Soko la Kariakoo nalo liuzwe kwa Mwekezaji Mzalendo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soko la Kariakoo nalo liuzwe kwa Mwekezaji Mzalendo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 17, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Shirika la Masoko ya Kariakoo linamilikiwa na Jiji la Dar (lenye asilimia 51) na serikali kuu (asilimia 49) - for the novices ni mgawanyo wa hisa kama uliokuwa kwenye Shirika la UDA. Kama UDA, SMK lilianzishwa mwaka 1974 chini ya Sheria ya Shirika la Masoko ya Kariakoo. Sheria hiyo ilifanyiwa mabadiliko mwaka 1985 (kuingiza mgawanyo wa hisa).

  Sasa taarifa mbalimbali zinaonesha kuwa shirika hilo lina hali mbaya ya kiuendeshaji na kifedha. Mojawapo ya matatizo yaliyopo yalionekana pale Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (inayoongozwa na Zitto) ilipowatimua viongozi wa "soko" hilo walipojitokeza mbele ya kamati hiyo mapema mwezi Juni mwaka huu. Kisa na Mkasa?

  Well, kama viongozi wengine wa mashirika ya umma waliitwa kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali kwa POAC lakini walipokuja "ikagundulika" kuwa wale waliokuja japo walikuwa wanatumia ofisi na vyeo vya shirika hilo hawakuwepo kwenye vyeo hivyo kihalali na Mamlaka yenye kuhusika na uteuzi wao (Rais kwa upande mmoja) ikiwa haijafanya uamuzi wowote kusahihisha.

  Kwa mujibu wa sheria hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo anatakiwa kuteuliwa na Rais na sheria iko wazi kabisa juu ya majukumu ya uongozi wa bodi. Kwa mfano Ibara ya 14:

  It shall be the duty of the Corporation to ensure that every specified market-
  (a) is kept clean and does not constitute a hazard to public health, safety or general welfare;
  (b) has an adequate supply of fresh water and, where possible, of electricity;
  (c) is managed in an efficient manner.


  Na kipengele (Ibara 23) kingine kinasema:

  23. The Minister shall as soon as may be practicable and not later
  and than twelve months after the close of a financial year, lay before the
  National Assembly the following documents in relation to such financial
  year-
  (a) a copy of the audited statement of accounts of the Corporation;
  (b) a copy of the auditor's report, if any;
  (c) a copy of the General Manager's report.


  Sasa shirika lina madeni na hali mbaya na yawezekana suluhisho laweza kuwa la kuliuza kwa wawekezaji wazalendo au wa kigeni? Je, Jiji la Dar liamue kuliachilia shirika hili na kuliuza kwa mwekezaji ili "liboreshwe" au pabomolewe na kujengwa jengo la kisasa la maduka, kuegesha magari n.k? au soko lenyewe lihamishwe na mwekezaji?
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  soko la kariakoo kuna mpango wa kuamishwa na kujengwa kinyerezi sijui kama litabomolewa na kujengwa mambo mengine pale
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  nipeni dili na mimi ninunue kwani nchi hii itaisha kuuzwa kabla mi mi sijapata kitu wakati ni yetu sote.
  kwani wanasema ni bei gani kaka mm?
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Poor Planning, Poor Management everything poor, poor, poor hakuna cha maana hata kama kuna tumaini lakini watu wanavizia vizia, ujanja ujanja mwingi hakuna uwazi kwenye inshu za public kama hapo.

  Hilo shirika lisingekuwa linaendeshwa kishikaji shikaji saizi tungekuwa na shopping Complex maeneo kama Mwenge, G/mboto, Tabata, Ubungo na Mbagala zinazofanana na Dar es salaam siyo kama saizi, hali inatisha sana watu ndo kwanza wanapiga politics za 2015 sijui lini watafanya kazi za kujenga taifa.

  Ukijichanganya ukaenda na gari kariakoo mida mibaya, unaweza kutamani kulia ni kero, usumbufu na kila aina ya khasia. Mimi kama mwananchi/mteja nahitaji mazingira salama, yenye kunivutia kwenda kufanya shopping zangu lakini kinyume na kariakoo, watu tunaenda tu kwa vile hakuna pakwenda.
   
 5. l

  lajabell Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  What do you intend to avail my dear brother MKJJ?!!!!
   
 7. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mzee MwanaKijiji suala hili litagua gumu maana bodi yao ilifukuzwa na kamati ya Bunge, huyo atakayelipwa pesa za mauzo ni nani? Maana za uda alipokea Iddi Simba? mtindo mpya wa malipo ya mauzo ya Mashirika ya Umma
   
 8. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Suluhisho sio kuliuza bali atafutwe mbia mwekezaji (wa ndani au nje) mwenye uwezo wa kuli-upgrade na kuliendesha kwa faida kwa maana lipo ktk sehemu nzuri sana/prime area pia eneo lililopo ni kubwa.
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Laki nane, lakini Muwekezaji amekwishapatikana
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Yanini kuuzwa? Na ligawiwe bure kabisa.
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu tujuze basi ni nani?
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  laki nane? are you serious?
  Ila naunga mkono lile soko liondolewe pale. it will good.
   
 13. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wangebinafisisha kwanza TABATA DAMPO.
   
 14. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mi sielewi hilo soko hua madeni linakopa ya nini maana haliitaji garama yoyote kujiendesha zaidi ya kusimamia uokotaji wa mapato kama ilivyo stand ya ubungo ambapo viongozi wa jiji wanapiga hela tu.

  Ishu hapa mzee mwanakijiji siyo kuuzwa kwa soko....ila ni kutafuta mtu ambaye anaweza kuokota mapato ya soko kwa mpangilio sahihi na kutumia hizo hela katika kuboresha miundo mbinu ya soko pamoja na kujenga other markets nje ya jiji ili kupunguza msururu wa foleni za kuta huduma sehemu moja.

  Serikali haina sababu ya kuendelea kushikilia uendeshaji wa vitu vidogo kama soko la kariakoo....kama iliweza kuuza TRL ambayo ni muhimili mkubwa wa uchumi soko wanashikilia la nini!!!!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Aug 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kama lisipouzwa ni mfumo gani mzuri wa kuliendesha? Au kwanini wasiliuuze kwa conglomerate ya makampuni ya wafanyabiashara wa Kitanzania?
   
 16. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,499
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  hii tabia ya kukubali kirahisi eti tumeshindwa! Tuliuze! Tunajenga ka utamaduni sugu kaajabu sana,tutauza mpaka familia zetu kwa mtindo huu wa "kushindwa"
   
 17. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,499
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  tunakubaliana na uzembe na kutokuwajibika kuwa ni "kushindwa" hilo neno kushindwa lina funika yote mpaka akili zetu! Uzembe tu hakuna justification.ufanywe uchunguzi wa sababu za failures then tuanzie hapo.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu chenye msamiati wa "Umma" kikafanikiwa. Ni moja katika madudu ya Nyerere.
   
Loading...