Soma hapa chimbuko la msemo "Ukistaajabu ya Musa,utayaona ya Firauni".

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Wahenga walisema:-

"Ukistaajabu ya Musa,Utayaona ya Firauni".

Katika kijiji cha Chamwino- Dodoma miaka ya 1970, jamaa mmoja alikuwa na familia ya mke (aliyekuwa mjamzito) na mtoto wake wa kwanza mwenye miaka 4.

Ikumbukwe kwanza, mimba zina tabia tofauti kama kuchukia watu, kula maembe mabichi, udongo, ndimu, magodoro, limao au chakula /kinywaji cha aina fulani. Kwa kifupi,mimba huchagua vyakula, vinywaji, marafiki nk.

Sasa mimba ya huyo mwanamke wa huyo jamaa ikawa inapenda "nyama choma".Yaani mwanamke akisikia tu nyama inachomwa mahali, hapakaliki.

Mimba ilipofikisha miezi 6, jamaa akaaga kwenda mjini kutafuta maisha kwa ajili ya familia ambayo ingeongezeka miezi 3 baadae. Kwamba angerudi kijijini baada tu ya mwanamke kujifungua huyo mtoto wa pili.

Mwezi mmoja baada ya kuondoka kijijini, nyumba ya jirani pakawa panatengenezwa nyama choma.Mama mjamzito akamtuma mwanae wa kwanza kwenda kuomba walau "finyango" mbili au tatu ili atoe hamu na msukumo uliokuwa unamsumbua. Yule mtoto alipoenda kuomba nyama,akajibiwa hivi:-

" mwambie hakuna nyama hapa,akaombe kanisani, au mwambie baba ako akanunue,hakuna nyama ya bure".

Yule mtoto akayafikisha maneno kwa mama ake kama yalivyo.Mama ake kwa mstuko mkubwa kwa hali aliyokuwa nayo, mimba ikatoka bahati mbaya!

Mume wake aliporudi toka mjn akaelezwa.Akapanic na kuwa na hasira sana.Akasema lazima amkomeshe huyo baba aliyemnyima mke wake walau finyango mbili.

Akaenda kwa kiongozi wa kiroho aitwaje MUSA.Baada ya kutoa malalamiko yake,Musa akamwambia:-

"Rudi nyumbani na mke wako,muombe Mungu,utapata mtoto mwingine".

Yule bwana akaona haitoshi,akaenda kwa Mtemi wa kimila katika eneo hilo aitwae FIRAUNI.Na baada ya malalamiko yake,akaomba kwa Firauni ili yeye apate mimba yake.Basi Firauni akaagiza askari/nyapara wake wakamkamate yule bwana aliyemnyima nyama mke mpk mimba ikatoka.

Alipoletwa huyo bwana,FIRAUNI akamwambia:-

"Mchukue huyu mwanamke wa huyu jamaa,kamtie mimba, ikishafika ya miezi sawa na ile iliyotoka,mrudishie jamaa mke wake.Mmenielewa?Haya poteeni."

Mwenye mke akashika kichwa na kusema:-

"UKISTAAJABU YA MUSA,UTAYAONA YA FIRAUNI".
 
Hadithi ina ukweli na uwongo
hayo mambo yalitokea enzi za nabii Mussa....nabii mussa alikuwa kiongozi wa wayahudi
huku firauni akiwa ndo mtawala

hilo tatizo lilitokea kwa wayahudi....wakampelekea kesi Musa..
waliposhindwa kukubali hukumu ya Musa ndo wakaenda kwa mtawala Pharaoh...

kulikuwa na kesi kama tatu
 
Wote acheni chai!! Msemo huo chimbuko lake ni kwenye biblia au msahafu, Firauni ni Farao.

Baada ya waisrael kuteseka sana misri Mungu alimtuma Musa kuwakomboa, baada ya Musa kufika kwa Firauni/Farao, aligeuza fimbo kuwa nyoka( hapa lazima ustaajabu) Farao kuona hivyo nae akawaita wachawi wake wakageuza fimbo zao kuwa nyoka pia (hapa utastaajabu pia) "Ukistaajabu ya Musa(fimbo kuwa nyoka) utaona ya Firauni ( fimbo kuwa nyoka)
Nb. Kulingana na simulizi Nyoka wa Musa aliwameza nyoka wa Farao kudhihirisha ukuu wa Mungu kwa Firauni.
 
Wahenga walisema:-

"Ukistaajabu ya Musa,Utayaona ya Firauni".

Katika kijiji cha Chamwino- Dodoma miaka ya 1970, jamaa mmoja alikuwa na familia ya mke (aliyekuwa mjamzito) na mtoto wake wa kwanza mwenye miaka 4.

Ikumbukwe kwanza, mimba zina tabia tofauti kama kuchukia watu, kula maembe mabichi, udongo, ndimu, magodoro, limao au chakula /kinywaji cha aina fulani. Kwa kifupi,mimba huchagua vyakula, vinywaji, marafiki nk.

Sasa mimba ya huyo mwanamke wa huyo jamaa ikawa inapenda "nyama choma".Yaani mwanamke akisikia tu nyama inachomwa mahali, hapakaliki.

Mimba ilipofikisha miezi 6, jamaa akaaga kwenda mjini kutafuta maisha kwa ajili ya familia ambayo ingeongezeka miezi 3 baadae. Kwamba angerudi kijijini baada tu ya mwanamke kujifungua huyo mtoto wa pili.

Mwezi mmoja baada ya kuondoka kijijini, nyumba ya jirani pakawa panatengenezwa nyama choma.Mama mjamzito akamtuma mwanae wa kwanza kwenda kuomba walau "finyango" mbili au tatu ili atoe hamu na msukumo uliokuwa unamsumbua. Yule mtoto alipoenda kuomba nyama,akajibiwa hivi:-

" mwambie hakuna nyama hapa,akaombe kanisani, au mwambie baba ako akanunue,hakuna nyama ya bure".

Yule mtoto akayafikisha maneno kwa mama ake kama yalivyo.Mama ake kwa mstuko mkubwa kwa hali aliyokuwa nayo, mimba ikatoka bahati mbaya!

Mume wake aliporudi toka mjn akaelezwa.Akapanic na kuwa na hasira sana.Akasema lazima amkomeshe huyo baba aliyemnyima mke wake walau finyango mbili.

Akaenda kwa kiongozi wa kiroho aitwaje MUSA.Baada ya kutoa malalamiko yake,Musa akamwambia:-

"Rudi nyumbani na mke wako,muombe Mungu,utapata mtoto mwingine".

Yule bwana akaona haitoshi,akaenda kwa Mtemi wa kimila katika eneo hilo aitwae FIRAUNI.Na baada ya malalamiko yake,akaomba kwa Firauni ili yeye apate mimba yake.Basi Firauni akaagiza askari/nyapara wake wakamkamate yule bwana aliyemnyima nyama mke mpk mimba ikatoka.

Alipoletwa huyo bwana,FIRAUNI akamwambia:-

"Mchukue huyu mwanamke wa huyu jamaa,kamtie mimba, ikishafika ya miezi sawa na ile iliyotoka,mrudishie jamaa mke wake.Mmenielewa?Haya poteeni."

Mwenye mke akashika kichwa na kusema:-

"UKISTAAJABU YA MUSA,UTAYAONA YA FIRAUNI".
 
Wote acheni chai!! Msemo huo chimbuko lake ni kwenye biblia au msahafu, Firauni ni Farao.

Baada ya waisrael kuteseka sana misri Mungu alimtuma Musa kuwakomboa, baada ya Musa kufika kwa Firauni/Farao, aligeuza fimbo kuwa nyoka( hapa lazima ustaajabu) Farao kuona hivyo nae akawaita wachawi wake wakageuza fimbo zao kuwa nyoka pia (hapa utastaajabu pia) "Ukistaajabu ya Musa(fimbo kuwa nyoka) utaona ya Firauni ( fimbo kuwa nyoka)
Nb. Kulingana na simulizi Nyoka wa Musa aliwameza nyoka wa Farao kudhihirisha ukuu wa Mungu kwa Firauni.
Sawa!!!
 
Nilipata kusimuliwa kuwa Mussa na Firauni walikuwa wanaishi sehemu moja na wakawa wanafanya biashara ya nafaka (wanauza), sasa Mussa alifayia marekebisho chombo kinachotumika kama kipimo cha kuuzia nafaka (debe) akakiminya kuwa kidogo na watu wakawa wanalalamika na kushangaa kwa nini anawauzia akiwa ameminya chombo hivyo (mfano debe ni kilo 20 yeye akaminya na kuwa kilo 17) ila bei ni ileile ambayo inatumika kwa kipimo ambacho hakijachezewa. Sasa Firauni yeye kwa nini watu wakamshangaa zaidi kuliko Mussa? Yeye hata hakuhangaika kuminya debe lake, alichofanya ni kugeuza debe kwenye kitako ndio akawa anaweka nafaka na kuuza bei ya debe, ndio watu wakaweka huo msemo, Ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni.
 
Back
Top Bottom