Soko la Karume haliwezi kubaki na mabanda ya mabati katikati ya jiji, Serikali ijenge soko la ghorofa kubeba machinga wengi

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,983
20,634
Nadhani Tume iliyoundwa isilegee kwenye hili, ipendekeze ijengwe ghorofa ambayo itabeba maelfu ya wamachinga, kuliko hali ya Sasa katikati ya Jiji Kuna mabanda ya mabati tu, ijengwe structure ambayo itabeba mambo mengi ikiwemo mabenki, mama lishe, maofisi, huduma mbalimbali.

Jengo hilo lijengwe ndani ya miezi 6 na wamachinga wakubali tu kukaa sehemu mbadala wakisubiri jengo liishe, waache ubinafsi pia, jengo jipya litabeba na wenzao wengi wanaopenda kufanya biashara mjini.

Serikali isikubali presha yao, majina yao yaorodheshwe, na wapewe kipaumbele pale jengo litakapoisha.

Vijengwe vizimba vidogo vidogo kwa ajili yao, na baadhi ya floor zipangwe shughuli nyingine, parking ya magari na stendi ya daladala ya kisasa.

Serikali iamue, ndio kazi yake, hata wakati wa vijiji vya ujamaa, serikali iliamua. Humo katika jengo ndio itakuwa mzizi mmoja wapo wa tatizo la chinga wanaokomaa kukaa kariakoo na posta. Chinga akipata Ofisi hapo na akashindwa kuinuka kiuchumi basi ana matatizo binafsi. Mkazo mkubwa uwekwe, wapewe chinga tu, sio wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa.
 
Mmewekewa la ghorofa 'machinga complex' ila hamtaki kulitumia, limejaa popo ndani

maajabu
 
Back
Top Bottom