Soko la SIDO (Mwanjelwa - MBEYA) linateketea kwa moto sasa hivi

umelipuka moto mkubwa kwenye maduka yaliyoko kabwe mbeya,ni tafrani tupu watu wanakimbia hovyo........fire hawajafika hadi saa hii,chanzo na maelezo mengine baadae ngoja nijisalimishe kwanza
 
Poleni mliopo huko. Nimeisikia hii habari sasa hivi redioni, Ebony fm ya Iringa.
 
Wadau, nimepata taarifa toka Mbeya kwamba soko jipya la Mwanjelwa linaungua moto hivi sasa....aliye karibu na eneo la tukio atujuze tafadhali...
 
hapa nipo eneo la tukio moto unawaka na watu bila kujali hatari iliyopo wanaiba bidhaa
 
pAKILIPUKA NDO YALEYALE YA KENYA NA BOMBA LA WESE!! MIAFRIKA SIJUI TUKOJE
 
fire wamefika na moto nao unaenea kwa kasi,watu nao wamekuwa wengi mno,wezi nao kazini....ni hatari
 
kufa kufaaana hapa,vibaka wako busy na mafurushi wanakimbia hovyo,boda boda naona kazini...
 
Duuuuhh!! Kweli zimwi la ajali limetuandama wajameni tukazane tusali mungu atuepushe na haya majanga mana sasa naona yanapishana mara moto mara maji mara ajali na vp ile sea bus iliyokwama jana kwenye visiwa vya nungwi mpaka masaa matatuuu iltoka kweli??
 
Mmmmmmmmh,..................tena MBEYA soko lingine lina ungua hapa si patupu why Mbeya kilasiku? nina wasiwasi hata lile soko jipya linalo jengwa mwanjelwa litaungua tu kwa mtindo kama huu....
 
Sina kumbukumbu vizuri lakini hili litakuwa ni tukio la pili bila shaka.
 
kuna godown karibu na airport moto umeshika kasi,niko upande wa airport na sijaona reaction ya hawa jamaa wa uwanja wa ndege
 
Du poleni sana wana~Mbeya... ila nako kumezidi Mwanjelwa 2006,Soko la Uhindini 2010,Soko la Sido 2011... Jamani...
 
Back
Top Bottom