Solo Thang alikuwa Msaada kwangu Masqo katika Mziki wa Bongofleva kuliko Juma Nature na East Coast team.

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
EAST COAST TEAM

Mimi Deogratius Nalimi Kisandu ambaye kwa jina la Kisanii nafahamika kama "MASQO" Kati ya mwaka 2003/2004 nilifika Upanga anakoishi Msanii wa Bongo fleva na mmiliki wa kundi la East Coast Team, King Crazy GK, siku hiyo nilipofika nyumbani kwao GK niliwakuta kundi lote la East Coast Team, walikuwepo O-Ten, Ay, Mwana FA, GK, Snare, na mwanadada Pauline Zongo wengine siwakumbuki vizuri, walinipokea Vizuri sana na tukaongea jinsi ya kuniinua Kimziki, ikumbukwe kipindi hicho nilikuwa bado nina wimbo mmoja tu wa "Nimepata Demu" niliongea nao jinsi ya kunisaidia na kumbuka O-Ten aliniomba nitoe Freestyle kidogo nami nikaonesha kauwezo kangu, ofcourse walinisikiliza wakanisihi nifanye mazoezi sana na niwatafute siku zingine lakini sikuweza kuwatafuta tena maana kwangu nilitaka msaada wa Promo na kusimamiwa Mziki wangu.

JUMA NATURE
.

Baada ya siku kadhaa niliwasiliana na Sir Nature na nikafika kwao KOTA za Temeke, tukaonana na Juma Nature na Tukazungumza lakini hakuwa tayari kutokana na kundi lao kuwa na watu wengi na hivyo sikuweza hata kupata nafasi ya kujumuika nao.

SOLO THANG.

Kwa kweli huyu Mheshimiwa nampa 5 kabisa, Bwana Solo Thang (Msafiri Kondo) niliwasiliana naye na kwa bahati nzuri alipenda kampani yangu sana hasa baada ya mimi Deogratius Kisandu a.k.a MASQO kufika nyumbani kwao Mbagala, nilifika mara nyingi bila kumkuta lakini nilikuja kufanikiwa kumpata hapohapo kwao, Solo Thang alisikiliza wimbo wangu wa "Nimepata DEMU" akaupenda sana na akanambia mimi nimependa Biti na Staili yako ya Kurap, alinitia moyo sana na kuniomba uvumilivu kwenye gemu la Muziki, aliniahidi kunipa Promo kubwa sana, tulianza makubaliano na alikuwa ananisihi niwe mchangamfu maana nilionekana mpore lakini nauwezo wa kuimba vizuri sana.

Kesho yake Solo Thang alienda kwa MAMU STRORE ili aiiuze ile nyimbo yangu ya "Nimepata Demu" ili pesa yake tufanyie Promo lakini alipofika kwa Mamuu Store akaambiwa hii nyimbo tayari iko kwenye Compilation ya BRATON, Solo alikasirika sana, maana Braton kauza nyimbo halafu hakuifanyia Promo, kesho yake aliniita tena kwao Mbagala tukakutana na tukala na ugali nyama choma getoni kwake, Solo Thang alinieleza yote yaliyojiri na kunihurumia sana, nilivyomuona mimi nikama nilitapeleliwa kiaina fulani hivi, alisema labda urekodi wimbo mwingine tuanze upya maana hii biashara ya "Nimepata Demu" imegonga mwamba. Akaniomba Biti yangu ya NIMEPATA DEMU aitumie kurekodia wimbo mwingine lakini mimi sikuafiki tena akanambia basi nikupoze kidogo na kijisenti lakini sikuwa tayari. Kiukweli Solo Thang alinishika sana akili yangu na nina imani nitafanya naye Kolabo hivi karibuni.

Tuliachana na Solo Thang na hivyo sikuweza kumtafuta tena maana nilipata kampani mpya Kiwalani DSM ya wasanii wa maeneo hayo (ZEBE D) na hivyo nikaendelea na mambo mengine mpaka kurekodi "Usiunyanyapae Moyo Wangu" lakini sikumfikiria tena Solo Thang wala East Coast Team.
View attachment 650195
DEOGRATIUS NALIMI KISANDU a.k.a MASQO
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom