Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,319
- 33,125
Picha inaonyesha jinsi gani moto ulivyoharibu miundo mbinu ya soko Thursday, March 04, 2010 2:58 PM
Soko la kukaangia samaki la Feri lililopo katika kivuko cha Kigamboni limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo. Soko la kukaangia samaki la Feri lililopo katika kivuko cha Kigamboni limeteketea usiku wa kuamkia leo , akizungumza shuhuda mmoja aliyekuwepo katika tukio hilo aliye jitaja kwa jina la Jafari Juma alisema kuwa soko hilo liliungua majira ya saa 4 usiku wakati wakaanga samaki wengi walikuwa tayari wameondoka.
Mmoja wa wakaanga samaki alikuwa anawahi kuondoka ndipo alipo chukua mafuta yaliyokuwa na uchafu wa samaki ambao tayari walikuwa wamekaangwa akarushia kwenye jiko ndipo mlipuko ukatokea mripuko huo umesababisha hasara ya Majiko 48 kuungua.
Kutokana na moto huo kuunguza soko hilo vibaka na baadhi ya wavuvi wameiba vitu mbalimbali vikiwemo vyuma chakavu vilivyo salia katika janga hilo.