Soko la Sabasaba mkoani Dodoma lipo bila Uongozi kwa miezi nane sasa

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,182
1,490
SOKO LA SABASABA KWENYE MKWAMO WA UONGOZI KWA MIEZI 8 SASA*

Na
Peter J Mallya

Soko kuu la Sabasaba Jijini Dodoma ni miezi 8 sasa limekuwa halina uongozi kutokana na uongozi wa mwanzo kuvunjwa kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali za soko hili. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi alivunja uongozi wa soko hilo mwezi wa 9 mwaka 2018 na kuteuwa viongozi wa muda ambao wangewaongoza wafanyabiashara kwa siku 21 kupata uongozi wa kudumu wa soko hilo.

Kwa sasa ni miezi saba (7) uongozi wa muda umeendelea kukaimu bila kupata uongozi wa kudumu wa soko,wafanya biashara wa soko hilo wamekuwa kwenye sintofahamu kutokuwa na uongozi wa kudumu wa soko hapo.

"Ndugu mwandishi hapa kuna makundi,yaani hapa mkurugenzi anataka kuweka uongozi wake,mtendaji anataka kuweka uongozi wake na CCM wanataka kuweka uongozi wao ndiyo maana uchaguzi haufanyiki humu labda waziri mkuu aingilie kati kuvunja haya makundi ili tufanye biashara zetu kwa amani." amesema Shaban Muhsini mfanyabiashara sokoni hapo.

Mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa kina la James Samson alisema tatizo la soko hili ni Baraza la wadhamini kuingilia uongozi wa mpito matokeo yake uchaguzi umeshindwa kufanyika mpaka sasa,nikupe tu mfano "wadhamini wanakuja wanasema wanataka uchaguzi ufanyike kwa wagombea wote hata wale waliowekewa mapingamizi jambo ambalo sio sahihi,inakuwaje watu hao walis jusimamishwa kwa tuhuma za ubadhilifu wakati bado wapo kwenye uchunguzi wachukuwe fomu wagombee tena!?" aliuliza mfanyabiashara huyo.

Alipotafutwa mkurugenzi wa jiji kuzungumzia mkwamo huo wa uongozi hakupatikana mpaka tunakwenda mitamboni.

IMG-20190311-WA0001.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom