Soma Hapa Kama Unataka Kuanzisha Au Kukuza Biashara Yako – Sehemu Ya Pili

guojr

Member
Dec 4, 2015
55
82
Kwenye hatua ya kwanza kama nilivyosema lazima ujue jamii inachangamoto gani. Changamoto zipo nyingi sana hata mtaani kwako na nyingine ni za kitaifa au kidunia kabisa, kwahiyo kadiri changamoto inavyokua kwa watu wengi basi ndio unajihakikishia soko kubwa.

Tunaendela kwa mifano sasa ili upate picha zaidi, mfano nimeona changamoto ya kina dada wenye chunusi, nami nataka kuwatafutia suluhisho la tatizo lao waweze kurudi kwenye muonekano wao mzuri ndani ya wiki 2.

Tatizo la walengwa wangu tayari nimelishalijua, sasa nitafanya nini ili niwatatulie tatizo lao? Inabidi nitafute njia ya kuwasaidia. Hapa nafanya utafiti kupitia kwa watu au mtandao kuona ni njia gani ninaweza kuondoa chunusi ndani ya wiki 2. Kuna mitandao mingi inauza bidhaa za asili zinazotibu shida mbalimbali za kiafya tena kama utanunua bidhaa nyingi kutoka kwao wanaweza hata kukuwekea brand yako.

Nakuwa makini ninapofanya uamuzi wa kununua bidhaa mitandaoni nahakikisha nasoma reviews za watu walionunua hiyo bidhaa tena kwa watu wengi wawe wameweka ushuhuda kuwa hizo bidhaa zimewasaidia. Nanunua bidhaa tofauti tofauti pisi chache kwasababu hapa nataka kujaribu bidhaa kama inafanyakazi kama ninavyokusudia, nawapa rafiki au ndugu zangu wa karibu wenye tatizo la chunusi nione ni bidhaa ipi ni nzuri inayoondoa chunusi ndani ya wiki 2. Nafatilia maendeleo yao hadi watakapo pona kabisa kwani huenda hao ndio wakawa ni wateja wangu wakwanza. Bidhaa itakayofanya vizuri zaidi hiyo ndio itakua bidhaa yangu yakuniingizia mkwanja.

Natengeneza page facebook, instagram na group la WhatsApp, naweka sponsored Ads naandika hivi.

KAMA WEWE UNA TATIZO LA CHUNUSI SUGU NA UMEHANGAIKA KWA MUDA MREFU BASI NAKUKARIBISHA KATIKA GROUP LANGU LA WASAP AMBAPO NITAELEZEA NAMNA GANI UNAWEZA KUJITIBU CHUNUSI NDANI YA WIKI MBILI TU. HUDUMA HII NI BURE KABISA KUINGIA KWENYE GROUP GUSA LINK HAPO CHINI.

Nakuhakikishia watu watamiminika kama mvua, hii ni Sanaa ya uandishi wa matangazo yanoyonasa wateja. Watu wakishaingia kwenye group unatakiwa uwe active, hakikisha unajibu maswali yao vizuri uwe mpole maana watu wengine wanaweza kuandika maneno makali.

Wape ABC za namna ya kutunza ngozi, hizi ABC unaweza kujifunza google au youtube halafu mwishoni unawatambulishia bidhaa yako kuwa unayo bidhaa ambayo inaondoa changamoto yao ndani ya wiki 2 na imesaidia watu wengi. Waambie unatoa punguzo kwa watu kumi wa kwanza watakao changamkia bei hiyo ndani ya saa 24. Mfano kwenye group lako wameingia watu 100 basi hata ukipata wateja kuanzia 5 na kuendelea sio mbaya kwani utakua unauza hiyo bidhaa hata mara 5 ya kiasi ulichonunulia. Idadi ya watu wakao jiunga kwenye group itategemea na bajeti ya sponsored Ad na targeted group hapo umakini unahitajika.

Hayo yote yanawezekana kama umejiandaa kupata mafanikio otherwise utaona nilichoandika kama hadithi za abunuwasi.

Itaendelea… Namna Ya Kufanya Mauzo.
 
Lete madini mkuu vitu nivipendavyo mim kila nkitaka kupractise nafail niliko ni village navipato vyao nividogo
 
Back
Top Bottom