua huyo mhindi hajaja na kitu humu, jamaa wana uhakika mhindi kaingia na box la hela kwa macho yao kabisa alafu box halionekani, wakatoa bastola kumtishia, jamaa anawaambia niueni ila mimi sijapewa chochote na huyo mhindi.

Wakati wanaendelea kupekua hela zilishafika hom na zimehifadhiwa mahala salama kwa ajili ya kuanza kutafunwa na watoto wazuri.

Jamaa akachukuliwa hadi polisi na yule mhindi akakamatwa aseme hela amampa nani, mhindi anasema hela kampa jamaa na jamaa anasema hela sijapewa, ikabidi jamaa aachiwe na mhindi akajambishwa hadi akalipa ule mpunga. Mhindi alikuja kumuomba jamaa radhi na bado jamaa akamkamua tena.

Hivyo ndivyo jamaa alikula hela za takukuru. Asikwambie mtu simba ni mkali sana ila bado anapewa mimba.

Ndio maana unashangaa pamoja na magu kua mkali balaa ila watu waloshamsoma na wanaendelea kupiga hela kama kawaida, kama wanakunywa juice.

Unamaana TAKUKURU ndio walitoa ela za mtego?
 
Back
Top Bottom