Soko la SIDO (Mwanjelwa - MBEYA) linateketea kwa moto sasa hivi

Soko la sido jijini mbeya linaungua moto sasa hv, fire bado wanahangaika kuzima, chanzo hakijajulikana, nitawajuza zaidi
 
Fire mbona sio wa kuwategemea linapotokea janga kubwa kama la maduka kuungua. Watakuwa busy na kuChukua Chao Mapema na kusingizia maji yameisha.
 
Yasemekana Soko la Sido Mbeya lawaka moto, watu waliokaribu fanyenyi uchunguzi mtujuze chanzo nini, na athari yake!
 
Sina kumbukumbu vizuri lakini hili litakuwa ni tukio la pili bila shaka.
<br />
<br />
litakuwa la tatu kubwa,ilinza soko la mwanjelwa,ikafuatia soko la uhindindi mwishoni mwa mwaka jana,na hili la leo....bado moto mkubwa
 
Du poleni sana wana~Mbeya... ila nako kumezidi Mwanjelwa 2006,Soko la Uhindini 2010,Soko la Sido 2011... Jamani...

Mkuu hii ni mara ya 15 masoko yanaungua mbeya katika kipindi cha miaka kama 10 hivi, soko la mwanjelwa hii ni mara ya tatu linaungua, soko kuu uhindini limewahi kuungua zaidi ya mara 4, soko matola limewahi kuungua zaidi ya mara 2, wakati soko la mbalizi limewahi kuungua mara 2 ndani ya mwezi mmoja miaka ya mwanzoni mwa 2000, kuna soko la ipinda pia liliwahi kuungua.

Mbaya zaidi matukio yote haya inasemekana yanasababishwa na hitilafu za umeme. Mimi nina mashaka sana na sababu kama hizi, naomba mamlaka husika zifanye uchunguzi wa kina juu ya sababu ya masoko ya mbeya kuungua moto.

Kwa taarifa yenu wana JF, hili soko la sido linaloungua hizi sasa ni soko lililoanzishwa mwaka juzi baada ya soko la mwanjelwa kuungua na hivyo manispaa kuamua kulijenga upya. Kwa hivyo kwa sasa hapa mbeya masoko makubwa mawili yamefungwa na yako kwenye matengenezo makubwa baada ya kuungua kwa moto.

Nawaonea huruma wafanyabiashara ambao kila mwaka wanapata hasara. Uwezi amini kinachotokea hapa sokoni sasa hivi....
 
  • Thanks
Reactions: SG8
What a coincidence! Wanajamvi, Usiku wa kuamkia leo nimeota, jamaa aliyekopa fedha kwangu, ameamua kuhamisha bidhaa za thaman (dhamana) zilizokuwa kibandani kwake na kuamua kukilipua.

Niliposhtuka nikasema leo lazima nianze kufuatilia suala la bima kwenye mikopo ninayotoa. Jamani Bima is for real. Ndugu zangu tukatie bima biashara zetu, la si hivyo tutapoteza hata kile kidogo tulichokuwa nacho. Na hii ni kwa wajasiriamali wote (wakopaji na wakopeshaji).

Poleni, ndugu zangu mliopoteza mkate wenu wa kila siku
 
Wana JF hivi sasa nipo soko kuu la mwanjelwa mbeya ambalo miaka 3 iliyopita liliwaka moto
hivi sasa linawaka moto tena, hivi nitaendelea kuwaleteeeni habari zaidi

SAM_0564.JPG
 
habari nilizo zipata hivi sasa ni kwamba soko la sido lililopo mkoani mbeya mjini linawaka moto, yaani linaungua, nitawajulisha baadae habari zaidi
 
WAna janvi taarifa nilioyoipata hivi punde kutoka mkoani mbeya inasema kuwa soko la SIDO ambalo ndilo soko kubwa zaidi na linalotegemewa na wakaazi wa jiji hilo limeteketea kwa moto leo tangu saa moja lililopita.
Bado sijapata hasara kamili na athari zilizotokea, ila bado linaendelea kuwaka moto huo. Soko hilo ndilo kubwa linalotumika baada ya lile la awali kuteketea mnamo mwaka 2006 December.
TAfadhali mlioko jirani mtujuze zaidi
 
Sina kumbukumbu vizuri lakini hili litakuwa ni tukio la pili bila shaka.
Umekosea mzeee, ni mara ya tatu "kama sikosei" Lilianza kuungua soko la Mwanjerwa (ambalo sasa linajengwa upya), likafuata la uhindini (Ssasa limefungwa) , leo la SIDO!
 
Sina kumbukumbu vizuri lakini hili litakuwa ni tukio la pili bila shaka.
Mara ya tatu, ilianza ya Mwanjelwa iliyoondoka na Akukweti, ikafuatia ya Uhindini 2010 na sasa hii ya Sido Mwanjelwa
 
Tanzania hatupumui,bado tunauguza maumivu ya ajari ya meli,soko tena polen wanambeya na Tanzanian wote.
 
Back
Top Bottom