Soma Hekima za Wadau: Ukilewa bangi au pombe na kufanya mambo ya ajabu huyo ndiyo wewe halisi

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,878
2,000
“When You smoke herb it reveals you to yourself. All the wickedness you do is revealed by the herb – it’s you conscience and gives you an honest picture of yourself.”
— Bob Marley

Tafsiri:

Ukivuta bangi inakutambulisha ulivyo. Mambo yote maovu unayofanya baada ya kuvuta bangi yanafunuliwa kwako na mmea (bangi), huo ndiyo uwezo wako wa utambuzi juu ya jambo baya au zuri, huyo ni wewe aliye ndani yako na hukupa picha ya ukweli vile ulivyo.

Naongezea hekima za Titicomb:
Ukifanya mambo ya ajabu au mazuri baada ya kunywa pombe ujue hivyo ndivyo ulivyo, pombe inakusaidia tu ujitambue wewe ni wa namna gani. Yaani ujitambue wewe ni mtu wa ajabu au mzuri kwa kiasi gani.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,180
2,000
Titicomb,

Yaani natetemekaaaaa......

Kuna post fulani, jamaa mmoja alilewa chakari akiwa mwandishi wa Rais, hadi ikabidi msafara wa Rais umsubiri airport, walikuwa wanaenda Saudi Arabia. Baadae akaja kuwa Rais.

Aliuza kila kitu, hadi utu wetu.

Pombe hizi jamani
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,878
2,000
“Every need got an ego to feed.”
- Bob Marley

Tafsiri:

Kila unachofanya kukidhi mahitaji yako au kutimiza malengo yako kimaisha , unafanya hivyo kwa sababu ya sifa tu, yaani unataka ushibishe nafsi yako ile tamaa ya kujisikia wewe ni bora na umefanikiwa kuliko waliokuzunguka au waliokosa hicho kitu ulichofanikiwa kupata.

Hii ni kweli ndiyo maana kila unapofanikiwa kumiliki pesa kiasi flani unatamani pesa zaidi, ukipata gari unataka kumiliki ndege, ukipata mke au mume mmoja mzuri uliyetamani kuwa nae kisha muda mfupi tu unamtamani wengine.
Siyo kwamba unahitaji sana vitu au watu hao ili uishi, ili usife la hasha! Unataka sifa na ukate kiu yako ya kujisikia wewe ni bora kuliko wenzio.
Ukinunua iphone 8 unataka iphone 9 muda mfupi tu...

Ukinunua nguo nzuri na mpya wakati unazo nguo zingine ni kutafuta sifa tu wala haikuwa lazima kama mahitai ya kuishi. You just need to feed your ego, you want to show people who surround you that you have ability to own nice clothes every now and then.

Kwanini unavaa madhahabu ambayo si ya faida yoyote ya kiafya? Hauli wala kuyanywa hayo madhahabu. Wewe unataka ule mng'ao wake ukuwezeshe popote pale ulipo uonekane uwepo wako kuliko wenzio.
Kwanini uishi kwenye nyumba ya vyumba 8 wakati familia yako mpo wanne tu? Wahudumu/wafanyakazi 6 wa nyumbani wanawahudumia watu wanne tu!!
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,878
2,000
Titicomb,

Yaani natetemekaaaaa......

Kuna post fulani, jamaa mmoja alilewa chakari akiwa mwandishi wa rais, hadi ikabidi msafara wa rais umsubiri airport, walikuwa wanaenda Saudi Arabia. Baadae akaja kuwa rais.

Aliuza kila kitu, hadi utu wetu.

Pombe hizi jamani
Mkuu nimecheka sana hadi nahisi watu wamenishangaa huyo jamaa anacheka nini muda huu.
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,878
2,000
Titicomb,

Yaani natetemekaaaaa...

Kuna post fulani, jamaa mmoja alilewa chakari akiwa mwandishi wa rais, hadi ikabidi msafara wa rais umsubiri airport, walikuwa wanaenda Saudi Arabia. Baadae akaja kuwa rais.

Aliuza kila kitu, hadi utu wetu.

Pombe hizi jamani
Kwamba pombe zinaweza kukuonesha watu kama malofa tu au siyo??
Unaweza ukawaona watu wote hapo kijijini kwenu ni malofa tu ukawachana live ukiwa jukwaani kwenye uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa kijiji chenu ...
Kwamba unaweza kuwachana live makavu hata wale ambao rafiki zako ulioonesha kuwaamini kwa miaka 10 au zaidi?

Daah pombe siyo kabisa. Sema nini pamoja na yote hayo zamani niliipenda pombe kiasi chake sikulala bila glasi ya mvinyo mkavu mwekundu.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,180
2,000
Kwamba pombe zinaweza kukuonesha watu kama malofa tu au siyo??
Unaweza ukawaona watu wote hapo kijijini kwenu ni malofa tu ukawachana live ukiwa jukwaani kwenye uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa kijiji chenu ...
Kwamba unaweza kuwachana live makavu hata wale ambao rafiki zako ulioonesha kuwaamini kwa miaka 10 au zaidi?

Daah pombe siyo kabisa.
Asante sana kwa kuelewa haraka.
Tusije tukaonekana tuna wivu wa kike
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,878
2,000
Mimi nikilewa natamani wanawake walionizidi umri.
Yaani huyo ndiyo wewe halisi huyu ambae akiwa hajalewa hatamani wanawake waliomzidi umri ni wewe aliyejivika unafiki au/na uoga wa kuomba mahusiano ya kimapenzi na watu waliomzidi umri.
 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
16,960
2,000
Aiseeeh, mara moja nikiwa safari ya kijamii nilikunywa mvinyo nukajiskia top. Nilikuwa naimba na kucheza tuu non-stop.

Well ntajaribu tena siku nyingine nione Kasinde anafananaje.
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
8,658
2,000
Titicomb,

Yaani natetemekaaaaa......

Kuna post fulani, jamaa mmoja alilewa chakari akiwa mwandishi wa rais, hadi ikabidi msafara wa rais umsubiri airport, walikuwa wanaenda Saudi Arabia. Baadae akaja kuwa rais.

Aliuza kila kitu, hadi utu wetu.

Pombe hizi jamani
Ben?
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,002
2,000
Mimi naamini hata maaumuzi sahihi hufanywa mtu akiwa High either kwa tungi au ganja
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,878
2,000
Mimi naamini hata maaumuzi sahihi hufanywa mtu akiwa High either kwa tungi au ganja
Mimi naamini maamuzi hayo yanatoka rohoni kwako kwa dhati lakini sina hakika iwapo maamuzi yakitoka rohoni kwa dhati ya moyo wako lazima yatakuwa sahihi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom