Soma hapa ujue kwanini wananchi wanataka kuiadhibu CCM jumapili

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,991
1,194
Haya ninayoyasema ni baadhi tu, huwezi kubishana na kifo maana utakayeumia ni wewe,ndivyo ilivyo kwa CCM na serikali yake ambayo kimsingi imeshindwa kuletea wananchi maendeleo.

Nyerere aliwahi kusema maendeleo sio barabara watu wengi hawakumuelewa alimaanisha nini,Leo inaweza kueleweka zaidi kwa watanzania wengi.

Barabara hazina maana kwa uchumi ulioporomoka,barabara hazina maana kwa wananchi kama serikali inayoongoza imejaa wezi,barabara hazina maana kama serikali iliyopo madarakani inatunza MAFISADI,barabara hazina maana kama serikali iliyopo madarakani haiheshimu utawala wa sheria,Barabara hazina maana kama uchumi wa nchi unamilikiwa na wageni kwa asilimia 80%, barabara hazina maana kama serikali inazitumia kutorosha nyara za nchi,barabara hazina maana kama BAJETI ya nchi haimjali mwananchi kwa namna yoyote ile,Barabara hazina maana kama serikali haiwezi kutafuta masoko kwa wakulima, Barabara hazina maana kama kila kukicha wananchi walio wengi wanailalamikia serikali hii iliyokwenda LIKIZO na haijulikani itarudi lini.

BUNGENI Mmejaza wabunge wajinga wajinga muda wote wao ni kutokujua wanaongea nini utadhani vichaa.

Wananchi wanasema hakuna dawa CCM na serikali yake wanasema zipo.Leo hii maji ni shida nchi nzima.

Nenda mahospitalini dawa hakuna muda wote ni danadana tupu huku dawa zikiendelea kuibiwa kila kukicha huku serikali ya CCM ikiangalia tu na kushangaa.Viongozi wamegeuka waigizaji kelele nyingi vitendo hakuna.

Kumbuka mtanzania penye mawazo ya wizi diama hapana maendeleo na katika hili wananchi wengi wameligundua na wanasema CCM ijiandae kisaikolojia kwa kiama kijacho jumapili hii.

CCM na serikali yake ikome kabisa kutoa vitisho kwa mamlaka halali wananchi.
Viongozi wa jeshi la polisi wakome kutishia wananchi wanaotaka kulinda mali zao.

Kamwe hakuna mtu atamzuia mtu kwenda kupiga kura huu ni uongo wa mchana kweupe wa viongozi wa ccm na baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi.

Mjue ni mjinga tu ndie atakae kubali kauli za CCM na jeshi lao la POLISI na hapa tusidanganyane kwa sababu lengo kuu la kulazimisha watu waondoke si fujo hata kidogo ILA NI KUFANIKISHA UINGIZAJI WA KURA FEKI NA KUHONGA MAWAKALA.

TUJIULIZE SWALI LA MSINGI KWA NINI CCM HAWATAKI KULINDA KURA KAMA WENZAO WA UKAWA NA BADALA YAKE WANASHABIKIA WATU KUONDOKA KWA SABABU KUONDOKA KWA WATU NDIO KETE YA MWISHO YA CCM ILIYOBAKIA,KUBAKI AU KUACHIA NGAZI.
NAMWAMBIA KIKWETE NA POLISI WAJUE AMANI YA NCHI IMELALA KATIKA HAKI PEKEE NA SI VITISHO NA MABAVU.

SISI TUNAJUA KWAMBA BABA NA MAMA WA AMANI NI HAKI NA SI MABAVU NA VITISHO.MSILAZIMISHE KUONGOZA UMMA MNAOENDELEA KUUTESA MIAKA YOTE HUKU WATOTO WENU WAKISOMA ULAYA NA MAREKANI NA HUKU WATOTO WETU WAKILA VUMBI MIAKA YOTE TOKA UHURU.

POLISI WAJUE WATAWAPIGA BABA ZAO NA MAMA ZAO,DADA NA KAKA ZAO,BABU ZAO WANAOWAPIGANIA ILI WAPATE STAHIKI ZAO NZURI KWA AJILI YA WATOTO NA FAMILIA ZAO.WAKIPINGA MABADILIKO WAJUE WANAPINGA UTU,MAENDELEO,WANAPALILIA RUSHWA NA UKABILA,WANALINDA WEZI NA WAKUZA UMASKINI,WAJUE WANALEA MFUMO KANDAMIZI AMBAO MWISHO WAKE NI KUZAA WATU WALIOKATA TAMAA YA KUISHI NA MWISHO NI MAUAJI.

KABLA HATUJAFIKA HUKO NI VEMA AKILI ZA VIONGOZI WA SERIKALI NA WALE WA POLISI WATAMBUE HILO NA WAJUE HAKUNA AMANI KATIKA MAZINGIRA YA UPOKAJI WA HAKI NA MAMLAKA YA WANANCHI.

MWISHO KABISA NASEMA WATU WALIOSABABISHA WANANCHI WAKAFIKA HAPA NA KUCHOKA NI CCM NA SERIKALI YAKE HIVYO BASI POLISI NAWASIHI MSITUMIKE VIBAYA MAANA HALI WALIYOISABABISHA CCM KWA WANANCHI NI MBAYA SANA HIVYO BASI POLISI WANANCHI WANASEMA WANATAKA MABADILIKO MIAKA HAMSINI NA NNE YA CCM NA TANU INATOSHA.

WANANCHI WANAKUTAKIENI MEMA KATIKA SAFARI YA MABADILIKO SOTE TUJENGE TAIFA NA SI KUTISHIANA MJUE MNAKAA KWETU MITAANI NA FAMILIA ZENU TUNAZIPENDA CCM WASITUFARAKANISHE KWA UROHO WAO NA UPUUZI WAO WA KIUONGOZI,MADHAIFU YA CCM YANAWEZA KUVUMILIWA NA MWEHU PEKEE NA SI BINADAMU AMBAYE YUKO (MENTAL FIT) TUJENGE UTAMADUNI MPYA ILI NCHI ISONGE MBELE,NA TUKUMBUKE WENZETU WAMEFIKA MBALI SANA UKIONA KENYA,RWANDA,UGANDA,ZAMBIA NA HAO WOTE HAWANA UTAJIRI KAMA WETU KWA MANENO MENGINE WAMEPAA, CCM WASIGEUZE NCHI NI YA KIFALME,HILO TUMELIKATAA NA TUNALIKATAA JUMAPILI KUPITIA DEMOKRASIA AMBAYO TUNASISITIZA SANA SANA SANA SANA IHESHIMIKE WENGI WALETE VIONGOZI NA SI WACHACHE KWA USALAMA NA USTAWI WA TAIFA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NAWATAKIA BARAKA ZA MUNGU MWENYEZI KATIKA KUTENDA HAKI NDANI YA UCHAGUZI HUU NA HAKI HIYO IKAZAE AMANI ILIYO NJEMA KWA USTAWI WA TAIFA LETU.
 
Huu uzi umeandikwa na mmoja wa watu wenye uwezo mkubwa sana wa kufikiri bila kujali itikadi yoyote..JET SALLI hongera mkuu nimekuelewa sana
 
mimi, mke wangu , wasichana wa kazi wawili na wadogo zangu wa tatu = KURA 7 kwa UKAWA (LOWASSA)
 
Huu uzi umeandikwa na mmoja wa watu wenye uwezo mkubwa sana wa kufikiri bila kujali itikadi yoyote..JET SALLI hongera mkuu nimekuelewa sana

Asante kamanda ERICK YUSTO pamoja tulivushe taifa letu ukweli daima fitina mwiko.
 
mabadiliko ni muhimu kuliko kitu chochote tuko pamoja ccm sina hamu nayo,nikiona ile rangi ya t-shirt zao nasikia kutapika
 
Wananchi wasipewe vitisho ukawa wameendesha kampeni za kistaarabu sana sana na wanastahili certificate of political tolerance.Wameonyesha uvumilivu wa hali ya juu sana kisiasa.
 
Huo uzi umeandikwa NA mtu aliyepoteza muda shuleni.uwezo finyu



Wewe unamuda wa zaidi ya mwaka mmoja humu JF na bado akili zako hazina akili! Huwezi kupinga ya kwamba wewe si mvivu! Wewe ni mvivu wa mawazo na fikra! Soma kilichoandikwa kwanza ndio utaweza angalaau KujisAidia ukienda Chooni.
 
Huo uzi umeandikwa NA mtu aliyepoteza muda shuleni.uwezo finyu


Aidia hebu kitendee haki kichwa chako walau kwa dakika 5 tu usikinyime aidia kipe tafakuri ili ujue kwa nn hali ya nchi yako iko kama ilivyo na unadhani CCM imewakosea nn watanzania.
 
Ukishidana na mfanyakazi uliyemwajiri unapumzisha kazi,ndio utaratibu,Leo hii CCM hawataki kutoka madarakani wanalazimisha kututawala ilhali wameshindwa kufanya kazi waliyotumwa kwa miaka mingi CCM imekosa kabisa cha kuwadanganya wananchi mwaka huu imebaki kuwahadaa watu eti ukichagua upinzani kutakuwa vita wakati watanzania maeneo mbalimbali wamechagua upinzani toka 1995 na hatujawahi kuona vita sasa tumejua kwamba kauli za CCM ni za kuchanganyikiwa kwa sababu uongo wao umegota mwisho.
 
Huo uzi umeandikwa NA mtu aliyepoteza muda shuleni.uwezo finyu





Hebu acha upoyoyo wewe...........sasa kati ya wewe na yeye ni nani aliye na ufahamu finyu...........yaaani umeshindwa hata kudadavua maoni rasmi yalipo ndani ya hiyo thread........umeshindwa hata kuelewa maudhui.......ndio kusema wewe mwenzetu maisha yamekunyookea ........na kwa sasa Tanzania hii ukikuta mtu anamafanikio pia ua galagaza huyo mtu anacheza dili haramu na anavunja sheria........ni ngumu sana kwa mtu sasa hivi kujipatia kipato stahiki kwa njia halali......hiyo ni never........kwa sasa uchumi wa tanzania si local tena ni foreign wageni wametutawala ........wao ndio wanafanya maamuzi........wao ndio wanawekeza......wao ndio wanazalisha bidhaa sisi ni wasindikizaji.......mfumo wa elimu unatufanya watumwa tuh ni si wakombozi wa uchumi wetu.........THIS MUST BE STOPPED ........AND THE ONLY CHANCE IS THIS SUNDAY.......!
 
Ukishidana na mfanyakazi uliyemwajiri unapumzisha kazi,ndio utaratibu,Leo hii CCM hawataki kutoka madarakani wanalazimisha kututawala ilhali wameshindwa kufanya kazi waliyotumwa kwa miaka mingi CCM imekosa kabisa cha kuwadanganya wananchi mwaka huu imebaki kuwahadaa watu eti ukichagua upinzani kutakuwa vita wakati watanzania maeneo mbalimbali wamechagua upinzani toka 1995 na hatujawahi kuona vita sasa tumejua kwamba kauli za CCM ni za kuchanganyikiwa kwa sababu uongo wao umegota mwisho.

Wabeja sana mwanawane! Na hiyo TR 25 kesho kutwa ndy itakuwa mwisho wa polisisemu Jamii kama kweli watabaki na msimamo huu wa kukataa watu wen ye nia njema kulinda kura zao.
 
CCM mambo yao mwisho mwaka huu, watashangaa kumbe hadi wale vijana wanyoa kiduku huwa wanapiga kura
 
Back
Top Bottom