Soko la hisa toeni elimu Kuepusha kama mambo ya Desi na Mr. Kuku

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
221
431
Najaribu kujiwekea Akiba ya hivi visenti vyangu kwa kuangalia tofauti ya taasisi mbali mbali. Kitu kinachonishangaza ni kwamba utaratibu wa mamlaka kutoa elimu ya kwenye haya masoko ya hisa imekuwa mgumu binafsi nimekwenda zaidi ya mara kadhaa DSE na UTT ila kiukweli sijaelewa chochote mbaya zaidi mtu mwenyewe aliyekuwa ananielewesha anaonekana kama ana haraka na Kazi nyingi mpaka kufikia hatua ya kutoleana lugha kali

Hii inapelekea watu kutakuwa na uelewa na huduma zitolewazo na mashirika haya madhara yake ndio tunaangukia sehemu kama DECI ama MR KUKU mbaya zaidi hizi kampuni za watu binafsi huwa zina pata usajili kutoka katika mamlaka, kama DECI ilizinduliwa kabisa na aliyekuwa waziri wa fedha kipindi hicho ila baada ya watu kuweka akiba zao ndio tunasikia imefungwa na Serikali, kwa kosa la kuchezesha upatu.

Hizi stock exchange market zingekuwa zinatoa elimu ya kutosha na hizi kampuni za watu binafsi zinachozesha UPATU zingenyimwa usajili hii ingesaidia watu kutotapeliwa akiba zao.
 
Kesho Nimesikia Waliopigwa Na Mr Kuku Wanataka Kuandamana Kuomba Huruma Ya Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Ili Warudishiwe Chao Halafu Mr Kuku
Aendelee Kupambana Na Hali Yake
Tanzania Watu Tunapenda Slope Sana, Yaani Uwe Jero Upate Buku


Ndiyo Maana Hata Elimu Ikitolewa Bado Wanaopenda Slope Utawakuta Wakiambizana Twende Kwa Mr Kuku


Tunategemea Kutakuja Jambo Jingine Jipya Utawakuta Wamejaa
 
Nakushauri ujisomee mwenyewe kutoka vyanzo tofauti ili ukienda huko uwe tayari na uelewa kiasi. Vinginevyo hutoweza kuwaelewa kwa urahisi.
 
Serikali imemuonea sana mr kuku. Watanzania ni wavivu wanapenda starehe na mafanikio makubwa ya haraka. Acha wapate hasara.

Miaka 4 ijayo nitaanzisha Penzi scheme yangu nipige hela, ikifika Billioni 3 nahama nchi.
 
Huko mkuu huu ndiyo wakati wa kununua hisa, ila research kampuni potential upate maono, miaka 10 ijayo ule faida..

Soma, na uwekezaji ufikirie uwe wa muda mrefu miaka mi5, siyo miezi 6, usepe...hakusomeki!

Hisa za kampuni nyingi tunaojaribu kuuza haziuziki..
Precisionair makaratasi yamejaa vumbi, hakujawahi kuwa na gawio wala uwezekano wa kuuza...
Swissport walikuwa na magawio, yameyeyuka...
NMB wanatoa magawio hisa haziuziki, inachosha sana!

TMRC wakija na bonds kachukue...wana terms nzuri.

Huko UTT binafsi nilishaondokaga, nilichukua changu mapema..
Wao wanawekeza huko huko kwenye makampuni ya hisa! Walikuwa vizuri, ila na huu upepo wa Covid sijui..

Kila la heri...

Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Kununua Hisa za Tanzania ni Bora ufugie kuku.

Ushindwe kununua Hisa za LSE au NYSE unaenda kununua Hisa za DSE huu ni ukichaa .. Yani Dunia nzima ilivyo mitandaoni unashindwa kununua hata Hisa za Facebook au Boeing au Manchester United unakuja kununua Hisa za Vodacom.
 
Kununua Hisa za Tanzania ni Bora ufugie kuku.

Ushindwe kununua Hisa za LSE au NYSE unaenda kununua Hisa za DSE huu ni ukichaa .. Yani Dunia nzima ilivyo mitandaoni unashindwa kununua hata Hisa za Facebook au Boeing au Manchester United unakuja kununua Hisa za Vodacom.
Mkuu hebu tusapoti. Lazima tupate mitaji ili tuwe Kama Manchester na Boeing. Wachina wameweza na sisi tunaweza kabisa tusaidiane tu
 
Mkuu hebu tusapoti. Lazima tupate mitaji ili tuwe Kama Manchester na Boeing. Wachina wameweza na sisi tunaweza kabisa tusaidiane tu
Mkuu watu tulinunua Hisa za voda Leo unaona hata aibu kuzichungulia.


Ubepari hauna Mambo ya uzalendo. Ubepari ni faida na soko huria. Ndio maana ukiwa na huduma mbovu mtu anaenda kununua Kitu nje ya nchi. Kuna nyama ya ng'ombe wa singida ila mtu anaagiza ng'ombe kutoka uarabuni. It's all about good offered service.


Wasijikite kwenye masuala ya uzalendo , wao waweke mazingira mazuri ya watu kupata faida na sio mtu aweke hela Yake halafu mwisho wa siku anapata hasara kwa justification ya uzalendo.
 
Back
Top Bottom