Soma hii kama una bahati mama yako mzazi bado yuko hai

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,211
5,936
Kelvin Ferlin
15 hrs ·

NITABAKI NA MAMA YANGU
Kijana mmoja Daktari alikwenda kuposa kwa familia moja yenye uwezo wa kifedha na Mali zao .
Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Baada ya kujua kwamba Mchumba ake alimchukua mama yake aishi naye kwake baada ya kuona mama yake amekuwa ni mzee Sana.

Yule Binti Akamwambia chagua mawili kunioa mimi au kukaa na mama yako pale kwako ?? ,
kwa sababu ukinioa mimi sitokubali kukaa na mama yako pale kwako maana itakuwa ni kwangu sasa mama yako akae pale ili iweje?

Yule kijana daktari alimuelewa. Hakujua la kufanya Kuhusu maisha yake na yule Binti , Mke mtalajiwa , Uku akitafakari Binti anampenda Sana lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu kwakuwa alikuwa wanatoka wote kijiji kimoja pia Ndio kiongozi wake wa maisha yake.

Daktari alimwambia mwalimu :- Mwalimu kama nilivyokueleza awali kwamba nitaenda kuposa kwa wazazi wa yule binti niliyekuambia yaani kwa Kweli moyo wangu unampenda mno yule binti siwezi Fikiria Mwanamke mwingine zaidi yake ,
lakini masharti aliyonipa yule Binti mke mtalajiwa ni kwamba nimfukuze mama yangu pale nyumbani kwangu ,,

kitendo ambacho kinaniumiza Sana Kichwa, mimi siwezi kuishi mbali na mama yangu maana amekuwa mzee.

Mwalimu sasa Nifanye nini na yule Binti nampenda vibaya mno ? Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa yule kijana daktari , alimjibu kwa kumwambia:

Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao wa kukaa naye nyumbani kwako fanya mambo yafuatayo:

Kwanza kabisa rudi nyumbani kwako, na leo usifanye chochote, ila Ukifika muombe mama yako umuoshe Miguu na mikono

Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya wasiwasi wowote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa, mikono kama mgongo wa kenge yote sababu ya kufanya kazi za sulubu wakati wa ujana wake.. ,

mama yake akamwambia mwanangu mikono yangu imegutaa kwasababu ya kufanya vibarua vya kulima viazi na kupalilia mipunga ktk Mashamba Ya watu , Kwaajili Ya kutafuta Ada yako ya shule na uniform ,
Baba yako alifariki ukiwa mdogo Sana...

Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kufanya kazi ngumu kwa ajili ya mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, mashambani, kulima viazi, kukosha nguo, kufyeka barabarani na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea fedha ya halali bila ya kujali ugumu hiyo Kwaajili Ya kumtunza Mwanae .

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana maendeleo mzuri.

Yule kijana Daktari alilia sana akaangalia viganja vya mama yake, akasema nakupenda mama yangu, nitakutunza kwa hali yoyote. .

Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia,

Mwalimu siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya huyo Binti msomi asiyejua thamani ya mama yangu.

Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi Mwalimu ! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya Mwanamke msomi ambaye hajali thamani Ya mama yangu wakati mama yangu ameteseka maisha yake yote kwa ajili ya yangu.

Mwacheni aende tu akaolewe na mwanaume yeyote ampendaye mimi nitabaki na mama yangu. Kama unampenda MAMA YAKO tafadhali usipite bila kucomment neno moja la kumshukuru mam kwa kukulea

Image may contain: 2 people, people sitting
 
Kuna kitu cha kujifunza hasa kwa sisi vijana tunaotarajia kuoa wasichana wa kizazi hiki. Binafsi mazingira kama haya yalinikuta ila nashukuru maamuzi yangu yalifanana na hii story.
 
Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, mashambani, kulima viazi, kukosha nguo, kufyeka barabarani na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea fedha ya halali bila ya kujali ugumu hiyo Kwaajili Ya kumtunza Mwanae.....
 
Bado ungeambiwa muogeshe, mtawadhe akijisaidia na mbebe mgongoni mpeleke hospitali akiugua ,maana yeye aliyafanya yote hayo kwa upebdo mkubwa kwako. Mzazi sio Wa kubeza ukitaka maisha mema hapa duniaini. Mke ni muhinu maishani ila so kwa masharti ya kumkana mzazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Haswa! Mke asiyempenda mama wa mumewe kakosa sifa ya kuitwa mke.
 
Hii story niliisoma sehem, but ilikuwa inamuhusu baba.
Muheshimu baba na mama yako, nawe utabarikiwa na kuwa na wingi wa siku
Mke ishini nao kwa akili.
 
Kuna mabinti wanajiona wana wakwe wakati wala hawatambuliki kwa wakwe zao
Nampenda mama yangu

"رمضان كريم وصوم مقبول"
 
Nimefurahishwa zaidi na gugutaa ndiyo naisikia leo.

ilivyogugutaa


Ila umenitafakarisha sana vipi kama hali ya mama ni tofauti na ya kwenye kisa, mama kama Prof Tibaijuka hivi, msomi maarufu na aliyeshika nyadhifa zake naye kwa mapenzi tu anataka akae nyumba moja na mwana.
 
"watoto wa mama" mna shida sana,kwa mawazo haya mgando mnayoyang'ang'ania tangu ujima eti hakuna kama mama,kwa hiyo hawa akina baba wanaojinyima na kuwa na madeni lukuki kisa kusomesha watoto wao nyi mnaona hawana thamani yoyote?!
msiishi kwa kukariri
 
May God bless my parents, wamejitoa sana kwa ajili yangu nipate kua na maisha mazuri yenye furaha na amani.
Pamoja na wazazi wote wanaopambana kwa ajili ya watoto wao Mungu awabariki sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom