Soko la Mayai (bei ya jumla) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soko la Mayai (bei ya jumla)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kanyagio, Dec 7, 2011.

 1. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wanandugu kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana kubadilishana mawazo kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai, hatimaye kumekucha.. Mimi nafuga kuku 1000, kati ya hayo 580 ambao ni awamu ya kwanza wanaanza kutaga. awamu ya pili wanaanza kutaga Januari. nina soko la mayai katika duka moja. ila ningependa kupata soko jingine pia.

  uzalishaji unategemea kuwa kama tray kama 10 kwa siku au 70 kwa wiki. production itaongezeka kadri ziku zinavyoenda na pia wale wa awamu ya pili wakianza kutaga.

  kama kuna mtu ahahitaji mayai au anaweza kunipa mawazo wapi naweza kuyauza haya mayai kwa ujumla tupeane ushauri.

  mayai ni wa kuku wa kisasa. wale wa kienyeji nitaanza kuwafuga next year baada ya kukamilisha sehemu ya kuwaweka shambani.

  Note: nafugia Dar, maeneo ya bunju.
   
 2. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Poa mkuu
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  MKUU HONGERA SANA KWA JITIHADA ZAKO, MUNGU AKUSAIDIE ZAIDI NA ZAIDI.

  - KUHUSU BIASHARA YA MAYAI, NI KWELI KABISA KUNA DEMAND NA KUNA COMPETITION KUBWA SANA MKUU, WAZALISHAJI NI WENGI SANA NA MASOKO NAYO NI KAMA HIVYO NI MENGI.

  - MKUU UFANYE NINI SASA? NAKUSHAURI UFANYE JAMBO MOJA LA MSINGI SANA NA JARIBU KUJIBU HAYA MASWALI,

  1. JE KUNA KITU CHA ZIADA KATIKA HAYO MAYAI YAKO YAANI UMEYAONGEZEA THAMANI?
  2. JE WANUNUZI WAKO NI WA KUAMNIKIKA? MMENGIA NAO CONTACT NA KUSAINI MOU?
  3. JE KWA NINI WATU WANUNUE MAYAI YAKO NA SI MAYI YA WATU WENGINE?
  4. UKIPATA SOKO NA KUKAWA NA SUPPLY WENGI WA MAYAI YA KIENYEJI UTAWEZAJI KU KOMPITI NA HAO WENGINE?

  - MKUU JARIBU KUTAFUTA NJIA YA KUYAONGEZEA THAMANI HAYO MAYAI YAKO HASWA KWENYE PAKING. USIISHIE KUWEKA KWENYE TRY NA KWENDA KUTAFUTA MTEJA.
  - TAFUTA VIFAA VYA KISASA VYA KUPAKI MAYAI KIASI KWAMBA MTU ANAWEZA BEBA BILA KUHOFIA KUPASUKA KWA MAYAI.
  - UKISHA PATA PATA HIYO PACKING NZURI YA KUWEZA KUPAKI HATA MAYAI MATANO MATANO, JARIBU KUTAFUTA SOKO KWA KUZUNGUKIA SUPERMARKET MBALAMBALI NA MIN SUPRTPARKET PAMOJA NA MADUKA YA REJAREJA, MKUU NINA UHAKIKA ASILIMIA 100% UTAPATA SOKO ZURI SANA ENDAPO UTAKUJA NA AINA MPYA YA KUPAKI MAYAI,

  - WOTE TUSIISHIE KUPAKI KWENYE TRY YA MAYAI 30, TUJE NA AINA MPYA AMBAZO HATA HUKU KWETU SI NGENI SANA KWA SUPERMAKET KUBWA KAMA SHOPRITE,
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
  - MKUU JARIBU KUPAKI IDADI NDOGO NDOGO KAMA HII MAKE KUNA WATEJA HAWAHITAJI KUNUNUA MAYAI 30 TREI NZIMA KUTOKANA NA MAISHA YAO.

  - SI KWAMBA HAYA MADUKA MAKUBWA YA MAKUBURU HAYATAKI KUNUNUA PRODUCT ZA WABONGO ILA NI AINA YA PACKEGING ZOTE NDO TATATIZO.

  - TUNAISHIA KULALAMIKA KWAMBA WANAAGIZA MCHICHA TOKA SOUTH AFRICA, TUKIZANI TUNAWEZA WAPEKEKEA MCHICHA UKIWA UMEFUNGWA MAFUNGU MAFUNGU NA KAMBA ZA MIGOMBA WANUNUE.

  INATAKIWA TUBADILIKE HASA KWENYE PACKEGING ZETU, TUSIISHIE KULALAMIKA NYAMA INAAGIZWA TOKA SOUTH AFRICA, HAYA MADUKA YANA MAINTAI QUALITY HAYA WEZI ENDA BUCHANI PALE KARIAKOO NA KUNUNUA TU NYAMA NA KUPELEKA MADUKANI MWAO,

  MKUU HUO NDO MCHANGO WANGU,  [​IMG][​IMG]
   
 4. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
  nikitaka kununua mayai yako yote.....utaniuzia bei gan kwa tray? we ucpate tabu ya ku supply?
   
 5. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Kanyagio hongera, umejenga daraja na siye tunakuja kuvuka sasa hv...jamani nashauri tuanze kitengo cha agri marketing humu humu jamvini....a toast for our fellow kanyagio
   
 6. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Hii iko vizuri! Actually mimi nafuga wa kienyeji na nina mayai kiasi cha trei 1 kwa siku sina wateja. Bei yangu ni 12,000/- kwa trei. Bado suala la packaging ni issue kwangu kwani sijui nitapata wapi hizo trei ndogondogo
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu kwa huku bongo sijui kama zinapatikana, ila kwa nairobi kuna kampuni moja huwa inatengeneza hizo trey ndogo ndogo ngoja nikipata contact zao nitawawekea humu ili mkontact nao msikie wanasemaje.
   
 8. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  aisee kwa kweli nashukuru sana kwa ushauri wako.
  nitarudi tena kuandika kwa ufasaha zaidi kuhusu hoja zilizotolewa hapa
   
 9. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu komandoo big up sana! Post yako imetulia.
   
 10. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  hongera sana
  ni kweli sasa tunahitaji umoja ili kuweza kushika soko, kama uko bunju basi we nenda bagamoyo ulizia wakala wa mayai ya jumla huwa anachukua hata tray 300 na kulipa cash hapohapo ila nenda kaunge biashara kwanza usiende nayo, Tray zako unarudi nazo.

  Hizi tray ndogo zipo tayari ulizia tu, ukipata nenda supermarkets siku hizi nyingi tu watajie kiasi cha kuanzia tray 200 - 300 mfano kwa kila wiki nk kisha ulizia bei zao ila kwa hawa jiandae kuacha tray hapohapo.

  Waweza kwenda interchick pale ni mwezi uliopita walikutana wafugaji ila mie sikwenda nilibanwa kazini ukiomba kuonana na meneja kwa tip kidogo anaweza kukupa idea mbalimbali. Bei ninazojua ni 5500 hadi 5800 kwa jumla na 6000 rejareja kwa tray.
   
 11. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  nitakuuzia 5800 kwa tray
   
 12. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Unacho sema ni sahihi kabisa but ishu haiko katika kuungana tu. kama utakuwa umenisoma vema ni kwamba kilichopo ni kubadilika completery.

  - Hivi kama south africa wanauza mayai Tanzania je c c hata kuuza kwenye mikoa yetu mingine na hata nchi za jirani haiwezekani? Ni nini kinacho fanya isiwezekane?

  - KUHUSU HUYO MTU WA BAGAMOYO ANAE NUNU KWA BEI YA JUMLA HATA TREI 300 JE
  1. MNAKUWA MMESAINI NAYE CONTACT YA KUKULINDA WEWE NA KUMLINDA YEYE?
  2. JE UKIPELEKA SIKU USIMKUTE UTAFANYAJE WAKATI HUNA CONTRACT NAE?
  3 JE UKIPELEKA TREY 300 AKACHUA 10 TU UTAMFANYAJE?
  4. hilo soko unauhakika ni la kudumu? au ni mtu anajitokeza nakusanya wiki mwezi akishaona vipi anakula kona?


  - SIKILIZA NI LAZIMA TUBADILIKE, TUFANYE BIASHARA KISOMI, TUSIPENDE VITU VYA RAHISI SANA NA VYA SHORTCUT, MAKE WATANZANIA TUNAPENDA VITU VYA SHORT CUTSANA,

  - NI BORA UTUMIE MUDA MWINGI KUJIPANGA KUTAFUTA SOKO LA UHAKIKA NA UNAPO KUJA UNAKUJA NA SOKO LA UHAKIKA 100% SIO SOKO LA WIKI MOJA/MWEZI MMOJA HALA FU BAADAE UNAANZA HADITH ZINGINE,

  - MIMI NILIBAHATIKA KWENDA KENYA NA KUKUTANA NA BAADHI YA HATA WAZALISHAJI WA KUKU, MAZIWA NA MAZAO MENGINE, NI WAAMBIE UKWELI KENYA HAKUNA MTU ANE FANYA BIASHARA KAMA TUNAYO IFANYA SISI HUKU,

  - MKENYA UKIHITAJI KUFANYA NAE BIASHARA HATA YA KUSAMBAZIA TREI MOJA YA MAYAI KILA SIKU NI LAZAIMA MUINGIE NAE CONTRACT YA KUMLINDA YEYE NA YA KULINDA MTEJA WAKE. NA UKIKATAA KUNUNUA NAKUSHITAKI KWA KUMSABABBISHIA HASARA NA ANALIPWA, NA YEYE AKISHINDWA KUSUPPLY ANAWEZA SHITAKIWA VILE VILE

  HUU MFUMO WA BIASHARA TUNAO ENDA NAO SIO SUSTAINABLE HATA SIKU MOJA, NI WA MUDA TU, NA HAUTATUFIKISHA MBALI HATA SIKU MOJA, HIZO NI MIFUMO YA BIASHARA ZA MIAKA YA 90 KURUDI NYUMA.

  - na haya ndo mambo yanawaumiza hata wakulima wetu, jaribu kutafuta mnunuzi/wanunuzi wa uhakika na ingia nao contract kabisa na akikataa contact tanbua huyo ni msanii tu
   
 13. ANKOJEI

  ANKOJEI JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 701
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  mkuu komandoo mawazo yako ni mazuri sana bu kwa kuku 1000 inamana kwa cku ni mayai 1000x0.8= 800 minimum 80% wanataga kila cku yani tray 30, ambazo kama una soko la kawaida kat ya lile la uhakikia na lisilo la uhakika then izo value adding itakuwa gharama sana kwa mkulima mdogo. apo ni lazima tuchukue wazo la wakulima wadogo kuungana na kuwa na central packing place.
  Otherwise i have taken your point and i will make use of it as well as my business expands,
   
 14. blea

  blea JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nafurahi kupata maarifa zaidi kuhusu biashara hasa swala la kuwa na contact kwani kibongo bongo hili swala si wengi wanolifuatilia. KOMANDOO naona una ujuzi zaidi kwenye haya mambo naamini nitajifunza mengi hapa
   
 15. serio

  serio JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2015
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  mkuu bado unauza mayai? unauzaje kwa tray bei ya leo?
   
 16. C

  Cyan6 JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2015
  Joined: Aug 8, 2013
  Messages: 4,539
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi ninayo pia. Tray 5800 bei ya jumla
   
 17. serio

  serio JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2015
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  nakuja inbox
   
 18. C

  Cyan6 JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2015
  Joined: Aug 8, 2013
  Messages: 4,539
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkuu bado unanunua Mayai kwa jumla? Nina mayai mengi ya Kuku wa kisasa
   
 19. C

  Cyan6 JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2015
  Joined: Aug 8, 2013
  Messages: 4,539
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mbona sijakuona inbox?
   
 20. r

  reen elius em Member

  #20
  Feb 16, 2016
  Joined: May 17, 2014
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15

  bado unayo mayai hayo ya kisasa, unauzaje kwa tray kwa bei ya jumla?nilikua naitaji
   
Loading...