Soko la Hisa

hsankey

Member
Dec 30, 2015
33
47
Habari naombeni msaada mwaka jana nilinunua hisa TCC ambapo hisa moja ilikuwa elfu 16000 sasa imeshuka kwa kias kikubwa sana leo n sh 12000 ivi imetokana na nn ? na niziuze tu maana nilikuwa najipa moyo labda hazita endelea kushuka nisaidien nifanyaje plz
 
Hisa ni kama umeingia ubia(ushirika) na kampuni hio ya TCC ila katika biashara kuna miezi yake ya biashara na miezi mingine hupungua kwa sasa hisa nyingi hushuka sio TCC tu. Ushauri wangu angalia hio kampuni kama unahisi itafanya uzuri miezi au katika miaka 2 hadi 3 usiuze inawezekana ukapata faida baadae. lakini pia kama unaona haina uwezo wa kuendelea kufanya vizuri kwenye biashara basi ni bora kupata hasara ndogo kuliko kukosa kabisa.
 
Zimeshuka I think maybe b'se Serikali walitangaza kuuza hisa zao kweny TCC na TBL kipindi cha uchaguzi ambapo mpaka saivi za TCC bado hazijaisha(supply &demand law) ila za TBL ziliisha..TCC bado wako vizuri if u look at their balance sheet.so kuna good prospects ..saivi ndo Mda wa kununua TCC shares for those who have money b'se they are expected to appreciate soon
 
Hisa ni kama umeingia ubia(ushirika) na kampuni hio ya TCC ila katika biashara kuna miezi yake ya biashara na miezi mingine hupungua kwa sasa hisa nyingi hushuka sio TCC tu. Ushauri wangu angalia hio kampuni kama unahisi itafanya uzuri miezi au katika miaka 2 hadi 3 usiuze inawezekana ukapata faida baadae. lakini pia kama unaona haina uwezo wa kuendelea kufanya vizuri kwenye biashara basi ni bora kupata hasara ndogo kuliko kukosa kabisa.
Hivi unaweza ukakosa faida kabisa yaani ikabaki ile pesa yko ya uwekezaji tu ama maana siko deep sana kene hii issue
 
Mkuu hilo ni kweli mm mwenyewe nilinunua tbl tangu mwaka Jana mwezi Wa Tatu hadi naona azipandi vinginevyo ziporomoka kutoka 15000-14500 kwa kununua sasa sielewi inakuwaje mzigo unabaki stagnant nafikilia kuziuza aisee
 
mi ninatamani kununua hisa ila bado sijapata somo vizuri kuhusu soko la ila.I know nothing about hisa japo nasikiaga kuna faida
 
WATANZANIA wengi hatujui bishara ya hisa inaendeleaje... wajuzi njooni mmwage nondo humu
 
Ukiwa kama mwanahisa mpya kwa kuwa umenunua hizo hisa mwaka jana tu ni vyema ukahudhuria mkutano wa mwisho wa mwaka,Kwa kuwa wewe ni mmiliki wa TCC kwa kiasi cha hisa ulizonunua,utapata wakati mzuri wa kuihoji management team na board of Directors ni kwa nini hisa zinashuka.Utaweza pia kupata taarifa ya mwaka ya maendeleo ya kampuni ili uweze kuamua kama uendelee kuzishikilia hizo hisa au uuze. Kwa mtazamo wangu makampuni mengi yaliyoorodheshwa kwenye soko la Hisa la DSE, Hisa zimeporomoka kwa kiasi,Hii inatokana na wamiliki wa hisa kutaka kuuza zaidi ya wanaotaka kununua.Hata wewe ukitaka kuziuza hizo hisa ili upate wateja itakulazimu kupunguza bei,Lakini kama wewe ni mjasiriamali hasa ningekushauri ununue zaidi kwa kuwa ndio wakati wa kununua hizo hisa kwa kuwa zitapanda baadaye.
 
Hivi unaweza ukakosa faida kabisa yaani ikabaki ile pesa yko ya uwekezaji tu ama maana siko deep sana kene hii issue
Sio kukosa faida tu unaweza kukosa hata pesa yako yote ikiwa kampuni ita bankruptcy. Mfano mimi wewe na Richard tunanunua boti ya uvuvi wakati tunaanza biashara imeshamiri na samaki wengi tunapata na kuwauza hapa Hisa(faida) zetu zitakuwa juu. Sasa kunakuja kipindi cha masika mvua na upepo mwingi baharini samaki ni tabu kupatikana hapa tumepata hasara ya mafuta,mkopo wa benki tunakosa kuwalipa. Hapo ndio bank inasema inazuwia boti kutokana hatujalipa mkopo wa miezi miwili. kwahio hapo ndio unapokosa mpaka pesa zako za mtaji na mwisho wa hisa yako,yangu na richard.
 
USHAURI wangu kwa mtu anaetaka kununua Hisa.
(1) Jifunze kwanza kujua nini Hisa na ukishajua angalia kampuni ipi inafanya vizuri kwenye kipindi hangalau miaka 3.
(2) Usinunue na kudhani utakuwa tajira haraka ila kuwa mwenye uvumilivu wa muda hata miaka kadhaa
(3) Nunua ikiwa imeshuka bei na iuze wakati ikiwa imepanda bei utakapoiuza basi angalia upate japo asilimia 50% hadi 100% na kuendelea.
(4) Kabla hujanunua Hisa jaribu kwenda kwenye mikutano au wapigie simu kujua kampuni ipo katika shepu gani kama kuna bidhaa mpya au kitu kitakachoiwezesha kampuni kuendelea kufanya biashara kwa uzuri.
(5) Usinunue Hisa kama hujajifunza chochote juu yake na kufata ushabiki tu, Usikubali kuitupa ovyo pesa ulioitolea jasho. Bila ya kujifunza kuwekeza ni sawa na kuitupa pesa chooni. Lakini kama ushajifunza vya kutosha basi utapata mafanikio mazuri tu.
 
Back
Top Bottom