Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,216
- 113,510
Jana Rais Samia kwenye uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Mwinyi, alitangaza kuwa katika pia kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais wetu huyo wa zamani aliyetimiza miaka 96, serikali imempatia gari [jipya?] aina ya Mercedes Benz iliyo chini [sedan] kwa sababu aliyokuwa akiitumia [nadhani ni SUV] ilikuwa inampa shida kuipanda na kushuka kutokana na umri wake mkubwa kwa sasa pamoja na kimo chake [hapa nahisi Rais Samia alisema kwa utani].
Tangazo hilo la Rais Samia limezua sokomoko kubwa, hususan mitandaoni.
Mimi sina tatizo na ‘zawadi’ hiyo kwa Rais wetu huyo mstaafu. Kwa maelezo machache aliyoyatoa Rais, sina pingamizi lolote lile.
Ila kuna wengine hawakufurahishwa na jambo hilo. Wamehoji kwamba iweje mtu kama Rais Mwinyi, ambaye katumikia taifa kwa muda mrefu na katika nafasi za juu kabisa, mtu mwenye istihaki nyingi hivyo, ashindwe kujinunulia gari linalomfaa kwa matumizi yake.
Rais Mwinyi keshawahi kuwa waziri. Keshawahi kuwa Rais wa Zanzibar. Na alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Sina hakika kama pia huwa anapata marupurupu ya utumishi wake kama Rais wa Zanzibar au la. Naamini ya urais wa Jamhuri ya Muungano anayapata.
Sasa mimi nina maswali kadhaa:
1. Je, hilo gari alilopewa hivi sasa ni la kwake? Limesajiriwa kwa jina lake? Yeye ndo analilipia bima?
Mimi muda wote huu nimekuwa nikidhani kuwa marais wastaafu huwa wanapewa gari ya matumizi na serikali na kwamba magari hayo huwa ni mali ya serikali.
Yaani, Rais mstaafu huwa anapewa gari, ofisi, watumishi wa ofisi, walinzi, na kadhalika.
2. Kama hivyo ni ndivyo, ni kapewa au wamembadilishia tu gari ya matumizi na siku atayoacha kuitumia itarudishwa ilikotoka?
3. Kama wamembadilishia tu gari, Rais angesema ‘tumembadilishia’ gari la matumizi kuliko kusema ‘tumempa’ gari jipya kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa, ingekuwa ni bora zaidi na isingezua sokomoko?
Tatizo nilionalo hapa ni kuhusu timing, optics, na word choice tu.
Zaidi ya hapo kelele zilizopigwa sizioni kama ni hoja zilizo compelling.
Rais Mwinyi siyo raia wa kawaida. Hawezi kulinganishwa na wazee wengine ambao hawajawahi kuwa marais.
Rais Samia kusema ile majuzi kuwa serikali haina hela za kutosha kuwapa posho wazee, hiyo haina maana serikali haina hela za kuwatunza marais wa zamani.
So this is much ado about nothing.
Go ahead and click that ‘Thanks’ button if you agree with me. Even if you don’t agree but you appreciate the content, go ahead and smash that button.
Happy Sunday and most importantly, have a very happy Mother’s Day!