Sokoine University of Agriculture (SUA): Hamtambui umuhimu wenu katika Taifa hili au mmeridhika na kuwa under-utilized?

Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
695
935
Hakuna shaka nchi yetu inategemea sana kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wetu. Asilimia zaidi ya 75% ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo, sasa ni kwanini taasisi hii muhimu inazidiwa na vyuo vinavyofundisha Science ya Siasa au Ubunifu wa Majengo na Ukandarasi wakati katika miradi yote mikubwa nchini ni asilimia 25% tu inafanywa na Watanzania? (wrong priorities?).

Kwanini SUA msiwe the leading high learning Institute katika nchi hii? Kilimo bado ni duni sana na sidhani kama hii ni bahati mbaya (coincidence). Mnafeli wapi?! Kwanini hatuoni positive impacts ya kutosha as a Nation? (ningefurahi Viongozi wa SUA wangekuwa wa kwanza kujibu haya). Naomba wadau au mnaojua zaidi mdadavue dukuduku hili, na ninashauri walengwa wachukue dondoo za mawazo ya kujenga yatakayoletwa hapa.

Serikali/ Wizara na Taasisi zetu zinahitaji sana mawazo yenu wananchi ili tusonge mbele, hii nchi ni yetu sote. Naomba msitukane, toeni maoni kwa staha.
 
Kabulala, Kusoma kilimo kunaitaji upende kazi husika, lakini waliosoma kilimo wanataka wakae town, umasikini kitu kibaya sana, hata mawazo yetu watanzania ni ya kimasikini sana, Mfano mdogo maeneo ya kilimo yamejengwa makazi ya watu na maeneo yasiyo na rutuba watu wengi wameyakimbia yamekuwa mapori. Na kingine bajeti itokayo ni kichekesho sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ya taasisi ya Elimu km SUA ni kuzalisha wataalamu wengi wenye weredi wa kutosha. SUA kwa kiasi kikubwa na kwa uwezo walio nao wameweza hilo kwa kipindi kirefu. Nazani SUA inaongoza kwa kuzalisha Maprofesa na PHD holders magwiji nyuma ya UDSM. Wamejitahidi sn.

Shida ni namna serikali ilivyojipanga kuwatumia wasomi hawa. Hakuna sera rasmi na ya kudumu kuhusu maendeleo ya kilimo. Kila Rais akiingia madarakani anakuja na sera yake itakayo mnufaisha kisiasa. Sera zinatungwa bila kuwahusisha wataalamu wa kilimo. Kilimo kimetekwa na wanasiasa. Angalia kwenye siasa zinavyopigwa kwnye korosho.Nenda kwenye Kahawa na Chai. Hv unaanzaje kukilaumu chuo cha SUA. Hv ni nani angeweza kumshauri Magufuli na akasikilizwa kuhusu madhara ya serikali kujiingiza kwenye biashara ya korosho?

Sekta ya kilimo licha ya kuwaajiri watu wengi lakin ndio sekta yenye uwekezaji mdogo sn na unaosuasua. Ukienda SUA kuna mambo mengi sn ambayo chuo kimefanya ikiwemo na ugunduzi wa mbegu bora mbali mbali za mazao ya mahindi,mpunga,maharage, kahawa,chai n.k. Ishu hapa ni je serikali inatumia vp hizi tafti na kuzifikisha kwa wananchi?

Nimesoma SUA na najua mazingira magumu wanayopitia wakufunzi wa chuo. Pamoja na changamoto hizo za miundo mbinu na zinginezo SUA kimebaki kua chuo bora Tanzania na Afrika mashariki. Nazani kabla ya kulaumu ni vema kutafakari kwa kina ili kujua tatizo liko wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamgomoli,
Vizuri Sana, kwahiyo unasema tatizo sio Chuo tatizo ni serikali!?..pia nimeona umegusia kuhusu wataalamu wengi na watu wa kumshauri Rais..hivi unawezaje kuwa Mbobezi wa fani Fulani especially Kilimo katika level ya prof..unatoa ushauri mara moja Hadi sita na ushauri wako haufatwi na wewe kila siku unawaaga mkeo na wanao eti waenda kazini!?

Lawama zangu ziko hapo, people should stand up and be counted hata Rais anapenda watu wanaomshauri Kwa kuwa na facts za kutosha na kuzitetea Kwa udhubuti na sio Kwa uoga au unafiki? Na je ni lazima wahitimu wote watumiwe na serikali!?...Chuo kimefanya nini kuhakikisha wahitimu wanaleta impacts bila kusubiri mkono wa serikali..are they creative and self-reliant?..au ndo wahitimu anaowasema DC Mtatiro?
 
Kabulala,
Kabulala, bandiko lako ni muhimu sana.
Yapo mambo kadhaa ya kujiuliza.
1. Elimu inayotolewa SUA, iko sawasawa?
>>Jibu lake ni chanya. Elimu iko sawa. Kwa hiyo suala hapa siyo SUA kama Taasisi, bali mimi hujiuluza siku zote kwa nini 'impact' ya Wahitimu, tena hususan Wahitimu wa KILIMO wa SUA hatuioni nchini mwetu?
Kwa nini KILIMO kilichokuwa kinalimwa Vijijini wakati tunapata Uhuru bado ni hicho hicho mwaka 2020?

2. Wahitimu wa Udaktari tunawaona, na 'impact' yao inaonekana. Wahitimu wa Uhandisi tunawaona, na 'impact' yao inaonekana. Hata Wahitimu wa Udaktari wa Mifugo (toka SUA), tunawaona.
>>Wote hawa wana kitu kimoja kinachowafanya waonekane. Nacho ni MKONO WA SERIKALI. Madaktari tunawaona katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati za Serikali.
Wahandisi tunawaona katika Miradi ya Barabara ya TANROADS na TARURA.
Hivyo hivyo Wataalam wa Mifugo. Bila Mkono wa Serikali, hakuna Taaluma ambayo ingekuwa inaonekana katika jamii yetu.

3. SWALI MUAFAKA hapa ni kuwa NI NINI KIFANYIKE ILI WAHITIMU WETU WA SUA WATOE MCHANGO STAHIKI KATIKA KUJENGA NA KUBORESHA MAISHA YETU HAPA TANZANIA.
Kabulala, umeeleza kuwa Kilimo kinahusisha asimilia 75 ya Watanzania.
Mimi nasema Kilimo kinahusisha asilimia 95 ya Watanzania wanaofanya kazi, bila kuhesabu wazururaji.
Kazi za maofisini na viwandani kwa pamoja zinaajiri asilimia 5 tu ya Watanzania
 
fundimchundo,
Good observation fundimchundo...vipi hao wakufunzi wa SUA hawana mbinu mbadala za kuwapika wahitimu ili wasitegemee mkono wa serikali!?.. Common sense inaonesha msomi anakuwa Yuko equipped kupenyeza maarifa yake kulingana na mazingira..vipi hawa wetu mbinu zimeishia kwenye Theories tuu( najaribu kufikiria Kwa uwazi..sina Nia ya kutilia mashaka weledi wa watu kwani hizo elimu walizonazo sijazifikia robo..nahoji tuu)
 
Vizuri Sana.. kwahiyo unasema tatizo sio Chuo tatizo ni serikali!?..pia nimeona umegusia kuhusu wataalamu wengi na watu wa kumshauri Rais..hivi unawezaje kuwa Mbobezi wa fani Fulani especially Kilimo katika level ya prof..unatoa ushauri mara moja Hadi sita na ushauri wako haufatwi na wewe kila siku unawaaga mkeo na wanao eti waenda kazini!?...lawama zangu ziko hapo.. people should stand up and be counted..ata Rais anapenda watu wanaomshauri Kwa kuwa na facts za kutosha na kuzitetea Kwa udhubuti na sio Kwa uoga au unafiki?...na je ni lazima wahitimu wote watumiwe na serikali!?...Chuo kimefanya nini kuhakikisha wahitimu wanaleta impacts bila kusubiri mkono wa serikali..are they creative and self-reliant?..au ndo wahitimu anaowasema DC Mtatiro?!
SUA imefanyakazi kubwa sana lakini tatizo lililopo ni kuwa wananchi wachacha sana wako katika kilimo cha kisasa. Pia skimu za umwagiliaji nyingi ziliharibika, zinahitajika fedha za kufufua skimu hizo. Pia masharti ya kupata mikopo kwa ajili ya kiimo bado si rafiki kwa mkulima wa kawaida. Miaka ya nyuma kulikuwa na mashamba ya ngano mkoa wa Arusha, Manyara. Je, kwa sasa bado hayo mashamba yapo? Yalikufa kwa namna gani? SUA pia wameinua ufugaji wa kisasa kwa mikoa ya Ruvuma, Morogoro, Iringa na Njombe. Tusikilaumu Chuo ila pia wanachanchi hawapendi kutafuta ushauri wa kitaalum kwa ajli ya kilimo cha tija!
 
Wizara ya Kilimo Tafadhali chukueni notice...mnapewa ushauri mzuri kuliko hata kipindi mko Bungeni...listen from the real stakeholders/grassroots.
 
Kabulala, Kusoma kilimo kunaitaji upende kazi husika, lakini waliosoma kilimo wanataka wakae town, umasikini kitu kibaya sana, hata mawazo yetu watanzania ni ya kimasikini sana, Mfano mdogo maeneo ya kilimo yamejengwa makazi ya watu na maeneo yasiyo na rutuba watu wengi wameyakimbia yamekuwa mapori. Na kingine bajeti itokayo ni kichekesho sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
Wilaya nzima ya kyela ni eneo LA kilimo lakini makazi ya watu ndio yanazidi kushamiri.
 
SUA kuna shida kubwa sana amna ata makongamano wanayoyandaa kwa ajili ya wananchi wakulima wa chini ili wawafundishe jinsi ya kuboresha kilimo. Sijui mkulima ili apate kujifunza mbinu za kulima kisasa inabidi asafiri adi Morogoro na uoneshe vyeti vyako vya NECTA.
 
Sua wana eneo kubwa tu kama chuo na sehemu kubwa wanaishi nyoka tu wa wakabaji nyakati zajioni hasa eneo lao la mazimbu,,wameubana mji sana na eneo lao lakini hatuoni IMPACT ya chuo hiki katika mapinduzi ya kilimo,,bora eneo lao lipunguzwe tu wapewe wananchi,,,maeneo yao hayaendelezwi kwa chochote zaidi ya wananchi kukodishwa nyakati za kilimo,,yaan kilimo nchini kipo hoi,,bado wanachi wanalima kijima na waralamu wanahitimu kwa mamia sua kila mwaka
Kazi ya taasisi ya Elimu km SUA ni kuzalisha wataalamu wengi wenye weredi wa kutosha. SUA kwa kiasi kikubwa na kwa uwezo walio nao wameweza hilo kwa kipindi kirefu. Nazani SUA inaongoza kwa kuzalisha Maprofesa na PHD holders magwiji nyuma ya UDSM. Wamejitahidi sn.

Shida ni namna serikali ilivyojipanga kuwatumia wasomi hawa. Hakuna sera rasmi na ya kudumu kuhusu maendeleo ya kilimo. Kila Rais akiingia madarakani anakuja na sera yake itakayo mnufaisha kisiasa. Sera zinatungwa bila kuwahusisha wataalamu wa kilimo. Kilimo kimetekwa na wanasiasa. Angalia kwenye siasa zinavyopigwa kwnye korosho.Nenda kwenye Kahawa na Chai. Hv unaanzaje kukilaumu chuo cha SUA. Hv ni nani angeweza kumshauri Magufuli na akasikilizwa kuhusu madhara ya serikali kujiingiza kwenye biashara ya korosho?

Sekta ya kilimo licha ya kuwaajiri watu wengi lakin ndio sekta yenye uwekezaji mdogo sn na unaosuasua. Ukienda SUA kuna mambo mengi sn ambayo chuo kimefanya ikiwemo na ugunduzi wa mbegu bora mbali mbali za mazao ya mahindi,mpunga,maharage, kahawa,chai n.k. Ishu hapa ni je serikali inatumia vp hizi tafti na kuzifikisha kwa wananchi?

Nimesoma SUA na najua mazingira magumu wanayopitia wakufunzi wa chuo. Pamoja na changamoto hizo za miundo mbinu na zinginezo SUA kimebaki kua chuo bora Tanzania na Afrika mashariki. Nazani kabla ya kulaumu ni vema kutafakari kwa kina ili kujua tatizo liko wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna tatizo mahali...huku JF serikali inashauriwa vizuri tu,sema wanatu ignore na ushauri unabaki kwenye makabati ya JF! sad

Kilimo

Mapinduzi yawe ni ya kilimo....

Kilimo as solution to unemployment

Tatizo la Ajira

Kilimo: Tuwe wabunifu zaidi tunapojihusisha na kilimo
Unasema kweli. Tungejitahidi kwenye kilimo kama nchi tungeondokana na utegemezi mwingi. Kilimo kinaongeza export business ya nchi na tena ni business yenye uhakika kwani watu hawawezi kuacha kula. Kilimo kinafanya nchi iwe na maisha rahisi na mazuri. Kilimo, kwangu mimi ndiyo njia inayohitaji teknolojia rahisi na isiyohitaji utaalam mkubwa. Tanzania tuna ardhi nzuri, tuna maji mengi na hali ya hewa nzuri sana, hakuna sababu yoyote ni kwa nini tunashindwa. Tena sasa hivi tukiwekeza kwenye mazao ya organic (yanalimwa bila kutumia kemikali) tutapata soko kubwa kwani watu wengi hawataki tena vyakula vyenye kemikali.
 
Back
Top Bottom