Sokoine bado hajazingatiwa ipasavyo na viongozi wa sasa

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Katika kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati EDWARD MORINGE SOKOINE, imeelezwa kuwa mengi aliyoyasimamia na kuyaamini kwa maslahi ya Wananchi, hayapewi uzito kama ilivyokuwa wakati wa uhai wake.

Kauli hiyo imetolewa na Mwandishi Nguli na Mkongwe wa Vitabu nchini, na Mhadhiri wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania, Prof EMMANUEL MBOGO wakati akitolea ufafanuzi juu ya namna alivyopata wazo la kuandika tamthilia ya Morani, kupitia maisha ya Hayati SOKOINE wakati wa uhai wake.

Prof MBOGO amesema akiwa tayari amekusanya taarifa mbalimbali kwaajili ya kuanza kuandika kitabu hicho, alifanya safari kurudi chuoni huko nchini Ujerumani wakati huo Marehemu SOKOINE akiwa bado yuko hai.

” Nilipofika Ujerumani katika Chuo nilichokuwa nasoma walikuja wanafunzi wenzangu, wakaniambia walikuwa wanataka kujua mengi kuhusu Tanzania, lakini wakaniambia kuwa walikuwa na Mkutano kuhusu kifo cha SOKOINE, nikashituka kwasababu nilimwacha akiwa hai” Anasimulia Prof MBOGO.

Kisha Prof EMMANUEL MBOGO ameongeza kuwa wengi wakisoma kitabu cha Morani ambacho muhusika wake mkuu ni Dongo, wanahisi kuwa yule ni SOKOINE la hasha ila nilitumia maisha yake kuandaa hicho kitabu.

Mwandishi huyo Nguli wa Vitabu nchini amesema kwa sasa mambo mengi aliyosimamia kiongozi huyo hayapewi uzito ipasavyo, kama ilivyokuwa wakati wa uhai wake jambo ambalo anashauri lipewe uzito ikiwemo kuandaa Makongamano kuhusu maisha ya Kiongozi huyo.

EDWARD MORINGE SOKOINE alipata kuwa Waziri Serikali ya awamu ya kwanza katika vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, mwaka 1984 kwa ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa, Wilayani Mvomero, huko Mkoani Morogoro.
 
Kama Tanzania ilipoteza KIONGOZI basi mwaka 1984 tulimpoteza real KIONGOZI,waliobaki wote ni wachumia matumbo,wanaoona MADARAKA ni bora kuliko RAIA,wanaoua na kutesa kwa sababu ya kulewa madaraka.

In short hatuna viongozi Tanzania
 
Sitaki unafiki japo kwa vijana wa leo huenda wasiyajue haya kwani hapa tanzania hajatokea waziri mkuu jembe kama hayati sokoine ni waziri pekee ambaye alishindwa kukubaliana na baadhi ya mambo ya rais nyerere hasa kwenye oprasheni uhujumu uchumi ambapo aliamua kuondoka na kurudi kijijini kuchunga ng 'ombe hadi hapo mwalimu alipotuma ujumbe kwenda monduli kumshawishi arejee ikulu labda nafasi hii agepewa rais wa sasa nafikiri rekodi ya sokoine angeifikia na kidogo mnyonge mnyongeni kwa karibu ambaye alitaka kuifikia japo hakuwa waziri mkuu ni bwana Lyayonga mrema!
 
Lowasa hakuhudhuria jana.
Si Kuwaasa tu ni Chadema nzima hawapo, si Mbuge wala madiwani. Unakumbuka binti yake Sokoine alipelekwa ujumbe ajitoe CCM agombee kwa Chadema akakataa ndio maana falia ya Sokoine imetengwa? Zingatia pia Sokoine ni Katoliki huku Lowassa alisema Tabora Chadema inataka Mluteri?
 
Sokoine alikuwa ni kiongozi shupavu na hakuna wa kumlinganisha naye, nakumbuka kabla ya kupanda gari kwenda dodoma na wakati anarudi ndipo alipo Pata ajali yenye utata, alimwambia rashidi kawawa rudisha pesa za wananchi au nenda radio Tanzania ukawaambie watanzania hizo pesa umepeleka wapi? Na alimpa siku 7.
 
Sokoine alikuwa ni kiongozi shupavu na hakuna wa kumlinganisha naye, nakumbuka kabla ya kupanda gari kwenda dodoma na wakati anarudi ndipo alipo Pata ajali yenye utata, alimwambia rashidi kawawa rudisha pesa za wananchi au nenda radio Tanzania ukawaambie watanzania hizo pesa umepeleka wapi? Na alimpa siku 7.
Evidence?
 
Back
Top Bottom