Uchaguzi 2020 Sokoine, Mbeya: Magufuli asema Tulia amemsumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya, amuomba Joseph "Sugu" Mbilinyi kura

Nimemsikiliza Tulia mwanzo mpaka mwisho, kama ndio sera zake ni hizi za kumsifu Magufuli kafanya makubwa Mbeya mjini then utegemee kumtenga mbunge Sugu na hayo mazuri anayoyahubiri badi PhD ya Tulia ina walakini mkubwa.

Nilikuwa sijui vizuri uwezo wa Tulia jukwaani kama mkutano huu mkubwa ndio yupo shallow hivi basi nashauri Sugu atumike kwenye majimbo mengine ya Mbeya kuongeza nguvu kwa sababu natamka rasmi Tulia atapigwa kwa kura nyingi zaidi ya alizoshinda Sugu mwaka 2015.

Mbeya mjini shughuli imekwisha, beti popote pale kwa dau lolote.
Huyu Tulia walau hata angekuwa na mvuto aisee...

Ningeweza mpa kura ya kumtamani.
 
Amekiri kuwa yeye hakuwaacha wana Mbeya lakini sasa iwe basi kwani amemleta mtoto msomi ambaye yupo vizuri hili kuleta maendeleo kwa kasi ya ajabu hili kila Masafwa na Mnyakyusa ashangae mwenyewe lakini yule mtu mwenye sugu mwili mzima apigwa srabu mwili mzima awe mlaini kabisa na Mbeya iwe katika mstari.

Huku akishangiliwa na maelfu ya watu waliojitokeza amesema sasa basi, imetosha, atarudi tena kwa ajili ya kuja kuweka msisitizo na kuwahasa wanambeya kuondoa tofauti zao zote na kumpa Tulia hii inamaana hata punda akifa mzigo unaweza kufaulishwa kufika ni lazima.
Taarifa zinasema kuwa CCM inaona ni bora ipoteze majimbo mengine yote ya Mbeya lakini jimbo la Mbeya mjini hapana. CCM chama kikubwa na tajiri kifedha kimesema kitatia nguvu ikibidi kama zote hili Sugu akaendelee na kutengeneza singo zake na si kurudi Dodoma tena.
 
Sugu ni mkoloni sio mzawa wa Mkoa wa Mbeya ni.mhamiaji mkoloni aliyekuja kutawala wenyeji wa mkoa wa Mbeya

Mkoloni Sugu lazima afungashwe virago aachie wenyeji wazawa wa mkoa wa Mbeya
 
Leo Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni katika mkoa wa Mbeya na mkutano huu utarushwa mubashara kupitia TBC, Channel ten, Star tv, ITV na mitandao mbalimbali.
Karibu.

Updates;
Uwanja umefurika wananchi wa itikadi mbalimbali na bendera zao hakika siasa siyo Uadui.

Viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.

=========

MAGUFULI: Mwaka 2015 tulipita hapa kuwaomba kura wana-Mbeya, mlitusikiliza na natambua nilipata kura nyingi sana Mbeya lakini kwa mbunge aliyekuwa wa CCM mkasema hapana, mkanichagulia pia baadhi ya madiwani lakini mkanichagulia wabunge katika maeneo ya Mbeya, Mkanichagulia Kyela, Chunya na maeneo mengine.

Hapa mjini mkasema hapana, niseme kwa dhati, nilisikitika lakini sikiuwachukia na nikaja nikaambiwa kwamba, kushindwa kwa CCM katika jiji hili la Mbeya ilitokana na ugomvi wa wana-CCM wenyewe.

Nilichofanya ndugu zangu na nataka niwaeleze hapa leo, kutaka kuhakikisha kwamba Mbeya haipotei kwenye ramani, nilimtafuta mwanamama mmoja msomi aliyekuwa akiitwa Dr. Tulia nikamteua kuwa mbunge kwamba yale yatakayokuwa kuwa yanajitokeza kwa ajili ya Mbeya angalau yawe na msemaji.

Nilipomteua Dr. Tulia kuwa mbunge na ndiye mbunge mmoja wa kwanza niliyemteua, alipoingia bungeni akateuliwa pia kwa nyota aliyokuwa nayo, akateuliwa kuwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Amefanya kazi zote zilizotakiwa kufanywa na mbunge wa Mbeya, napenda leo kwa hadhara hii Tulia nikushukuru sana kwa sababu ulinisumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya na kwa sababu leo umekuja mwenyewe na kwa vile sitakuteua tena kwa viti maalum, nimekuleta kwa wazazi wako, dada zako, kaka zako, wazee wako wakusulubu wewe kwa ajili ya kazi zako nzuri.

Nina matumaini makubwa kwa hadhara hii, tofauti zilizopo miongoni mwa wana-Mbeya mtaniletea Dr. Tulia Ackson awe mbunge wa hapa.

Ninayasema haya kwa sababu pamonja na kwamba hakutuchagua hapa Mbeya mjini tuliendelea kufanya kazi kwa manufaa ya wana-Mbeya wote kwa sababu ninafahamu maendeleo hayana chama.
Kwa hiyo wana Mbeya miaka 5 maendeleo aliyowaletea ni Tulia ......... Kazi kweli kweli!!
 
magufuli mitano tena
tapatalk_1601418168188.jpeg
 
Muulizeni kwa nini aliogopa kuja huko mpaka zile bendera za CDM zilipoondolewa?
 
Debate fanyeni na akina Shibuda.

Dr Magufuli kazi zake zinaonekana bwashee!
Kazi zake zimekugusa vipi moja kwa moja kama mwananch wa kawaida?? Maana wakulima wanalia, wafanyakazi, na wafanyabiashara kote mazingira ya utendaji wao yamevurugwa makundi haya yote lazima wamchinje... Waliobaki na nafuu ni wale anaozunguka nao kwenye magari pamoja na wapiga debe wake kama wewe...
 
Kwani Diamond na Ali kiba si washaimba sasa mbona watu bado wapo wanamsikiliza Magufuli au watakuja kuimba tena?
 
Nimefurahishwa sana Chunya mmeniletea mtoto wa Njeru Kasaka,Baba yake alikuwa Rafiki yangu sana wakati mi ni waziri......

Nchi bila connection kutoboa ngumu
 
Back
Top Bottom