Uchaguzi 2020 Sokoine, Mbeya: Magufuli asema Tulia amemsumbua sana kwa ajili ya maendeleo ya Mbeya, amuomba Joseph "Sugu" Mbilinyi kura

Cheza na kila sehemu lakini achana na Mbeya. Mbeya wameikataa CCM, Mbeya wamemkataa TULIA. Kila utakachokifanya ujue wao wana msimamo wao, watakuheshimu kama Rais kakini utashanga maamuzi yao. Mbeya watamchagua Sugu ndiye Rais wao na Mbunge wao. Mbeya watapiga kura na kuzilinda na wala msithubutu KUZIIBA. Damu itamwagika yaweza kuwa ya Polisi, Mkurugenzi wa Uchaguzi au mwananchi Lakini mwaka huu DHULUMA haina nafasi kwa Mbeya.
Vipi upo Mbeya au? Tusijekuta kumbe tuna chat na mbumbumbu yuko Ulaya anabeba mabox.
 
Wekeni MOTION
Opposers na Propposers.

Napendekeza iwe
Samia ni bora kuliko Mwalimu.
Halafu Lisu awe Propposer na JPM awe Opposer
We can adopt the US-style ie contestants addressing specific topics that touch peoples needs, not that topic you have proposed which simple-minded people would discuss
 
Mida hii ya saa mbili asubuhi wanafunzi wanatafuta nini uwanjani badala yakuwa darasa
Kwani hujui wanafunzi ni wakigakura wa miaka ijayo? CCM itaendelea kutawala miaka mingi ijayo kama akili zenu ni za kisaccos saccos! Wanafunzi hawawezi kuja kwenye mikutano yenu kwa kuwa mikutano ni vujo vujo tuuu wavuta bhangi kibao.
 
Tulia Ackson anamwaga sifa ya mambo mazuri yaliyofanyika Mbeya mjini.

Sasa najiuliza hapa unamtengaje Sugu na mafanikio ndani ya jimbo lake?

Tulia anamfanyia kampeni Sugu huku akidhani anampamba Magufuli peke yake.

Aliyewaroga ccm kafa, hawajielewi hawa watu.
 
IMG_7320.jpg

tumeambiwa twende wanafunzi wote na nguo za nyumbani
 
We can adopt the US-style ie contestants addressing specific topics that touch peoples needs, not that topic you have proposed which simple-minded people would discuss
Simple minded people ndio tunadhana maneno mengi ya mtu ndio utendaji, kama ni hivyo basi Kasuku anaweza kuwa kiongozi.

Kama ni issue ya kueleza topic fulani hizo ni Sera za kila mgombea na chama chake ambazo kila mkutano mtu anazinadi.
 
Nimemsikiliza Tulia mwanzo mpaka mwisho, kama ndio sera zake ni hizi za kumsifu Magufuli kafanya makubwa Mbeya mjini then utegemee kumtenga mbunge Sugu na hayo mazuri anayoyahubiri badi PhD ya Tulia ina walakini mkubwa.

Nilikuwa sijui vizuri uwezo wa Tulia jukwaani kama mkutano huu mkubwa ndio yupo shallow hivi basi nashauri Sugu atumike kwenye majimbo mengine ya Mbeya kuongeza nguvu kwa sababu natamka rasmi Tulia atapigwa kwa kura nyingi zaidi ya alizoshinda Sugu mwaka 2015.

Mbeya mjini shughuli imekwisha, beti popote pale kwa dau lolote.
 
Naona kama vile JPM leo hayuko sawa. Nahisi kajichanganya kwa kuanza kuangalia press conference ya Tundu Lisu huko Arusha. He seems to be in very deep thinking! Sijui Kama atamudu kufanya kampeni ilivyo kusudiwa.
 
Labda nikulize ni nani asietaka kumuona daimond? Kipimo sahihi cha kujaza watu kingefanyika kama wasanii wasingetumika
Hicho nacho ni kipimo kizuri cha uelewa wa watanzania kwamba pamoja na yote anayoyaeleza Lissu kuhusu serikali ya ccm ila bado watanzania ndio kwanza wanaenda kujazana kwenye mikutano ya ccm kwa ushamba wa kumuangalia Diamond.

Binafsi nilitegemea watanzania wakati huu ndio watawaonesha ccm kuwa tumewachoka kwa kutokuja kwenye mikutano yenu hata mkileta hao wasanii,kwa anaejielewa hawezi kwenda kupumuliana pale et ili amuangalie Diamond na Kiba halafu kibaya zaidi walioandaa ni ccm.

Hao watu wangekuwa na hasira kweli na ccm wasingekanyaga hapo kisa wasanii.
 
Back
Top Bottom