SOMA HADIHII HII YA KUSIKITISHA NA UJIFUNZE

Zepha mastory

New Member
May 19, 2019
4
6
SIMULIZI FUPI



_ SOMA KISHA JIFUNZE_

Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha, kwanini umeruhusu Dunia iniadhibu kiasi hiki. Baba wa mbinguni sina tofauti na mfu, ili kwangu ni pigo la umauti, ni pigo la mwisho, mwili wangu wote umepoa najiona kama nimebebeshwa msalaba wa chuma.

Leo niko katika kaburi la mwanangu Emmanuel, ni miaka saba imepita tangu kafariki. Mwanangu Emma uliniacha katika kipindi kigumu sana, uliondoka pasipo kuniaga, uliondoka Ghafla mwanangu, umeniacha mpweke sana, Leo nimejifunga kile kipande cha kanga ulichoniletea kama zawadi.

Mwanangu kila nikikumbuka kifo chako nashindwa kuvumilia yaani ulikatwa mapanga mpaka ukafariki, nilipofatilia naambiwa ni watu wasiojulikana. jamani nani wakunitunza Mimi, nilibahatika kupata Mtoto mmoja tu ambaye ni Emma.

Dunia kwanini hautendi haki?, kwanini unakuwa na ubaguzi? Dunia nazungumza na Wewe nione huruma basi uliyonifanyia yanatosha.
Mwanangu Emma Leo niko katika kaburi nimeushika msalaba huu kwa maumivu makali sana, nisamehe mwanangu nimeshindwa hata kujengea kaburi lako, udongo umeshuka muda sio mrefu kaburi litatoweka katika uso wa Dunia.

Jamani mwanangu, mama yako sina hata pesa, siku tano bila kula kwangu ni jambo la kawaida sana, kama kulia nimelia sana nasubiri Mwenyezi Mungu atende miujiza, sina wa kumtegemea zaidi yake yeye.

Jamani mwanangu nilikuwa nimelima mahindi angalau nipate chakula lakini, lakini, lakini eeeeeh masikini masikini ya Mungu wakayakata yote wakidai nimevambia hifadhi ya wanyama, nililia sana mwanangu kuona Mnyama anathaminiwa kuliko binadamu.

Wanawake wenzangu nisaidieni kuyafuta machozi yangu, mwenye kipande cha kanga anisaidie niweze kuufunika mwili wangu uliojawa na makovu yasiyopona.

Mwanangu Emma narudia tena niko Juu ya kaburi lako nikipaza sauti unisikie, Leo mama yako nazilaza mbavu zangu nje, yaani kale kajumba nilikoachiwa na marehemu Baba yako kamebomolewa wakidai kwamba tumejenga kwenye hifadhi ya barabara, jamani binadamu wamekoswa huruma kabisa ntaenda wapi mjane mimi!? Nitaenda wapi yatima Mimi wa miaka thelathini iliyopita, Dunia nakuomba unipunguzie Adhabu nami ni binadamu naumia, Nina moyo wa nyama sina moyo wa chuma.

Mwanangu Emma, mama yako sina pakwenda sina pakulala ila Leo nitalala hapa Juu ya kaburi lako mwanangu, nitakesha nawe hapa, nilikuzoea sana mwanangu, niliangaika sana kukulea baada ya Baba yako kufariki, lakini Leo naambulia kulitazama kaburi lako ni machungu kiasi gani haya, niambieni jamani! Niambieni jamani nimekosea wapi nikaombe msamaha.

Emma mwanangu Leo uko ndani ya kaburi ukiwa umefunikwa na udongo mzito, umelala umetulia tuli, kweli kifo hakina huruma, hakiangalii umri wala Mali, eeeh jamani kifo, ni kiumbe gani Wewe kifo hata kwa sisi masikini u atuchukua maisha tunayoishi hapa Duniani ni kama wafu tayari.

Kwanini mwanangu uliamua kuhama duniani, ikawa hakuna budi, ukaamua kwenda zako kwa ya Rabi maanani.

Mwanangu kwanini uliamua
Kuipa dunia mkono wa buriani? Amka unijibu mwanangu kwanini uliamua Kuaga dunia Kuionyesha dunia kisogo? Siamini mwanangu kama uliamua Kutangulia mbele ya haki Kwenda kuzimuni na kuniacha mama yako nikiteseka.

Ilaaniwe tarehe Mbili mwezi wa kwanza mwaka 2011 ni Siku ambayo kijana wangu alifariki Dunia, jamani siwezi kuendelea kuzungumza niacheni nilie, niacheni nilie niambie nitaenda wapi mjane, yatima, masikini mimi tumaini langu liko ndani ya kaburi la mwanangu, nasema asante Dunia, ipo Siku nitaonana na mwanangu pamoja na mume wangu Baba Emmanuel, nazidi kuwaombea wapumzike kwa Amani.

SHARE UJUMBE HUU UWAFIKIE WENGI
FB_IMG_1558510646630.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom